Kama mke hazai ni vema kuachana naye?

Binafsi nina mifano mingi tu katika ili tatizo la kutopata watoto. Nima mfanyakazi mwenzangu alikaa ndani ya ndoa miaka 15 bila kupata mtoto mwaka wa 16 mkewe akapata mimba. Alianza kusikia kichefu chefu mara hiki sipendi mwisho wa siku wakaenda hosptali akakuta ana mimba ya miezi 5. Sasa hivi mtoto wao mkubwa anasoma shule. Mwingine naye alikaa ndani ya ndoa miaka 12 bila mimba na wala dalili za kupata mtoto. Baada ya hapo mkewe akapata mtoto. mtoto wao kwa kipindi ana miaka 5. Mwingine alikuwa rafiki yangu, alipata rafiki wa kiume wakati ana mtoto wa miaka 4, alipoanza rafiki mara uchumba familia ya mwanaume wakawa hawampendi binti kwakuwa alikuwa family friend. Walidumu katika uhusiano kwa muda wa miaka 6 hivi. Wakafunga ndoa. Mke akawa hapati mimba kipindi chote tangu rafiki hadi ndoa. Ndugu wakaanza kumsakama kuwa hazai. Binti alikuwa na kazi ya uhakika akaanza kuangaika hospital moja baada ya nyingine. Kila anakokwenda anaonekana hana tatizo lolote. Mme anagoma kwenda kwa kisingizio kuwa mbona ana mtoto? Mke alipoona manyanyaso yamezidi siku moja akagharamia safari ya kwenda Nairobi yeye na mme, bila mme kujua kuwa wanakwenda kufanya ninini. Mme alidhani wanakwenda kutombea tu? Walivyofika wakaenda kupima ikaonekana mme ndiyo tatizo la kutopata mtoto. Bwana likamshuka! Ikabidi mama apandikizwe mbegu za mmewe. Hivi ninavyowaambia wana watoto wawili wakwao na yule wa mme aliyepewa zawadi. Ushauri wangu kwako, nenda na mkeo mpime mtapata ufumbuzi wa tatizo na njia ya kukabiliana nalo.
 
Nimeoa mke miaka SABA lakini hazai ,nifanyeje wakati nimefunga naye ndoa?Mimi nina uhakika mzima.Naombeni msaada umri unanitupa mkono

usimuache ila katest kupiga goli la nje
unasema wewe mzima umepima kama kweli huna mapungufu?
 
mkuu usiache mke sababu ya kutopata mtoto.
mfano mmoja wapo ni mimi mwenyewe, wazazi wangu walikaa miaka13 ya ndoa bila mtoto, mwaka
wa 14 wa ndoa ndio nikazaliwa mimi JEJI, lakini hawakuwahi onyeshana tofauti yoyote.
 
Nimejaribu kusoma maoni ya wadau kwenye jf hasa kwa tatizo la Mutta,Hata mm ninatatizo kama hilo,kibaya zaidi mke wangu mimi ni mkorofi hataki kusikia ninalomuambia,nimejaribu kwenda nje mpaka sasa nimejikuta nikitoa mimba 4,nikijua kama labda nisubiri mwezi huu atashika mimba lakini wapi hadi leo.sasa nimefikia hatua nimeamua sitoi tena huko nje,bora niwe na mtoto na umri nao unakwenda.Aliyesababisha nikajua huko nje ni yeye,maana aliaza kejeli na kiburi cha kutaka kushindana na mwanaume.Mutta sikushauri uchukue maamuzi niliyoyafanya mimi.maana sijui tabia ya ubavu wako(Mkeo)kama ni mwanamke wa kujishusha na nyenyekevu mvumilie.lakini kama ndio anajidai mbabe tena kwako kaka angalia ustaharabu wa kuwa na chapa yako.Hutashindwa kupeleka matumizi
 
Unakumbuka kwenye ndoa ulikula kiapo cha kwamba utamvumilia kwenye raha na ...........halafu kujua jibu la swali lako em put yourself into her shoes tuassume kuwa we ndo ungekuwa huna uwezo wa kuzaa ila unampenda mkeo ungependa akuache kwa sababu hiyo au ungetakaje?
Nimeoa mke miaka SABA lakini hazai ,nifanyeje wakati nimefunga naye ndoa?Mimi nina uhakika mzima.Naombeni msaada umri unanitupa mkono
 
