Shy land
JF-Expert Member
- Jul 28, 2013
- 6,024
- 1,960
Mimi ni mchawi naheshimu sana, imani na dini za watu japo kuwa sisi wanatudharau kwa kuwa eti tuna imani za kichawi.
Kama nilivyozoea kusema serikali ya Tanzania haiko katika utawala unashikamana na dini yoyote, kwa sababu itikadi za kidini zinaweza kuleta machafuko makubwa katika taifa letu.
Mwl. J.K. Nyerere popote pale ulipo tunakupongeza Watanzania kwa kufanikiwa kiasi kikubwa kutunyofolea dhana za kidini, ukanda pamoja na ukabila katika taifa letu, ndio maana hadi leo Watanzania tunaishi kwa amani bila shaka yoyote japo kuwa ni masikini.
Umasikini wetu ni bora zaidi kwa kuwa tuna amani katika taifa letu, wahenga walisema NI BORA KULA UGALI NA CHUMVI KWENYE AMANI, KULIKO KULA WALI NA NYAMA YA KUKU KWENYE VITA.
Hoja yangu ni kuhusu kwa wenzetu wanaodai mahakama ya Kadhi yatambuliwe na serikali na yaendeshwe kwa hela za umma hata kama sisi wachawi hatuhusiki kwenye mahakama hizo.
Kama serikali itakubaliana na madai hayo, na sisi wachawi tuko tayari kuishawishi serikali ya Tanzania kufugua mahakama zetu.