Kama makanisa yataendekeza kwaya kuimba style za Mayele kanisani mimi nitaacha kusali

Mimi huwa nakereka sana katikati ya ibada inasimama kwaya kuimba mwishoni wanaanza kucheza style ya Mayele kwa kupiga mikono na kutetema, hicho kitendo ni cha kipuuzi sana!

Kwanza mnajua huwa anamaanisha nini? Au kila mtu aje na style ya mchezaji anayempenda tucheze kanisani?

Tuheshimu ibada, mwambieni Mayele awakataze mashabiki zake kabla hakijamkuta cha kumkuta!
Kanisani huwa hakuna ibada Bali shughuli/event...ibada gani kula humohumo,kuomba na kucheza,Nina uzoefu na Roma,nimeingia Sana ibadani
 
Simple: ukiona kanisa la aina hiyo basi hao ni wajasiriamali na siyo kanisa. Siku hizi inabidi kuwa makini ili uweze kutofautisha kati ya kanisa na utapeli. Kwa taarifa yako matapeli wengi wamehamia nyumba za ibada kwani wanajua huko ndiko rahisi kutapeli.
Ibada ya Roma ukiacha kula mikate ni theater na mhadhiri
 
Waoneshe pia style ya kushangilia ya yule striker wa Mbeya City
 
Asee kweli mkuu.
Leo wanakwaya wamebadili na wamekuja na staili ya Tariq seif kiakala asee kabisa zima tumefurahi sana😄😄😄
 
Ikiwa ni kweli hili ulisemalo, basi huko kanisani kuna vituko.
Kwahiyo hapo ndio munaabudu, sio?
 
Tumemshauri atumie style ya Tariq seff wa mbeya city Ili huko kanisani wasiteteme
 
Hakika
Duuuuuuu!!¡! Dini ya kikristu bwana inashangaza sana,akija mchezaji mwingne na style nyingne wataimba kwa style hiyo.Ndugu yangu zinduka hiyo sio dini ,hicho ni kikundi cha wauuni wanakutana na kuwashawishi watu wapeleke sadaka ili wakazipige.
 
Mpaka style za Pepe Kale zipo, utafurahi. Wanafanya mazoezi kwani huko Mbinguni ni kuimba tu na kucheza.
 
Mimi huwa nakereka sana katikati ya ibada inasimama kwaya kuimba mwishoni wanaanza kucheza style ya Mayele kwa kupiga mikono na kutetema, hicho kitendo ni cha kipuuzi sana!

Kwanza mnajua huwa anamaanisha nini? Au kila mtu aje na style ya mchezaji anayempenda tucheze kanisani?

Tuheshimu ibada, mwambieni Mayele awakataze mashabiki zake kabla hakijamkuta cha kumkuta!
🤪🤪🤪nimecheka
 
Back
Top Bottom