Elections 2010 Kama hali ndio hii, basi Dr. Slaa asubiri kuapishwa tu

Mtoka Mbali

JF-Expert Member
Aug 11, 2010
237
25
Mwaka 2005 mzee wangu alikuwa haabiwi lolote juu ya Kikwete. Alidiriki hata kumpigia kampeni nyumbani kwetu na hata kwa majirani. Hakutaka kumsikia mtu yeyote akiongea jambo lolote baya juu ya JK. Kwa kifupi mapenzi yake kwa CCM na JK yalikuwa motomoto.

Tukiwa tunaelekea kwenye uchaguzi wa mwaka huu nikaona si vibaya nikafunga safari kwenda kumtembelea mzee na kumsikiliza msimamo wake juu ya Kikwete na chama chake.
Kama kawaida nilijua mzee bado hapendi kusikia ubaya wowote wa CCM na hivyo ili nisimuudhi nikaona ni bora nianzishe mada kwa kumsifu Kikwete na chama chake kuwa wametekeleza ahadi nyingi walizoahidi kipindi kile. Nilianza kwa kusema 'Mzee, hivi hapa kampeni zinaendeleaje maana kule mjini ni kivumbi na jasho ila tunamwamini rais wetu Kikwete atashinda maana kutekeleza ahadi karibu zote alizotoa kipindi kile'.
Sikuamini nilichosikia kuto kwa mzee wangu. Akasema kama umekuja kwa ajili ya kumpigia kampeni Kikwete, hapa umepotea njia na inawezekana labda ulikokuwa ukienda bado haujafika hivyo tuulize ni wapi ili tukuelekeze.
Nilichanganyikiwa ikabidi niwaulize taratibu waliokuwa karibu kilichomsibu mzee na nilichoambiwa ni kwamba mzee hivi sasa hataki kusikia kitu chochote kinachohusiana na Kikwete na chama chake. Na kweli mzee wangu kaweza kubadilisha watu wengi tu ikiwemo na majirani zake.
Nilifurahi sana kusikia hivyo na nikamwambia kuwa nilikuwa namsanifu tu, ndipo tulipoanza kuongea lugha moja, yaani mwaka 2010 HATUDANGANYIKI

Ndio maana ninasema kama mambo yenyewe ndo hivi basi Dr. Slaa asubiri kuapishwa tu maana kama ushindi tayari amekwisha upata.
 
Well...

Kama ni mabadiliko ya kififra naamini mwaka huu kuna mapinduzi makubwa! Ikiwemo maoneo ya vijijini.

Ngoja tuone... Slaa aongeze nguvu tu.
 
Sema huko kijiji kwenu ni wapi isije ikawa hapo kivule. Ila siyo siri watz sasa wameshtuka sana tuache na ushabiki, na chama kilichofanya kazi kubwa kinafahamika ni chadema. Chadema imefanya kazi kubwa kuwaelimisha watz juu ya nchi yao. Nazidi kuwaombea waendelee kutupa mwanga. Pamoja tutafika kwa amani na utulivu.
 
Mwenyewe sikuamini nilipopiga simu kijijini kuulizia vipi ziara za mheshimiwa jibu nililopewa na mama mhhhhh nilishtuka.Aliniambia hivi,hakuwahi kusikia wala hakuna aliyekuwa akiongelea kuhusu Chadema,muda wote amekuwa kisikia kelele za ccm ila alishangazwa na umati uliojitokeza alipofika Dr.Slaa kijijini kwao.Kila mwanakijiji anasema huyu ndie.Nikamwuliza ccm je akanijibu imetosha.
 
Mwaka 2005 mzee wangu alikuwa haabiwi lolote juu ya Kikwete. Alidiriki hata kumpigia kampeni nyumbani kwetu na hata kwa majirani. Hakutaka kumsikia mtu yeyote akiongea jambo lolote baya juu ya JK. Kwa kifupi mapenzi yake kwa CCM na JK yalikuwa motomoto.

