Kama bado tutakuwa na watendaji wabovu, bado nchi yetu haitokuwa na nishati ya uhakika

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,136
7,711
Pamoja na jitihada kubwa zinazo fanywa na Serikali ya awamu ya 6 chini ya Mama, kuhakikisha kuwa nchi yetu inapata nishati ya uhakika lakini bado naona kuna tatizo la msingi ambalo pamoja na mambo yote lazima litizamwe upya, nalo ni watendaji/wafanyakazi wa TANESCO.

Ni muda mrefu tumekuwa tukisikia kuwa kuna watendaji ambao sio waadilifu wanahujumu shirika, sio wazalendo, watendaji wa aina hiyo hawafai wanapaswa wasafishwe.

Tanesco ni shirika nyeti hivyo ltunapaswa tuwe na watendaji waadilifu na wazalendo kwa Nchi.

Tusisahau kuna vita ya kiuchumi, lazima vita hiyo itapiganwa, haikwepeki. Tunafahamu kuwa baadhi ya mataifa hawafurahii kuona mradi wa Bawa la Nyerere unafanikiwa.

Lazima tuwe na watendaji wazalendo katika vita hii ambao hawatoisaliti nchi kwa masilahi binafsi.

Tujipange kabla ya kupangwa.
 
Haswa tusipokuwa makini bado tatizo la umeme litaendelea hata bwana la Nyerere likufanya kazi bado kuna shida zinazotokana na miundombinu mibovu ya kusafirisha umeme.
 
Lakini tutachelea zaidi kupiga hatua tutaendelea kuwa na wakosoaji wanalalamika tu bila kuonyesha mipango, mikakati na uelekeo mdalala wa kutatua changamoto hizo mathalani kwenye nishati 🐒

Wakosoaji wasio wabunifu na ambao sio kitisho kwa Taasisi au Serikali iliyopo madarakani ni mzigo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla 🐒
 
Back
Top Bottom