Kama unaingiza faida ya Tsh. 30,000 na kuendelea kwa siku pita hapa

Hongera kijana, ila naona kuna kijana mwingine hapa namsoma anasema kwamba kupata hio faida kwa siku lazima uanze na mtaji wa milioni 50, je ni kweli ? Nimeuliza makusudi nipate jibu kutoka kwako usaidie na wengine ili wengine wenye kutaka kuanza business kama yako wasikate tamaa na capital waliyonayo au wanaokatishwa tamaa na comments kama hizo Kashindi,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unanunua wap mkuu
Bei inategemea na quality ya beli nililofungua kwa mfano nguo za watoto kila moja inakuwa na bei yake. Ila viblause naweza kuanzia 10,000 kwa kimoja vikishachaguliwa sana nashusha nafanya 5000. Magauni naanzia 10,000 - 15,000 na unakuta beli la magauni linakuwa na kg 100 hivyo nguo no nyingi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
iko hivi ndugu yangu King999 hao wateja wakuvutiwa na ka ofisi kako kazuriiiiiii sio wengi kama wateja wale waaopenda

ingia sehemu local/kawaida,halafu wateja hao wanaovutiwa na ofisi yako nzuriii wakija ofisini wana mbwe mbwe nyingi

halafu akiingia ofisini kama yupo na demu wake wataishia kunywa SODA 1 na kutoka,(ofisi yako wataifanya kama kfc)

kijiwe cha stori ila hawatokuja ofisini kwako kwasababu kweli wanahitaji walichokifata (wewe mwenyewe unaweza kuwa mfano)

n mara ngapi week end ukitaka kutoka out kwenda sehemu nzuri huwa ukifika kule unaishia kunywa ka juice na maji 1 kubwaaa then unarudi nyumbani??

sehemu local/kawaida ni maalumu kwa wenye shida haswaaa yani ukienda sehemu hiyo unakua kweli "u need service" kama wewe leo umesema umeenda kibanda cha mpesa ukaondoka kwasababu hukudhani kama ana salio...

Unajua kwanin hukuenda pale kwenye kile kibanda??? "wewe sio mteja serious" hukuwa na shida na ile huduma ya pesa kwa haraka ndio mana wewe kwako unaangalia ofisi kuliko Lengo lako linalokupeleka pale.

Mtu kama mimi nikiwa nahitaji pesa huwa sijali ofisi ya mtu ikoje as long as kachora MPESA mimi naendaaaa,yule jamaaa wa kibanda cha mpesa ametulenga wateja sisi (mimi) na si wateja wewe maanaa wateja wewe huwa mnaenda ma ofisi ya watu badala ya kufata kilichowapeleka mnaanza angalia ofisi za watu wamekalia nini,wamevaa nni,nk

wateja sisi (mimi) ndio wengi katika ulimwengu huu kuliko wateja wewe boss King999 maana sisi vi hela vyetu ni kidogo ila tunavitoa kila siku,ila mteja wewe ulikua unataka ukatoe sh.laki 9 ila kuja toa hiyo amount n mpk mwezi ujao,wakati huo sisi wa vi elfu tano tano tunaena ile ofisi daily,kila saaaa ila mteja wewe unatokea mara 1 kwa wiki.

Umeona utofauti hapo sasa mkuuu.

Sina cha kuongeza. Umesema yote


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa nn unatoka tahadhari kuwa watu wasikope? Hata kwa mtumishi ambaye ana mshahara wake nae asikope? Ili ajitafutie kipato cha ziada?
Mawazo yote huko juuu ni mazuri na yana faida kama yalivyoandikwa

ONYO

Usilogwe na mtu au usipate mzuka ukapitiliza ukatamani kwenda KUKOPA

ili uje ufanye moja ya mawazo waliotaja wadau huko juuu (usijaribu) narudia tena (usijaribu)

Kama huna hela tafuta njia ya kupata pesa (hakikisha pesa ni yako) usiazime kwa mtu yeyote yule

Wala usichange na mtu yeyote yule Hata kama una rafiki yako (mmeivana kama nyanya) na mnasoma wote hii thread

Usijichanganye mkasema eti tuchange tufanye PROJECT hiii (we we we we we) msitake nimalizie.

Katika mawazo yote CHOMOKA na wazo lako 1 litafutie hela(mtaji) ukishika pesa yako mkononi ambayo

Hujamuomba mtu,hujamuazima mtu,hujamkopa mtu,nk Ingia Mzigoni weka vitendo sasa.

Fanya PEKE YAKO

usiogope kugombana na rafiki kisa mlikua mmeivana unashindwa kujua utajitengaje nae

Usijitenge nae kwa ubaya,kama unampenda sana Muite mwambie kuna A B C D.... then msikilize respond yake

mwambie nataka tufanye 1 2 3.... ila wewe ufanye kivyako na mimi kivyangu then tukutane jioni tupongezane au

kupeana pole Akikubali haya asipokubali (ndio pona yako)

Thanks.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
dada manengelo uko serious na ulichoandika au ni typing error?? yaan gunia lenye ujazo wa debe 10 unasema lina kilo 40 how comes??

sorry nikuulize ktu,,, huwa unaskiliza taarifa za biashara pale radio free wanapotangaza bei za gunia la mahnd,mchele,maharage n.k

huwa unamsikia yule mtangazaji huwa anasema gunia lina kilo ngapi vile?

Sent using Jamii Forums mobile app


😅😅😅!... Bahati nzuri nnaifanya hii biashara mkuu! Anywys tuyaache haya!
 
  • Thanks
Reactions: amu
Back
Top Bottom