Shigganza
Senior Member
- May 24, 2018
- 160
- 412
Kampuni ya uchimbaji madini ya Barrick Gold Corporation ambayo ni mwekezaji katika Migodi ya Bulyanhulu na North Mara kwa Ubia na Accacia imetangaza nia ya kununua hisa za kampuni ya Acacia kwa gharama ya dola za Marekani milioni 787.
Uamuzi wa Barrick unafuatia kampuni ya Acacia kutotoa ushirikiano kwa Barrick dhidi ya makubaliano ambayo imeafikiana na Serikali ya Tanzania kupitia kamati za majadiliano. Kutokana na kukosekana kwa ushirikiano huo, Barrick ambayo inamiliki kiwango kikubwa cha hisa ambacho ni theluthi mbili imeamua kununua hisa zote za Acacia ili kuiwezesha kuwa na umiliki kamili wa Migodi hiyo.
NIni kitatokea baada ya Barrick kununua hisa za Acacia? ni wazi kuwa kampuni ya Barrick itaweza kutekeleza makubaliano iliyoingia na Serikali ya Tanzania mara moja kwani kwa muda huu wote Acacia imekuwa kikwazo kikubwa.
Kwa minajili ya rejea tembelea https://www.miningweekly.com/articl...tanzania-refuses-direct-settlement-2019-05-22