Kama jina lako ni Mary, marufuku kuwa kahaba...!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398
IndiaTv4166d3_sex-worker.jpg

Huko Italy katika mji wa Siena ambao ni maarufu kwa mambo mengi, kuna sheria ya ajabu kidogo. ni ya ajabu kwa sababu, ingawa imejifunga na imani, lakini imesahau kwamba, jina ni jina tu. Kwenye mji huo mwanamke yeyote ambaye anaitwa Mary haruhusuwi kufanya biashara ya ukahaba.

Kama ataamua kufanya biashara hiyo, inabidi abadilishe jina kwanza. Akishindwa kubadili jina halafu akaenda mitaa ya mji huo inayotumiwa na makahaba na kujiuza kama ilivyo mitaa Kimboka Buguruni au Ambiance maeneo ya Sinza kwa hapa kwetu, na kujitambulisha kwa jina hilo la Mary, ni lazima atapelekwa lupango Segerea ya huko..............
 
Nasikia hata bongo ikonjiani kuja sheria hiyo. Ila wana tafuta nijina gani liwekewe sheria marufuku kuwa kahaba.
 
Fumbo la imani
Bahati mbaya kwaresma imeanza leo ningeenda mtafuta Maria pale shivas
 
When in Rome, do like Romans...

Washukuru huko wanaruhusu biashara ya makahaba, hapa Bongo, na nchi karibia zote (apart from Holland na nyingine chache) Ukahama hauruhusiwi hata ukiitwa Kicheche
 
hongera kwa status yako. nimebarikiwa sana kwa hilo.

huu uzi umenifurahisha sana manake kuna majina yana portray status fulan huwez ukaitwa jina la mama Yesu halafu ukaenda kuuza mwili ama ukaitwa jina Yasinta ukauza mwili ama fatima. utakuwa hata wale watakatifu wa Mungu unawakosea heshima kiukweli.

ama leo hii umkute kijana anaitwa Joseph halafu ametelekeza familiia huyu lazima apimwe akili. lakini ukikutana na mtu anaitwa Baraba ama Dismus halafu ni mwizi hutoshangaa
 
Mtambuzi kuna siku utakuja na story inayohusu jina la mwaJ maana naona zile za sura zimeisha.
 
Last edited by a moderator:
hongera kwa status yako. nimebarikiwa sana kwa hilo.

huu uzi umenifurahisha sana manake kuna majina yana portray status fulan huwez ukaitwa jina la mama Yesu halafu ukaenda kuuza mwili ama ukaitwa jina Yasinta ukauza mwili ama fatima. utakuwa hata wale watakatifu wa Mungu unawakosea heshima kiukweli.

ama leo hii umkute kijana anaitwa Joseph halafu ametelekeza familiia huyu lazima apimwe akili. lakini ukikutana na mtu anaitwa Baraba ama Dismus halafu ni mwizi hutoshangaa

Ha ha ha haaaa!!! Umenifurahisha kweli...Mbona umemsahau Yuda?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom