Kanali mstaafu wa JWTZ analipwa Pensheni 22,000/= na Jenerali analipwa 50,000/=

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,223
1,670
Kanali mstaafu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Ameen Kashimir, ameilalamikia serikali kwa kutotambua mchango wake licha ya kuinusuru serikali wakati wa maasi ya jeshi hilo ya mwaka 1964.

Kadhalika, alisema pamoja na mchango wake kwa taifa mpaka sasa analipwa Sh. 22,000 kwa mwezi kama mafao ya uzeeni.

Kashimir ambaye alikuwa afisa wa kwanza kupata Kamisheni Jeshi la Tanganyika Rifles, kabla ya uhuru na baada ya uhuru, alikuwa Mnadhimu Mkuu wa kwanza wa jeshi hilo ambaye alifanya mambo mbalimbali ikiwemo kuwafundisha wanajeshi 30,000 kwa ajili ya kuanzisha jeshi jipya.

Hayo aliyasema jana jijini Dar es Salaam wakati alipohojiwa na waandishi wa habari wakati wa uwasilishwaji wa video kuhusiana na historia ya maisha yake.

Alisema mchango wake katika jeshi umesahaulika licha ya kwamba umesaidia kujenga msingi wa jeshi kutoka askari 50 waliobakia baada ya waasi na kuanzisha jeshi jipya la wanajeshi 30,000.

Alisema jeshi hilo lilikuwa imara na lilionyesha uhodari wake katika vita dhidi ya Idi Amini wa Uganda.

Kashmir alisema, yote waliyoyafanya yamesahaulika. "Kwa mimi binafsi nilibaki na cheo cha Kanali wakati nilitakiwa kuwa Meja Jenerali sasa hapa labda kulikuwa na ubaguzi wa aina fulani au sijui ni nini lakini nadhani serikali inatakiwa kuangalia suala la maofisa wa zamani."

"Kwa mfano Jenerali Mstaafu Mrisho Sarakikya mafao anayopata ni Sh. 50,000 kwa mwezi na mimi napatiwa Sh. 22,000 na kama nisingekuwa na akili timamu na nguvu ningekuwa maskini na kuomba omba," anasema.

Aliomba serikali ifikirie upya waliojitolea na kusaidia kujenga jeshi linaloonekana sasa wakumbukwe katika michango yao.

Aidha, alisema vijana wanatakiwa kuiga mfano wao kwa kuwa walikuwa ni wazalendo na nchi yao.

Alisema kuonyeshwa kwa video hiyo kutasaidia vijana kuelewa kazi walizokuwa wakizifanya katika kujenga nchi.

Alilishauri jeshi kuwa la kisasa lenye silaha za aina mbali mbali zinazotumia teknolojia mpya.

Kwa upande wake, Mhadhiri wa chuo kikuu, Profesa Issa Shivji, alisema mchango wa mtu binafsi unakumbusha suala la historia na kwamba ni jambo zuri kukumbukwa kwa Kanali Kashmir kwani baada ya kutokea waasi wa jeshi mwaka 1964 ni nchi pekee Afrika ilivunja jeshi lake na kuunda jeshi jipya.

Alisema hatua hiyo ni muhimu kwa upande wake kwa kuwa ilikwenda sambamba na kizazi kile kujenga utaifa.

Profesa Shivji alisema wanapoangalia michango ya watu wanatakiwa kujikumbushia historia zao kwani ilikuwa na dira kwa nchi hivyo ni muhimu wakakumbukwa.

CHANZO: NIPASHE
 
Duuh, very sad jamani!!!!! Major generali analipwa 50,000tshs��

Jeshini siendi bora nipige biashara zangu.
 
Chili jambo la mafao ya uzeeni kwa wastaafu wa kada mbalimbali waliotumikia taifa kwa miaka ya zamani linapaswa kuangaliwa tena kwa umakini.

Viwango hivyo vya fao la uzeeni haliakisi viwango vya maisha vya sasa.
Viwango hivyo vilikokotolewa zamani, mazingira ya uchumi kipindi hicho ni tofauti sana na sasa.

