Kama mpaka TBC 1 wameokoka basi CCM ni yatima sasa. Yametimia!

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,802
71,229
Katika pitapita yangu nikaangukia kwa bahati mbaya TBC1 kwenye Television. Eeh Mungu, maajabu niliyoona ni kwa TBC1 kuonyesha coverage ya ujio wa Tundu Lissu kwa bashasha na uhalisia na nikashtuka!

Je, niyaonayo yanatoka TBC kweli au hii TV yangu ni zile fake ambazo habari za BBC inasema ni VOA? Sasa kama hata TBC wanaripoti haya basi IMEKWISHA!

CCM tuliyo nayo imebaki yatima na inakufa kwa sonona. Upweke kitu kibaya sana. Ila ni ndugu zetu hao hata kama hawana aki.i tutawatunza na kuwaelimisha.
 
Tokea January 3 tangazo la Rais kuruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa, TBC nao wamefunguliwa minyororo.

Kweli unafiki unawaweka wengi mjini, sasa tunashuhudia ladha stahiki kutoka chombo hiki cha taifa. Kwa ubora wa teknolojia wanayotumia, wakiendelea hivi kuwa huru hata kwa 50%, itavutia watazamaji wengi.

Leo habari za CHADEMA unazipata kabias TBC, maneno ya Katiba mpya sasa yanasikika vizuri kupitia TBC. Hakika Mama Samia ameifungua nchi kila sehemu.

Ushauri kwa Warioba; aongeze majembe zaidi hapo TBC ili wanasiasa uchwara waumbuke kwa kupata mahojiano tahadidi.

Wasalamu,
TT.
 
Hao Ni Wapuuzi Sana Wana Vipindi Zaidi Ya Miaka 3 .

Kwenye Radio Na Television Wanarudi Hivyo Hivyo

Wakati Mwingine Unajiuliza Hakuna Wahariri, Wasimamizi Wa Vipindi

Utagundua Hawa Ni Wavivu Siyo Wabunifu Kwenye Radio/Television
 
Back
Top Bottom