Kamati kuwafuata Wazanzibari waliokimbilia Somalia

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

[FONT=Arial, Helvetica, sans-serif]
[/FONT]
Saturday, 26 November 2011 08:47

Keneth Goliama

KAMATI ya kutathmini wakimbizi waliokimbilia Somalia baada ya vurugu za uchaguzi Zanzibar mwaka 2001, imeanza kuundwa ili kuwarejesha nchini.

Wajumbe wa kamati hiyo wanatoka taasisi mbalimbali; Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi (UNHCR), Ofisi ya Rais na Idara ya Uhamiaji Tanzania.Hatua hiyo inatokana na baadhi ya Watanzania 21 waliokimbilia Somalia wakati wa vurugu za uchaguzi Zanzibar Januari 26 na 27, 2001 kufikia 81.Hivi sasa wanaishi kambi za wakimbizi nchini Somalia.

Kaimu Msemaji wa Idara Uhamiaji, Tatu Burhani, alisema kuna mipango inayoendea kusukwa na kwamba, kamati itaondoka wiki ijayo.Burhani alisema kamati maalumu itakayokwenda Somalia kuwafanyia uchunguzi wa Watanzania hao, itawakilisha mashirika mbalimbali ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Alisema kutokana na Waziri wa Mambo ya Ndani, Shamsi Vuai Nahodha, kuagiza mchakato huo wa kuunda kamati kwenda kufanya utambuzi, zoezi hilo linafanyika haraka ili kuwarudisha nyumbani.

Burhani alisema tayari mchakato huo umefanyika, kwani hadi sasa mikakati yote imefikia mwisho na kamati hiyo inaweza kuondoka wiki ijayo.Watanzania hao wameishi miaka kumi nchini Somalia na kwamba, tayari wengine wameoana na kuolewa hadi kufikia zaidi ya 81, kutokana na ongezeka hilo Tanzania imeona bora kuwarudisha nchini wale watakaokidhi vigezo.

“Kamati hiyo itafanya kazi ya kwenda Somalia kuwatathmini Watanzania, lakini watoto kwa mujibu wa sheria za kimataifa wana uraia wa nchi mbili, wana uhuru wa kuamua. Hivyo cha msingi ni kuwafanyia tathmini wale wanaozidi miaka 18,” alisema Burhani.

Katika vurugu za Januari 26 na 27, 2001 zilizotokana na Chama cha Wananchi (CUF), kutokubali ushindi wa mgombea wa CCM, Amani Abeid Karume, zilisababisha zaidi ya watu 30 kuuawa na wengine kukimbilia kambi za wakimbizi, Dadab na Kakuma nchini Kenya, huku wengine wakiamua kwenda Somalia.
 
Sasa hapo ni hatari ndio hao waliojiunga na Al - Shaahab?

Kitu kinachonisikitisha ni kuwa sasa Viongozi wetu wa kiislamu wanatutisha kuwa tusizungumzie Masuala mabaya kuhusu Uislamu; ni tangu lini sisi watanzania tunafanya Mambo hayo?

Ni kwanini tunakuwa na chuki kiasi hicho? Baba Muislamuyangu alikuwa mtanzania na alikuwa na kabila alimpenda mama yangu ambaye ni Mkristo yaani maishani mwangu sikusikia wakigombana kuhusu Udini, wote walikuwa wasomi walijali haki na maendelea kwa watanzania wote...

Leo hii kila kusemwacho ni chunga usizungumzie Uislamu, Chunga usiwaseme vibaya... Yemeni ni nini huko? Syria ni ya nini huko?
 
kama ukifanikiwa kwenda nchi kama saud arabia ndiyo utaona utofauti kati ya waislamu wa huku na kule
 
Wengi ya Wananchi Raia wa Saud Arabia hawafanyi kazi; Wanalipwa kwa Mwezi Stipend...

Wafanyakazi wengi ni toka India, Bangladesh, Nepal na domestic servants toka Kenya, Tanzania wanateswa haswa bora utumwani

Wauaji wa NY zaidi ya nusu walitoka Saud Arabia sasa niambie tofauti yao iko wapi? na Mapesa yote waliyonayo?
 
Wengi ya Wananchi Raia wa Saud Arabia hawafanyi kazi; Wanalipwa kwa Mwezi Stipend...

Wafanyakazi wengi ni toka India, Bangladesh, Nepal na domestic servants toka Kenya, Tanzania wanateswa haswa bora utumwani

Wauaji wa NY zaidi ya nusu walitoka Saud Arabia sasa niambie tofauti yao iko wapi? na Mapesa yote waliyonayo?

Deceived or progrmmed mind..

Jisomee mkuu siyo kila kitu unayoambiwa kanisani na CIA ni kweli

Elimu itakusaidia kupambanua kati ya appearance and realities..
 
Deceived or progrmmed mind..

Jisomee mkuu siyo kila kitu unayoambiwa kanisani na CIA ni kweli

Elimu itakusaidia kupambanua kati ya appearance and realities..

Nimeishi Saud Arabia ndugu yangu siongelei ya kuambiwa
 
Sasa wakuu mbona mnaacha kujadili hoja ya msingi mnajadili mambo ya saudia? Kimsingi wakimbizi hao wa kizanzibari wamesalitiwa na cuf.hakuna cha duni haji wala mtatiro wote ni wasaliti
 
Back
Top Bottom