Serikali ikokotoe mafao hayo kwa kuzingatia mazingira ya kiuchumi ya sasa, kama mfumuko was being(inflation rate) na viwango vya riba n.k

Poleni sana wazee wetu.
 
Duuh, very sad jamani!!!!! Major generali analipwa 50,000tshs��

Jeshini siendi bora nipige biashara zangu.

..wanajeshi wastaafu kuanzia Brig.Gen wana mafao mengine mazuri.

..kwa uelewa wangu jeshi linaendelea kuwahudumia kwa masuala kama chakula, usafiri, na matibabu.

..labda Col.Kashmiri anaona alistahili kuwa Jenerali na siyo kuachwa akastaafu kama Colonel.

cc Echolima, Kichuguu
 
Last edited by a moderator:
Ehhhh us dollars Ama madafu? Nimesoma heading tu!!!weekend mood IPO ON baada ya kumaliza kikao kawe!!!
 
hii habari ilinishtusha sana sikuamini kwenye masikio yangu,hivi ni kweli ss ni masikini kiasi hicho cha kushindwa kuwalipa wanajeshi wetu wastfu kwa kiwango hicho? alfu tunapiga kilele tunahitaji amani kweli?
 
Inapofikia mahali hapo mimi naumia sana maana wanajeshi wastaafu karibu wote sasa hivi wanaishi maisha ya ombaomba au kulinda kwenye maduka ya watu binafsi.Hii inatutia aibu sana ni kweli Kashmir amesema kweli hii elfu Hamsini serikari yetu imeamua tu kutudhalilisha mitaani lakini ikumbukwe sisi tumetoa mchango mkubwa sana kwa nchi yetu wengine tumeshiriki vita na operation kadhaa za kuhatarisha maisha yetu lakini ni ajabu sana serikali hii umetufanya kama USED-TOILET PAPERS Inauma sana sana.
..wanajeshi wastaafu kuanzia Brig.Gen wana mafao mengine mazuri.

..kwa uelewa wangu jeshi linaendelea kuwahudumia kwa masuala kama chakula, usafiri, na matibabu.

..labda Col.Kashmiri anaona alistahili kuwa Jenerali na siyo kuachwa akastaafu kama Colonel.

cc Echolima, Kichuguu
 
Last edited by a moderator:
Mimi bado sijakuelewa unaunga mkono hiyo 50,000/kwa wanajeshi waliostaafu au vipi????
Kweli nimegundua JF ina watu wengi vilaza!

Yani hata kujua namna mafao yanavyo kokotolewa hamjui?

Ninyi ni watu gani!?! Makondakta au ndio maBAVICHA yenyewe haya?

Kwa ufupi, huyo mwanajeshi anapewa hiyo pesa ya mafao kulingana na mshahara wake wa kipindi hicho. Pesa yake haijapatiwa thamani ya pesa ya sasa na ndio maana anapatiwa kaisi kidogo cha pesa. Kwa kuwa hiyo ndio michango yake. Hana wa kumlaumu hapo.

Kwa wanajeshi wa sasa, mfano Brigedia, ambao wanakula mishahara mpaka milioni 7 (inategemea na factors mbalimbali) kwa maana vyeo vinaweza kuwa sawa ila maslahi tofauti kabisa. Hawa wakistaafu mafao yao sio mchezo! Kwanza ile lump sum tu inaweza kuwa Milioni 300! Na hata yale mafao ya kila mwezi yanakuwa mazuri pia.

Ni suala la wakati tu. Nashangaa vikaza humu wanaosema eti jeshini hakuna maslahi!
 
haha..wamezoea danganyaika na biana nyama pori wanazopewa kila wiki kwa kutumiwa vijana wakapige wanyama wetu.Ndio wafunguke akili wajue kuna tofauti ya kuw amzalendo kwa ccm na kuwa mzalendo kwa taifa.Waisubiri sana ccm pengine atapewa ukuu wa wilaya za mipakani si huwa wanapeleka wanajeshi..Burundi waeshaanz apika issue.
 
