pwilo
JF-Expert Member
- May 27, 2015
- 10,098
- 12,474
Habari za wakati huu wakuu,
Jana ilikuwa siku muhimu sana katika Historia ya Soka la Tanzania na Africa kwa ujumla baada ya Ufunguzi wa African Football League katika Uwanja wa Benjamin william Mkapa mechi ambayo iliisha kwa sare ya goli mbili.
Wadhamini wakubwa wa mashindano haya ni Saudia na Rwanda, ambapo wakati mechi inaendelea maneno kama Visit Rwanda na Visit Saudia yalionekana, ambayo kiuhalisia hiyo nafasi ilitakiwa iwe yetu.
Inamaana kuanzia zanzibar na Tanzania bara hawakuona umuhimu wa kutafuta kitu cha kututangaza kama nchi mpaka Rwanda na Saudia wanachangamkia fursa sisi tupo tumelala usingizi wa pono! Hapo kama nchi tumefeli.
Kwa tukio la jana ambalo watu maarufu na viongozi mbalimbali wa mpira Duniani walikuwa uwanjani akiwemo Rais wa FIFA na aliyekuwa Kocha wa zamani wa Arsenal, Mzee Arsene Wenger ilikuwa fursa adhimu ya kuonyesha vipaji mbalimbali tulivyonavyo katika nchi yetu.
Hivyo nilitegemea wachezaji wa Timu ya Wanawake ya Simba na wachezaji vijana wa Simba kucheza mechi za ufunguzi kabla ya mechi rasmi, kwasababu jana kulikuwa na football agents kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Kweli mtu amuangalie Kibu Denis na Saido Ntibazonkiza hata kama ni wachezaji wazuri atawapeleka wapi kwa umri wao? Kosa kama hilo tulifanya walivyokuja Sevilla kutoka Spain, walisema wachezaji wa Simba ni wazuri ila umri ndio ilikuwa tatizo.
Wenzetu hutumia fursa kama hizi kama njia ya kuonyesha vipaji walivyonavyo na kuonyesha uwezo wa wachezaji wadogo kama njia na fursa ya kusakata kabumbu nje ya Bara la Afrika na Tanzania kiujumla, ila na hapo pia tumefeli kama nchi na kama club.
Simba kwa kushirikiana na serikali walitakiwa waingie makubaluano katika mashindano haya makubwa kwa ngazi ya vilabu Barani Africa, nilishangaa kuona M-Bet badala ya Visit Tanzanka kwenye kifua wakati mkataba wa M-Bet ulikuwa ni CAF Champions League kwa Level za Kimataifa na Mashindano yote ya ndani, nilishangaa kuona na hili pia linatupita kama nchi tumefeli kwenye hili tena.
Kuteleza si kuanguka, ila wakati mwingine tutumie haya mashindano kibiashara zaidi kuliko kuangulia tu matokea. Bado hatujachelewa, tujipange tena kwenye Maandalizi ya AFCON, tusichezee fursa wakati zipo mlangoni mpaka majirani wanazichangamkia.
Tatizo tunaangalia kila kitu kisiasa na kiushabiki, ndio maana kila siku tunakumbuka shuka kumekucha! Tuamke wazee, Dunia ya 1980 sio ya leo 2023, next time tujipange.
Alamsik.