Nimejaribu kusoma maoni ya wadau kwenye jf hasa kwa tatizo la Mutta,Hata mm ninatatizo kama hilo,kibaya zaidi mke wangu mimi ni mkorofi hataki kusikia ninalomuambia,nimejaribu kwenda nje mpaka sasa nimejikuta nikitoa mimba 4,nikijua kama labda nisubiri mwezi huu atashika mimba lakini wapi hadi leo.sasa nimefikia hatua nimeamua sitoi tena huko nje,bora niwe na mtoto na umri nao unakwenda.Aliyesababisha nikajua huko nje ni yeye,maana aliaza kejeli na kiburi cha kutaka kushindana na mwanaume.Mutta sikushauri uchukue maamuzi niliyoyafanya mimi.maana sijui tabia ya ubavu wako(Mkeo)kama ni mwanamke wa kujishusha na nyenyekevu mvumilie.lakini kama ndio anajidai mbabe tena kwako kaka angalia ustaharabu wa kuwa na chapa yako.Hutashindwa kupeleka matumizi

mjomba hapo wee umelitoa jibu la hakika, sio kuacha kwanini uache, km anaheshima mvumilie kama ana kiburi mjuaji sana chapa nje sana, ila mind u ngoma nayo isikunyemelee
 
Nimeoa mke miaka SABA lakini hazai ,nifanyeje wakati nimefunga naye ndoa?Mimi nina uhakika mzima.Naombeni msaada umri unanitupa mkono
Miaka saba bado mapema mkuu. Ndoa inahitaji upendo, uvumilivu na kubebeana mizigo.kama wengi walivyoshauri ni vema wote mwende hospitali kupima mpate ushauri wa wataalamu. Pia na muhimu mwamini Mungu nenda kwenye maombi na mke wako muombewe inaweza kuwa tatizo ni jambo dogo sana. Inawezekana hata ni maneno tu ya laana yalinenwa sasa inawafuatilia au maagano yalifanywa juu ya familia yenu au ya mke wako juu ya kutopata watoto n.k. Hakuna jambo linaloweza kumshinda Mungu. Mpende sana mkeo wala usimwache kwani yeye hajaamua kutopata mtoto na laiti ungalijua yeye ndiye anayetamani kupata mtoto kuliko wewe. Usiingie kwenye hilo kosa kwani litakugharimu hata kwa mke mwingine utakayeamua kumwoa.
 
umejuaje kama we mzma? kama nyie ni wakristo ile kitu mlivyoapa pale si mpaka kifo kiwatenganishe? hii sasa ndo inaitwa "for better or for worse until death do us apart".
 
mkuu usiache mke sababu ya kutopata mtoto.
mfano mmoja wapo ni mimi mwenyewe, wazazi wangu walikaa miaka13 ya ndoa bila mtoto, mwaka
wa 14 wa ndoa ndio nikazaliwa mimi JEJI, lakini hawakuwahi onyeshana tofauti yoyote.

hawakuwahi kutofautiana? ulikuwepo?
 
Kwanza ni vizur kwenda hospital kujua nan mwenye tatizo na ni tatizo gan. Pili mkigundua tatizo mkae chin wote wawili mshauriane njia sahihi ya kulitatua. Kama mmoja wenu ndo anatatizo na mnataka motto nn kifanyike? Mawazo yenu wote yatasaidia kuendelea kudumu katika ndoa. Tatu, kama wewe ndie mwenye tatizo uko tayari mkeo akuache kama wewe unnavyotaka kumwacha? Kiapo chako cha ndoa kinamaana gan hapo?
 
Hahaha, mke nae atachacharika kimya kimya. Pamoja na kuoa wake wengi bado hawaachi kutongoza kila uchao.
Hii safi sana. I hope ikigundulika kuwa Mutta (mwanaume) ndiye mwenye tatizo hawezi kusababisha mimba basi na mkewe naye atakuwa na haki ya kutafuta mtoto kwa namna nyingine kutoka kwa mwanaume mwingine. Kweli ni dini mzuri sana.
 
