Kamata kamata inayoendelea ni maazimio ya Kina Kinana na viongozi wa CCM baada ya kushindwa siasa za majukwaani; ogopa kukataliwa

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
877
4,106
Viongozi wote wa CCM wameamua kurudi na kukaa ofisini baada ya kuona kila wanapopita kutetea DP world mambo yanavurugika.

Soon after kusarenda wameshauri turudi kwenye mfumo wa Magufuli; lakini pia pressure ya kisiasa iliyopo Afrika kaskazini na Magharibi inatoa piacha kwamba siasa za kidemokrasia siyo mtaji tena.

Kinana ameanza kumwishtaki Kubenea yeye na JK na since day walipojitokeza tu kamata kamata imeanza rasmi.

Jambo la pili, bunge linategemea kupitisha mabadiliko ya sheria ya rasilimali; ili kupunguza kelele lazima wanaopiga kelele wawe ndani hadi kazi uishe.

Katika kuthibitisha ili utaona Diamond amerejeshwa kutoka Rwanda kuja kupambana jukwaani na Chadema jambo ambalo usingelitegemea kwa viongozi ambao wanaamini wanayofanya yana maslahi kwa Taifa.

OPERESHENI ya Chadema kanda ya ziwa imekuwa mwiba mkali kuonyesha kwamba hali hiyo isipodhibitiwa hawa wananchi wakiwemo wa CCM wataendelea kuikataa serikali. Kukamata wachache kunasaidia sana jamii kuendelea kushabikia muziki na mpira kuliko kushabikia siasa.

Mwisho namwona pia Dr. Slaa akiingia maabusu pamoja na Tibaijuka kwa sababu wao wamekuwa vinara wa mabadiliko.

Kinana alipoona hali ni mbaya majukwaani alidiriki kutaka kuwakumbusha Chadema kwamba awakukukubaliana wafanye siasa za kukosoa majukwaani na kwamba wasitoe siri.....ile kauli haikuwa ndogo .ni matokeo ya mtu aliyeamini amekunyamaz8sha kumbe amekupa kick upige kelele zaidi.

Changamoto ya kamata kamata ni moja tu; wapinzani watapoteza na serikali itapoteza. Hakuna mafanikio yanayolindwa na dola kwa gharama ndogo ..mafanikio haya yanatumia gharama kubwa zaidi ikiwemo kujilazimisha KWENDA KWA MABEBERU KILA WAKATI KUWAELEZA KWAMBA NCHINI KWAKO KUNA AMANI. Tunarudi kule kule kwa wageni kubembelezwa waje kuwekeza badala ya kuandaliwa mazingira wasione fursa na kuja kwenye bergaining
 
Back
Top Bottom