Kama kawaida yetu tutalalamika tu kwa wiki mbili hizi mfululizo, ila tutazoea kwa miaka mingi ijayo

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
57,114
110,498
Ifike tu wakati sasa tukubalini kuwa 'tumesharogwa' na Moshi (Mvuke) wa Mwenge ndiyo maana tunapelekwa na kufanyiwa watakavyo na tunaenda nao hivyo hivyo tu.

Si muda mwingi tulikuwa tunamjadili sijui Sadala baadae akaja Mzee Mpili kabla ya akina Msukuma na Muhongo kutuchanganya zaidi na Zawadi Mauya akapigilia Msumari wa Kutusahaulisha Kujadili Mambo makubwa na ya Msingi Kwetu.

Tutulieni tu hivi hivi 'tukomeshwe' vizuri mpaka Akili zetu zitukae sawa huku kila Siku tu watu wa SSIT wakiendelea kuwa Wabunifu kwa kujua vyema Akili za Watanzania na kutuhamisha au kutupeleka watakako na tunatii kama wale Mbuzi wa Yule Mpemba anayeogopwa kwa Uchawi (Ndumba) pale Mbezi Beach Makonde.

Kwa hili wala siwaonei Huruma. Mkome!
 
Ifike tu wakati sasa tukubalini kuwa 'tumesharogwa' na Moshi ( Mvuke ) wa Mwenge ndiyo maana tunapelekwa na kufanyiwa watakavyo na tunaenda nao hivyo hivyo tu.

Si muda mwingi tulikuwa tunamjadili sijui Sadala baadae akaja Mzee Mpili kabla ya akina Msukuma na Muhongo kutuchanganya zaidi na Zawadi Mauya akapigilia Msumari wa Kutusahaulisha Kujadili Mambo makubwa na ya Msingi Kwetu.

Tutulieni tu hivi hivi 'tukomeshwe' vizuri mpaka Akili zetu zitukae sawa huku kila Siku tu Watu wa SSIT wakiendelea kuwa Wabunifu kwa kujua vyema Akili za Watanzania na kutuhamisha au kutupeleka watakako na tunatii kama wale Mbuzi wa Yule Mpemba anayeogopwa kwa Uchawi ( Ndumba ) pale Mbezi Beach Makonde.

Kwa hili wala siwaonei Huruma. Mkome!
Wiki mbili nyingi sana. Hii ni nchi ya 7 days
 
Sisi tupo uchumi wa kati tulikua tunaishi maisha yasiyoakisi uhalisi awetu wa uchumi na hapo bado namuomba macho malegevu aongeze kutupelekea moto zaidi mpaka tufikie viwamgo ambavyo ni saozi yetu sisi nchi ya kipato cha chini
 
Lipa kodi wewe Acha kulalamika kama unakazwa,ni hivi unalalamika wewe na watu wako.

Wimbo wa mafuta umeisha sasa ni miamala,mlie au msilie kodi lazima zilipwe Kazi iendelee.

Unataka sgr ila kodi hutaki kulipa? 😂😂 Mwendazake alikuwa anapora wawekezaji saizi wote mnalipa kodi
 
Back
Top Bottom