Kama Mradi wa Mwendokasi akibinafsishiwa mwana JF basi azingatie sana haya

themagnificient

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
988
3,318
Najua Jf ina Madon wengi tu sishangai siku serikali ikampa mwekezaji Binafsi huu mradi alafu akawa ni mwanachama mwenzetu hapa maana mradi ndipo unapoelekea

sasa ukipewa huu mradi Ili usifilisike maana ni lazima utaleta vyuma vipya na utahitaji faida
Maana kutakuwa na mgao wa Serikali kama Dp vile sasa fuata yafuatayo

1.Ukipewa tu huu mradi hakikisha unafukuza wafanyakazi wote kuanzia Managent,Wahasibu,Mafundi yaani timua wote hadi wale wachukua tiketi safisha

Hawa watu waliukuta mradi una mifumo ya kisasa ya kulipia tiketi kwa kutumia kadi wakacheza nayo ikafa wakapata mwanya wa kukata matiketi ya mkono ili wapige pesa na ushahidi ni Waziri mkuu alivyofanya Ziara Bandarini alisema ana taarifa kuwa kuna wafanyakazi wanaingia na tiketi feki pale zikiwa zimwprintiwa kisha zinauzwa kama tiketi halisi hadi ikapelekea watu kutimuliwa pale

Wakaona waajiri wakata tiketi na wachana tiketi mwisho wa siku wanasema wanapata hasara kampuni haina faida

Fukuza mafundi wote pale wanajaza vyoo tu think unaambiwa kuna Gari 70 zimekufa tokea lini gari ikafa wakati spare parts zipo , Mafundi na timu ya wanunuzi wote timua lazma ijulikane pesa inaenda wapi kama pesa ipo kwanini gari 70 zife na Mafundi wapo na pesa wanapata nakwambia timua wote ajiri wapya na kuwa Gaidi

Safisha ile management yote timua usiache uchafu wowote pale

2 Fukuza Madereva wote yaani timua wote na kama ukibaki na madereva basi hakikisha uwe umepata taarifa zao kuwa walikuwa na utendaji mzuri, Moja ya watu wanaoua huu mradi ni madereva hawatunzi magari, Maajali ya mara kwa mara na ushahidi ni juzi mwendokasi mbili ziligongana think, na zifuatazo ni tabia zao:

Madereva wa mwendokasi wana majivuno na ni wajeuri kupindukia,

Dereva wa mwendokasi anaweza akakuta abiria wamejaa kituoni alafu anapitisha basi tupu pasipokupakia.

Dereva wa mwendokasi anaweza akashusha abiria gerezani au kivukoni alafu akapaki gari likiwaka akashuka na kwenda kusiko julikana na abiria wamesimama kituoni.

Mradi unatakiwa gari ziwe barabarani hadi usiku wa saa 6 ila wakishusha abiria kimara saa 2 usiku tu wanakimbilia kwenda kupaki magari kule yadi yao ya mto msimbazi wanaenda kulala waati bado abiria wamejaa vituoni.
 
Back
Top Bottom