Acha kupotosha.Angekuwa anatamani cheo kwanini amsemee Mrisho Sarakikya mwenye hicho cheo unachomaanisha?
Elfu 50 kwa meja jenerali?
Wakati fisadi linatumia milioni 10 kwa ajili ya mboga tu? Hii nchi imefikia kwenye U-turn.
..wanajeshi wastaafu kuanzia Brig.Gen wana mafao mengine mazuri.

..kwa uelewa wangu jeshi linaendelea kuwahudumia kwa masuala kama chakula, usafiri, na matibabu.

..labda Col.Kashmiri anaona alistahili kuwa Jenerali na siyo kuachwa akastaafu kama Colonel.

cc Echolima, Kichuguu
 
Last edited by a moderator:
Kashmir alisema, yote waliyoyafanya yamesahaulika. "Kwa mimi binafsi nilibaki na cheo cha Kanali wakati nilitakiwa kuwa Meja Jenerali sasa hapa labda kulikuwa na ubaguzi wa aina fulani au sijui ni nini lakini nadhani serikali inatakiwa kuangalia suala la maofisa wa zamani."

cc pepsin
 
Last edited by a moderator:
Inapofikia mahali hapo mimi naumia sana maana wanajeshi wastaafu karibu wote sasa hivi wanaishi maisha ya ombaomba au kulinda kwenye maduka ya watu binafsi.Hii inatutia aibu sana ni kweli Kashmir amesema kweli hii elfu Hamsini serikari yetu imeamua tu kutudhalilisha mitaani lakini ikumbukwe sisi tumetoa mchango mkubwa sana kwa nchi yetu wengine tumeshiriki vita na operation kadhaa za kuhatarisha maisha yetu lakini ni ajabu sana serikali hii umetufanya kama USED-TOILET PAPERS Inauma sana sana.

..inaanzia kule ambako tumekuwa tukisema mara nyingi.

..hata habari/historia za yale mliyoyafanya mnazificha-ficha.

..nyinyi wenyewe mngekuwa mstari wa mbele kuielimisha jamii kuhusu kile mlichokifanyia taifa hili, serikali na CCM wasingewadhalilisha kiasi hicho.

..yaani mimi kila nikiona shamra-shamra za sikukuu za mashujaa za nchi nyingine nabaki kuisikitikia nchi yangu na watu kama nyinyi mliojitolea mhanga ili sisi wengine tuishi kwa raha zetu, na hata wengine kufanya ufisadi.

cc pepsin
 
Last edited by a moderator:
Wanajeshi na nyie acheni starehe, mkipata mshahara wekeni akiba,na nyingine wekezeni,tatizo wanajeshi wengi wanaendekeza pombe tu na starehe,wakistaafu wanaishia kuwa omba omba
 
Kweli nimegundua JF ina watu wengi vilaza!

Yani hata kujua namna mafao yanavyo kokotolewa hamjui?

Ninyi ni watu gani!?! Makondakta au ndio maBAVICHA yenyewe haya?

Kwa ufupi, huyo mwanajeshi anapewa hiyo pesa ya mafao kulingana na mshahara wake wa kipindi hicho. Pesa yake haijapatiwa thamani ya pesa ya sasa na ndio maana anapatiwa kaisi kidogo cha pesa. Kwa kuwa hiyo ndio michango yake. Hana wa kumlaumu hapo.

Kwa wanajeshi wa sasa, mfano Brigedia, ambao wanakula mishahara mpaka milioni 7 (inategemea na factors mbalimbali) kwa maana vyeo vinaweza kuwa sawa ila maslahi tofauti kabisa. Hawa wakistaafu mafao yao sio mchezo! Kwanza ile lump sum tu inaweza kuwa Milioni 300! Na hata yale mafao ya kila mwezi yanakuwa mazuri pia.

Ni suala la wakati tu. Nashangaa vikaza humu wanaosema eti jeshini hakuna maslahi!
He ka hiyo wew unaa 22,000na haa 50,000.0 kwa mwezi mind you sio wa siku ni sawa?
 
Back
Top Bottom