Kama kuna Taasisi inaongozwa na 'mungu mtu' kama asemavyo Lissu basi ni CUF na CHADEMA

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
85,724
145,604
Namshauri tu Makamu mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu aanze kuhamasisha mabadiliko ya Katiba kwenye UKAWA yaani CUF na CHADEMA.

Prof Lipumba, Mzee Cheyo na Mhe. Mbowe ni miungu Watu hawa kwenye vyama vyao.

Sifa ya Taasisi zinazoongozwa na miungu Watu utaziona nyakati za Chaguzi Zao za ndani, mungu Mtu huwa haguswi.

Pentekoste Njema 😀😀🌟
 
Namshauri tu Makamu mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu aanze kuhamasisha mabadiliko ya Katiba kwenye UKAWA yaani CUF na CHADEMA.

Prof Lipumba, Mzee Cheyo na Mhe. Mbowe ni miungu Watu hawa kwenye vyama vyao.

Sifa ya Taasisi zinazoongozwa na miungu Watu utaziona nyakati za Chaguzi Zao za ndani, mungu Mtu huwa haguswi.

Pentekoste Njema 😀😀🌟
Yaan leo umekuja na thread moja nzuri sana na potential sana. CDM na vyama vingine vinahamasisha sana katiba mpya. Lakin katiba zao ni za hovyo kabisa. Na wenyeviti wa hivyo vyama vya siasa, wanatumia hizo katiba za vyama vyao ambazo naweza kusema ni mbovu kuwa wenyeviti wa kudumu.

Vyama vya siasa vya Tanzania, vinahitaji sana kujitafakari katika muundo mzima wa, katiba zao. Ni ngumu sana na haitawezekana vyama hivi kudai katiba mpya ya JMT wakati vimeshindwa kabisa kutengeneza katiba nzuri na bora kwa ajili ya vyama vyao.

Si rahisi kabisa kutangaza kuwa watu wote wawe wanaoga na kufua nguo zao kila siku wakati ww hauogi na wala haufui nguo zako. Kwa mfano huo ni ngumu sana kwa CDM na vyama vingine kuja Kushida uchaguz wa Rais ,hapa Tanzania labda malengo makuu ya vyama hivi yawe ni Kushida ubunge na udiwani tu.

Kwa sisi ambao sio wanachama wa vyama hivyo au CCM , Ila tu ni wazalendo wa nchi hii. Tunapendekeza CDM na vyama vingine virekebishe kabisa zao ili viweze kuonyesha mfano mzuri wa democracy na hali hiyo itasababisha CCM na serikalini yake ya JMT , kukubali kubadilisha katiba ya JMT.

Kama CDM watakomaa tu na katiba waliyonayo ya kuwa na mwenyekiti wa kudumu, watanzania wenye akili hawatawaelewa kabisa na pia watabaki kuwa vyama vya ruzuku ambayo pia inafaida kwa watu wachache. Na pia kuwa vyama vya wabunge na madiwani sio vyama vya kuiongoa nchi ya Tanzania.

Na hii itadhibitisha maneno ya JK Nyerere kuwa 'I can't leave my country to the dogs'
 
Mhe. John.

Vipi fomu ya mgombea urais wa chama tawala kuchapishwa moja, huo siyo uungu mtu? Kwani Katiba ya chama tawala huwa inasemaje? Je, inafuatwa?
 
Back
Top Bottom