nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
*Yagomea bajeti Wizara ya Miundombinu
*Yadai imeshindwa kufufua TRL, ATCL
Na Dunstan Bahai
KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imetishia kutoipitisha bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa madai kuwa wizara hiyo imeshindwa kuwekeza kwenye mashirika nyeti ambayo ni mhimili wa nchi.
Mashirika hayo ni Shirika la Reli Tanzania (TRL), Shirika la Ndege la Taifa (ATCL) na Bandari.
Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya majadiliano ya asubuhi ya kamati hiyo, Mwenyekiti wa kamati, Bw. Peter Serukamba alisema serikali imekuwa na matumizi mengi yasiyo ya lazima lakini imeshindwa kuwekeza katika mashirika hayo na kusababisha kuelekea kufa.
"Serikali na wizara kwa ujumla inatakiwa kuweka kipaumbele kwanza kwa mashirika haya. Haya mashirika ndiyo uti wa mgongo wa uchumi wa nchi, ukisema unawekeza kwenye kilimo kwanza, huwezi kufanikiwa kama huna miundombinu bora," alisema.
Alitoa mfano kuwa ATCL ili iweze kufanya shughuli zake kwa ufanisi inahitaji sh. bilioni 23 tu wakati serikali imelaumiwa kwa kushindwa kuilipia gharama za matengenezo ndege moja iliyopo Afrika Kusini ya shirika hilo, deni la sh. bilioni moja tu.
Aidha TRL nayo inahitaji sh. bilioni 241 kulifufua shirika hilo.
"Wanaosema serikali haina fedha siwaelewi, imekuwa na matumizi yasiyo ya lazima na kushindwa kutoa fedha kwenye maeneo ambayo yanachangia uchumi wa nchi. Lazima mashirika haya yapewe fedha vinginevyo hatuipitishi bajeti hii," alisema.
Kwa mujibu wa Bw. Serukamba, Wizara ya Uchukuzi kwenye bajeti yake kwa fedha za ndani ilikuwa sh. bilioni 95 lakini ambazo wizara imepewa ni sh. bilioni 45 tu wakati za wahisani zilikuwa ni sh. bilioni 65, lakini zilizopatikana ni sh. bilioni mbili tu.
Kutokana na mazingira hayo, alisema wizara haiwezi kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Mjumbe wa kamati hiyo ambaye ni Mbunge wa Tunduru (CCM) Bw. Mtutura Mtutura alisema serikali inachokosea haitengi vitu ambavyo ni vya kipaumbele.
Alisema kwa wakati uliopo sasa bandari ndogondogo sizitiliwe umuhimu kwani hazichangii uchumi wa nchi kwa kiasi