Kama unataka kufanikiwa na kuwa tajiri, acha tabia hizi...

Kila tumizi lako liandike kwenye diary yako.
Hakikisha kila unapotaka kulala unahesabu hela ulopata na kutoa uliyotumia hili kujua upotevu wa pesa yako.
Kamwe huwezi kutunza pesa hadi siku utakapojua wapi inapotelea.
Asante sana mkuu!, record keeping inanisumbua sana. Nimejaribu hizi siku tano zilizopita naona nazidi kuchanganyikiwa (5days----145,800/= expenditure), ila nakushukuru kwa kunikumbusha. Nimejigundua pesa zipo ila zimekosa management
 
Acha kabisa tabia ya kutoa tip ukienda bar!
Umenifurahisha! lla sio kwamba tunapenda kutoa tip, ila ukishapiga vitu vyako unashangaa tu mwenyewe unatoa bila kuombwa!

Sijui kuna kaushirikina hapa!?
 
Kila tumizi lako liandike kwenye diary yako.
Hakikisha kila unapotaka kulala unahesabu hela ulopata na kutoa uliyotumia hili kujua upotevu wa pesa yako.
Kamwe huwezi kutunza pesa hadi siku utakapojua wapi inapotelea.
Aisee nami nitaanza kufanya hivyo
 
Imekaa vizuri.

Ingawa ukiangalia kiundani sana, hakuna kanuni maalum kufanikiwa kimaisha.

Wapo wenye vigezo hivyo vyote ulivyovitaja, na bado hakijaeleweka mpaka hii leo.

Na kwa kumalizia, kwa ambae unaemwamini Mungu.

Jitahidi kumtanguliza Mungu kwa kila jambo unalofanya


Asante kwa ujumbe uliokamilika.
 
...Na acha tabia ya kuwaamsha walio lala maana wote wakifanikiwa, Nani atamshikia mwenzake akili?

Nimecheka sana, ukimwasha aliyelala utalala wewe. Anatakiwa akigutuka upo maili milion mbele hata akikimbia hataweza kukushikia chini tena
 
Dah..somo mororo.. Hii ndiyo elimu bure...kwa kuongeza achana na kampani za matumizi... Jikite kwenye kampani za kipato
 
Back
Top Bottom