sammosses
JF-Expert Member
- Jan 24, 2011
- 1,682
- 1,110
Madaraka ni dhamana tu wanayo tunukiwa viongozi ilikuwaongoza/kuwaonyesha njia kwa wale wanao waongoza.Bunge ni chombo cha uwakilishi cha wananchi kwa kuwatumia wabunge kuelezeayale yote wananchi wanayoyataka.Rais ni mtumishi wa wananchi ikiwa ni pamoja na wale wote aliowateuwa kumsaidia kazi.Serikali ni watu,na watu ndiyo wenye maamuzi juu ya mustakabali wa nchi yao iendeshwe vipi.Sasa basi mawaziri waliokuwa wanadhani rais ambaye ni mtumishi mtukuka wa nchi hii atawabeba,amepima ameona hambebeki,ndo maana ametoa kauli kali kwa watendaji mnao jifanya kupe kunyonya rasilimali ya taifa.Kwa kitendo hiki mnataka nini zaidi ya kuita press conference na kutangaza yale yaliyokuwa yanategemewa kwa muda na waajiri wenu(wananchi) kwa kujiuzuru na kupisha ofisini ili tuweze kujiridhisha huenda ikawa mmekula zaidi ya kilichoanikwa!Msisubiri nguvu ya umma tuingie barabarani hatutakuwa na salia Mtume.