Tukiwa tunaelekea kwenye uchaguzi wa mwaka huu nikaona si vibaya nikafunga safari kwenda kumtembelea mzee na kumsikiliza msimamo wake juu ya Kikwete na chama chake.
Kama kawaida nilijua mzee bado hapendi kusikia ubaya wowote wa CCM na hivyo ili nisimuudhi nikaona ni bora nianzishe mada kwa kumsifu Kikwete na chama chake kuwa wametekeleza ahadi nyingi walizoahidi kipindi kile. Nilianza kwa kusema 'Mzee, hivi hapa kampeni zinaendeleaje maana kule mjini ni kivumbi na jasho ila tunamwamini rais wetu Kikwete atashinda maana kutekeleza ahadi karibu zote alizotoa kipindi kile'.
Sikuamini nilichosikia kuto kwa mzee wangu. Akasema kama umekuja kwa ajili ya kumpigia kampeni Kikwete, hapa umepotea njia na inawezekana labda ulikokuwa ukienda bado haujafika hivyo tuulize ni wapi ili tukuelekeze.
Nilichanganyikiwa ikabidi niwaulize taratibu waliokuwa karibu kilichomsibu mzee na nilichoambiwa ni kwamba mzee hivi sasa hataki kusikia kitu chochote kinachohusiana na Kikwete na chama chake. Na kweli mzee wangu kaweza kubadilisha watu wengi tu ikiwemo na majirani zake.
Nilifurahi sana kusikia hivyo na nikamwambia kuwa nilikuwa namsanifu tu, ndipo tulipoanza kuongea lugha moja, yaani mwaka 2010 HATUDANGANYIKI

Ndio maana ninasema kama mambo yenyewe ndo hivi basi Dr. Slaa asubiri kuapishwa tu maana kama ushindi tayari amekwisha upata.

Hayo ni kweli kabisa juzi nilikuwa vijijini Dodoma mbali sana na miji yote midogo unayoifahamu, kuna vijiji vingi sana huko lakini hakuna huduma za jamii kabisa, Na ni vijiji vina watu wengi tu wanatafuta madini huko. Nilichoshangaa kule hakuna TV wala radio inayokamata lakini wazee na vijana wa kule nilijaribu kuwauliza kama wanamchagua nani!!! , Amini usiamini wote wanamjua Dr. Slaa wala sijui wamemsikia wapi na hawataki kuambiwa chochote juu ya CCM!! Wanasema wamechoka
kuchezewa kama kichwa cha wendawazimu.
 
Hivi huamini zile takwimu za TISS kwa JK na waraka ule wa Slaa? Andaa Jambia..... Ee Mungu tuepushe na hili na waambie CCM wajiandae kuondolewa kwa kura wala sio jambia,,,,,,
 
Hiyo nimeiona mbeya mwenyekiti wa ccm kata ya salaga-uyole katoka na kundi kuubwa kwenda chadema, yaani watu wamechoka kweli! Nimeshangaa sababu huko ndiko ilikokuwa ccm damu cjui nini kimetokea!!
 
Kwa kweli muamko wa Watanzania ni mkubwa ila tatizo wengi hawajajiandikisha kupiga kura na wengine wanashangilia tu ukiwauliza shahada za kupigia kura hawana tayari waliziweka rehani CCM toka wakati wa kura za maoni hivyo changamoto za kuelekea kwenye mabadiliko ya kiuongozi bado ni kubwa ila Slaa anaweza
 
hebu tusambaze ujumbe huu ili watu wasiendelee kudanganyika tena.......mimi ni mfanyakazi na kikwete hataki kura yangu mimi ni baba ba mama yangu kule kijijini, nina kaka na dada zangu pia, lakini nina marafiki wengi wa kike na kiume, nina ndugu wengi wanaonitegemea babu na bibi zangu wapo hai kule kijijini kwa kweli nimetekeleza wajibu wangu kwa kuwaeleza jinsi ccm ilivyotufikisha mpaka hapa tulipo na mbinu zao wazitumiazo na nimewaambia kuwa pilau wale na pombe wanywe ila wamekubali na wameaapa kuwa kamwe hawatompigia kura kikwete na ccm yake........

NINGEKUWA MTU WA AJABU KM NISINGETEKELEZA WAJIBU HUU NILIOUTEKELEZA, WAFANYAKAZI WENZANGU MMEFANYA HAYA?
 
wadau, tuzidi kuwaelimisha wazee wetu huko vijijini, kwani huko ndo kuna kura nyingi za dr slaa
 
Sema huko kijiji kwenu ni wapi isije ikawa hapo kivule. Ila siyo siri watz sasa wameshtuka sana tuache na ushabiki, na chama kilichofanya kazi kubwa kinafahamika ni chadema. Chadema imefanya kazi kubwa kuwaelimisha watz juu ya nchi yao. Nazidi kuwaombea waendelee kutupa mwanga. Pamoja tutafika kwa amani na utulivu.

Ni mkoa wa Kagera, wilaya ya Bukoba Vijijini na kijiji kinaitwa Lubale karibu na kijiji maarufu kiitwacho Izimbya. Umenipata???
 
ccmbabati.jpg
 
Well...

Kama ni mabadiliko ya kififra naamini mwaka huu kuna mapinduzi makubwa! Ikiwemo maoneo ya vijijini.

Ngoja tuone... Slaa aongeze nguvu tu.
Vijini ndio kwenye mapinduzi makubwa matitizo yako mnjini hasa D.S.M na zaidi kwa wasomi walio wengi
 
Back
Top Bottom