Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Kampeni zamngoa Mkurugenzi Arusha
Harakati za uchaguzi mkuu jimbo la Arusha, sasa zimechukua sura mpya baada ya kuhamishwa ghafla Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Raphael Mbunda katika mazingira yanayohusishwa na siasa.
Mbunda, mmoja wa wakurugenzi wa muda mrefu nchini, amehamishwa ghafla kwenda ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na amepewa siku tatu tu kuachia ofisi yake kinyume na taratibu za serikali za kupewa siku 14 kujiandaa kuondoka.
Hata hivyo, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais tawala za Mikoa (TAMISEMI), Selina Kombani aliliambia gazeti hili kuwa uhamisho huo kuhusishwa na siasa akisema ni uhamisho wa kawaida.
Uhamisho huo ni wa kawaida kama wengine wanavyohamaishwa kwa hiyo sioni kama ni habari, alisema Kombani.
Alifafanua zaidi kuwa Mbunda hana tatizo lolote linalohusiana na uhamisho huo na kwamba atapangiwa kazi nyingine nzuri.
Hata hivyo baadhi vyanzo vyetu ndani ya manispaa hiyo vinaweka wazi kwamba uhamisho huo unatokana na vuguvugu la kisiasa.
Jambo hili ni la ajabu sana hata kama mtu ana makosa si anaheshima yake. Mbunda amekuwa Arusha muda mrefu kabla ya kuwa Mkurugenzi katika halmashauri mbalimbali halafu wanamhamisha kama mwizi Hii sasa inatufikisha wapi, alisema mtumishi mmoja wa Manispaa ya Arusha kwa sharti la kutotajwa gazetini.
Mkurugenzi huyo, katika siku za karibuni, alitupilia mbali mapingamizi ya kumuondoa mgombea wa Ubunge wa Chadema jimbo la Arusha, Godbless Lema kwa tuhuma za kumchafua na kumdhalilisha mgombea wa CCM.
Habari za uhakika kutoka ndani ya halmashauri za Arusha zimebainisha kuwa nafasi ya Mbunda sasa inachukuliwa kwa muda na na ofisa kutoka ofisi ya mkoa wa Arusha, Estonmi Changah ambaye alikuwa idara ya serikali za mitaa ..
Habari zaidi katika Mwananchi Jumapili
My take: Hivi Tume ya Uchaguzi iliafiki kuhamishwa huyu? Ilishirikishwa katika uteuzi wa huyo mwingine? Ingefaa Makame aulizwe, na akubali kuwa wasimamizi wake wa uchaguzi ni makada wa CCM na kwamba serikali ya CCM inaweza kuwafanya wanavyotaka iwapo itaona inaelemewa sehemu fulani fulani.
Aidha Chadema inapaswa ilalamikie hili ikiwa ni pamoja nakwenda mahakamani kupinga.
Mbona hivi jamani demokrasia ya akina JK ina uminywaji wa waziwazi dhidi ya upinzani ili ishinde kwa kishindo?