Kama serikali tatu ni 'Hatari' na mbili ni 'sintofahamu' tuuvunje muungano

tpmazembe

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
2,469
581
Wana ccm wanasema serikali tatu jeshi litatawala nchi,Mara muungano utakufa. Ukawa wanasema serikali mbili ni sintofahamu,znz kutojitambua,kutokuwa na mamlaka kamili, huku watanganyika wakiona kama znz ni nchi nyingine ndani ya nchi moja.

Mimi nashauri ili kurahisisha mambo kwanza huu muungano ufe. Mpaka pale tutakapotaka kuungana tuanzishe mchakato wa kuungana kama livyo mchakato wa eac.

Hatuwezi kupitisha serikali mbili leo kesho tusikie vurugu znz, mara watanganyika machinga wanachomewa vibanda vyao huko visiwani angali ni nchi moja.malalamiko ya znz yamedumu karne na karne.

Pia hatuwezi kupitisha tatu bila kuangalia utayari wa washiriki kuchangia, isije kutokea mdau mmoja anaambiwa lete mchango wako aseme hana kitu huku watumishi miezi inasonga hawajalipwa nayo ni hatari kwa taifa.Alafu muungano wa serikali tatu kati ya tanganyika na zanzibar wa nini serikali zote angali znz na tanganyika wakiachana watakutana eac ambako nako tuna mchakato wa kuwa na dola moja.isiwe kulazimishana.muda uliopotea ni mkubwa kuliko mapato yapatikanayo kwa sababu ya muungano.

Ukipiga hesabu zaidi ya siku hamsini sasa wajumbe zaidi ya 600 wanakula laki 3 kwa siku kuhusu muungano alafu ukiiuliza tra imekusanya kiasi gani znz kuleta hazina unaweza kuta hata mil 100 haifiki.
 
Muungano ukifa kipindi hiki itakuwa ni nafasi ya kujiinua hata wale waliofichama! Lazima Tanganyika na Zanzibar ziwe na mamlaka kamili, hii ya muungano kama itateteleka hawa wataendelea!! Jeshi likichukua nchi bado ni letu watanzania, hakuna cha ajabu katika mabadiliko na kuirejesha nidhamu!!
 
samweli sitta alienda znz kupeleka muswada wa katiba ukachomwa moto mbele yake. akaokolewa na polisi mpaka uwanja wa ndege akapanda na kurudi dar. hao aliokuwa anaongea nao sio watoto wa mtaani bali ni watu wazito asilimia kubwa wakiwa ni wawakilishi wa baraza la mapinduzi. Lakini nashangaa sasa.ANATAKA TUENDELEE KUISHI HIVYO.yaani mtanganyika ukiwa kenya au msumbiji unajiona uko safe kuliko ukiwa znz na unakuwa ukicheka na kupiga stori na wakenya au wazambia kwenye nchi yao kwa raha kabisa kuliko ukiwa kwenye nchi yako tanzania sehemu inaitwa zanzibar.WE NEED TO CHANGE.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom