Kama Yesu angezaliwa na kumtumikia Mungu zama hizi za leo maana yake angefungwa Segerea nasio kutundikwa msalabani.

Sa 7 mchana

JF-Expert Member
Dec 30, 2018
4,975
9,723
No OFFENCE NO OFFENCE


Naomba mada isichukuliwe tofauti na pia niweke bayana baadhi ya mambo. Kwanza mimi ni mbatizwa kwa Jina la Joseph ( na sijui kwa nini sisi wenye majina yetu asili uwa tunapewa majina mengine, sitaki kuamini kama Mungu ni mbaguzi kiasi icho).

Nilibatizwa mpaka kupata kibaimala katika Moja ya Parokia kongwe Tanzania Bara.

Baada ya kusema hayo naomba itambulike kuwa mada hii imeletwa na mtu kutoka ndani nasio kama ilivyozoeleka.


Nimefuatilia historia ya adhabu kwa mababu wa kizungu, nimefanikiwa kujua namna tofauti tofauti ambazo miaka hiyo walikua wakitumia kuwaadhibu wahalifu wa namna tofauti tofauti.

Hata biblia inaeleza kuwa Yakobo alikatwa kichwa, Yesu na wenzie walisurubiwa na wamo waliopigwa mawe mpaka kufa bila kusahau wapo waliotupwa kwenye mashimo marefu.
images (5).jpeg


Lakini pia mengi yanazungumzwa Paulo na sila walifanya prison break kwa maombi na mengi kadhalika.

Kinachonekana mababu wakizungu walikua na bufee ya adhabu, yani walikua na option nyingi kinoma za kuhakikisha mtenda anapewa stahiki yake baada ya kukengeuka taratibu walizokua wamejiwekea. Ila hii ni wazi ipo tofauti kabisa na leo Ikiwa na maana kwamba kuna machaguo machache sana ya mtu kuadhibiwa pale anapokua amevunja sheria.

Adhabu ambayo inatumika kwa wingi ni kuwekwa kifunguni( gerezani).

Basi iyo ilitosha mimi kuona kwamba endapo Yesu masia angezaliwa zama hizi na kuhuduma maanake angewekwa ndani nasi kutundikwa msalabani, yote hayo ni kwa sababu kutundikana msalabani si adhabu za kipindi hiki.

images (2).jpeg


Baada ya kuwaza hayo nikajakuona kuwa mambo mengi yangebadilika ikiwemo alama ya Ukristo. Isinge kuwa tena msalaba ingebadilika na kuwa picha ama taswira ya GEREZA.

Sasa can you imagine Padre inasalisha huku nondo za GEREZA zimening'iniza kifuani.😂🤣😂

Na wala kusingekuwa na ishara ya msalaba tena, tumepata ishara ya GEREZA dah sijui ingekuwaje 😂🤣😂 Naona mambo yamekua mengi au basi.



images (4).jpeg


images (1).jpeg
 
Back
Top Bottom