Kama kazini kwako hawajali kuhusu wewe unapata wapi nguvu ya kujali kazi zao?

BabaMorgan

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
4,059
10,514
Unapata kile unachotoa haiwezekani usambaze chuki utegemee return ya upendo.

Kuna baadhi ya mabosi wanatreat wafanyakazi wao kama takataka kazi kubwa isiyolingana na mshahara, mazingira hatarishi bosi anachofocus nacho ni kazi yake nothing else.

Unakutana na mfanyakazi anajituma kwa kufanya kazi kwa bidii akiwa na imani bosi anamuona na atamfikiria kwenye kuboresha maslahi yake huo ni uboya wa daraja la kwanza ukweli ni kuwa watakupongeza kwa mdomo na kuwa mfano kwa wafanyakazi wenzako kila mnapokutana kwenye vikao huku wale ambao wanaonekana wavivu na walalamishi wakipata mashavu wewe ukiendelea kusema dunia haiko fair.

Dawa ya bosi ambaye hayapi kipaumbele maslahi yako ni moja tu ni kumsababishia loss ile hela ambayo anaona shida kukupa wewe basi na yeye asiifaidi kiufupi haikose anamwaga mboga basi na wewe mwaga dona kwani hamjifunzi kwa waalimu wa serikali maslahi madogo wameamua kuzalisha zero kwa wingi ili tuwe taifa la mbumbu ambao hawawezi kuajiriwa ama kujiajiri namba ya vijana tegemezi inaongezeka ambayo inaenda kuwa loss kwa Taifa.

Naumia sana sana kuona vijana wenzangu wanapata ulemavu wa kudumu au vifo kutokana na kazi wanazofanya kwenye magodauni ama viwanda yaani una risk maisha kwa maslahi kiduchu.

Usimpake rangi punda ili awe pundamilia.
 
Kuna mdau alikuwa anasema kuna viwanda vya wachina wilaya ya mkuranga kwa Siku wanakupa elfu 6 na kazi unafanya masaa 12 . Na kazi zenyewe usipojikata kidole mshukuru mungu sana Mana ni hatari
 
Kuna mdau alikuwa anasema kuna viwanda vya wachina wilaya ya mkuranga kwa Siku wanakupa elfu 6 na kazi unafanya masaa 12 . Na kazi zenyewe usipojikata kidole mshukuru mungu sana Mana ni hatari
Mimi ofisi yangu inalipa 4500 kwa siku, changamoto ya kujikata ni ZERO.

Niletee vijana wawili waaminifu niwape kazi.
 
Back
Top Bottom