Mkuu nendeni mkapime tu! Siku hizi vipimo vipo kibao, kuna wanaume wana low sperm count yaani anazaa kwa kubahatisha! So usione umezaa ukajidai kidume, sana sana utamfanya mkeo atoke nje kujicheki kama yuko slama au vp! Kapime
 
huu uzi wa zamani kidogo
Mutta twaomba mrejesho tafadhali
 
Last edited by a moderator:
Nimeoa mke miaka SABA lakini hazai ,nifanyeje wakati nimefunga naye ndoa?Mimi nina uhakika mzima.Naombeni msaada umri unanitupa mkono

Umehakikishaje kuwa wewe ni mzima? The best way ni kufanya vipimo vya kitabibu kwanza then mtajua nani an shida. Pole kwa tatizo hilo
 
ndugu yangu mipango ya kuwa mtoto ni Mungu ndiye anayepanga umejuaje kuwa na wewe ni mzima kwanini umwambie mkeo yeye ndo ana tatizo bila ya wote kwenda kupima ni heri wote mkaenda kupima ikagundulika tatizo liko wapi kisha mkaanza kusali na kumwomba Mungu ndiye atupate zawadi ya watoto, hivyo nakushauri usimwache mkeo kwani hiyo miaka 7 ni midogo sana kwake kwani kwake Mungu Siku moja ni sawa na siku 1000, wako wenigne ndani ya ndoa wanakaa miaka 15 - 20 na hawana watoto lakini wanafurahia ndoa zao iweje wewe unaona mzzigo wa mkeo? Je ULIMPENDA MKEO? unakumbuka kiapo ulichosema pale hadharani kwa padre, mchungaji, ? chukua hatua madhubuti ya kufanya usimwache mkeo
 
Kwanza napenda nikupe pole

Ndoa si watoto,wala mali,kazi,pesa,ndugu,marafiki,elimu,dhahabu,magari,nyumba na vingine vingi unavyojua wewe hivyo vyote si ndoa.Ndoa ni makubaliano ya watu wawili mke na mume kukubaliana kuishi pamoja kwa upendo na kuvumiliana katika nyakati zote umaskini au utajiri,raha au tabu,magojwa au afya na mengineyo.

Ulikubali kumuoa mkeo kwa sababu ulimpenda na ukamchagua wewe uishi naye katika maisha yako yote,matokeo ya ndoa ni pamoja na watoto,mali,kazi na vingine vyote vitakavyokuja baada ya kuanza kuishi pamoja.

Tatizo la mke kuzaa si lako wala la mkeo maana ulimuoa kwa sababu ulimpenda na si sababu anazaa au azai,muhimu hapa ni kushirikisha watu wazima wenye hakima na si marafiki wala ndugu maana wengi ni wanafiki na pia jaribu kuonana na watu wa afya pia.

Mie nimekaa na mke wangu baada ya miaka 3 ndiyo akapata ujauzito najua inaumiza lakini hapo ndipo kipimo chako cha imani na uvumilivu wenu ulipo.Mwamini mungu funga na kuomba atakusaidia.mafanikio mengine yako katika maisha yako kwa mkeo wa ndoa.

Rafiki yangu mmoja mwezi January katikati mke wake kazaa mapacha baada ya kuishi naye kwa miaka 12 kwenye ndoa,unafikiri asingefanya uvumilivu nadhani angeweza kuona hao mapacha?aliweza kufanikiwa kiuchumi lakini Mtoto ilikuwa shida.uvumilivu ndiyo unaotakiwa katika maisha yetu.

Napenda kukutia moyo usikate tamaa na endelea kuwa mvumilivu haja ya moyo wako Mungu atakujibu,usiogope swala la umri,umri na number tu hakuna aliyeweka contract na Mungu wa hiyo hilo lisikutishe.


WEEKEND NJEMA
Ni sahihi kabisa ,lakini hii hali ni ngumu ndugu ,rafiki wala wazee wenye BUSARA,hawezi kupata ufumbuzi! Wahusika ndio wanaweza kulitatua ,hapo ndipo unapokuja umuhimu wa kuoana mkiwa mnapendana!
Kama walioana for sake ya kuoana tu huu ni mtihani mkubwa !
Mhusika kaa chini na mkeo mlijadili kwa kina!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom