Kama angekuwa Mtikila, Wachadema au CUF au NCCR amesema anaenda msituni angepona?

SIGULULA

Member
May 1, 2013
74
23
Wanajamii,
Nashindwa kabisa kuelewa kwamba hawa wabunge wa katiba wanania njema na sisi au wanataka tufahamu kuwa sisi wanainchi tutake tusitake tutabidi tukubaliane na maoni ya ccm na pale watakaposhindwa watatumia nguvu ambapo ni kutumia mtutu wa bunduki.
Kweli komba ambae ni Kapteni katika jeshi anapata wapi ujasiri wa kusema hayo? Mwenyekiti aliyechaguliwa na kura nyingi mbona nae anakaa kimya nimesikitika sana hata kukata tamaa kabisa kwamba mabillioni yetu yameungua bila sababu. KULIKUWA NA SABABU GANI KUANZISHA BUNGE HILI ?

Hivi haingii akilini kwamba kuna watu ati akina dr nchimbi na wengine wakizungumza ati Mh. Warioba anyamaze ati asiwakoroge wanainchi, hivi ni kwa sababu sisi hatuna uwezo wa kukutana na waandishi wa habari au???????? Wangekuwa wastaarabu wangejaribu kujibu maswali ya Warioba WASIJIDANGANYE WANAINCHI TUNAJUA LA KUFANYA UKWELI UTUWEKE HURU NDIO MBIU YA PASAKA.
Jana kuna mbunge toka Zanzibar ambae alitoa uelewa wa serkali tatu kiuchumi na kutoa mfano wa Uarabuni na muungano wao na akatoa namna sisi tungefuata ilikupata muungano ambao ungetufaidisha kiuchumu. Mheshimiwa huyu hakuungwa na wabunge licha ya kutoa ufafanuzi akinifu ila aliposimama mbunge wakumkashifu Mhe. Warioba alishangiliwa na kupigiwa makofi nikajiuliza hivi hawa ni watoto wa mitaani wanoshangilia matusi ya mitaani au?????Magazeti leo nilidhani pia wangetoa hata neno la Mbunge huyu na ushajaa wa kuelezea serkali 3 lakini kama kawaida yamezibwa mdomo puuuu!

Hivi najiuliza tena kodi zetu zimeungua hivi, kama walipa kodi hakuna njia ya kutafuta ufumbuzi wa kuzuia ulaji huu?????
Wanafunga leo tunawangoja huku mitaani watueleze vizuri walikuwa na maana gani kula pesa zetu bila huruma. Naungana na mtoa maoni aliyesema komba na lukuvi wanatakiwa wasipewe nauli ya kurudi nyumbani kwa uchiochezi wao, makonda apelekwe kwa viongozi wa dini yake akapewe elimu ya kina juu ya AMRI YA 4 ili aweze kuwa na heshima na ulimi wenye kuleta amani kwani hafahamu kuwa mtoto mwenye malezi mazuri ni tunu kwa familia na Taifa lake si uliona Yesu alipowajibu wazazi wake pale kanisani kwa unyenyekevu ingawa alijua wanaelewa kuwa yeye Yesu amekuja kufanya nini hivyo walipaswa wasimuulize maswali mengi.

Mhe. Warioba na wajumbe wote Mungu awalinde, awaongoze awatie nguvu ilimsikate tamaa na yote yanayosemwa dhidi yenu . Takwimu mlizotupa zinakila ukweli kwani mliangalia uzito wa maeneo mfano Pemba na Kigoma kuwa na watoa maoni wengi it was obvious these areas are victim of poor infrastructure, poor economy and most Leaders have been spending less time to these areas BUT YOU WENT AND CONSOLED THEM BY TAKING TIME TO READ THEIR HEARTS!!! BRAVO nadhani wasomi wengi wenye PERMANENT HEAD DAMAGE hawakuliona hilo . CONGRATS…………. VIVA du Warioba Viva du Wajumbe wote tu lemond!
 
image.jpg Ona komba alivyojiandaa ...kuingia msituni.....
 
Ccm wanaamini watanzania wote ni mazezeta na hawana uwezo wa kufanya chochote dhidi yao! Na ndo maana wameamua kuweka kando mawazo ya wananchi dhidi ya katiba waipendayo na kuamua kujadili rasimu yao ya chumbani!
 
Wanaojiita Tanzania One walinishangaza pale wanataka Warioba anyamaze sababu wakati wake wa kuongea umeisha,ningewaona wa maana kama wangekuwa na confidence ya kuwaambia wajumbe wa CCM waache kumtukana na kutuhumu,kumdhalilisha kwani hata yeye ni binadamu.

Hivi kuna sheria inayosema kuwa ukitukanwa ni kosa kujitetea?Wanaponyoosha vidole kwa UKAWA kwamba wamemtusi Mwalimu,je wao wanahaki ya wakutukana wengine?Inashangaza!
 
Ccm wanaamini watanzania wote ni mazezeta na hawana uwezo wa kufanya chochote dhidi yao! Na ndo maana wameamua kuweka kando mawazo ya wananchi dhidi ya katiba waipendayo na kuamua kujadili rasimu yao ya chumbani!
Komba ni mojawapo wa Wabunge wanaosinzia sana Mjengoni,sitashangaa kusikia kauli Kama hizo Maana pengine alisinzia mpaka akaota alipoitwa jina akakurupuka na Kuanza kuropoka Ujinga ili kuwafurahisha wenzake wasije wakamnyang'anya Bendi akabaki na Posho za bunge ambazo hazimtoshi kulingana na matumizi yake na vimada akina Lulu na wenzake, utafiti wa kiina Mara nyingi Watu wanene kupindukia huwa na maamuzi ya ajabu ajabu sana ! Ndio Maana Dunia nzima Unene unapigwa Vita.
 
Serikali mbili zilizopo sasa ni Ghari kuliko Serikali 5-7 Maana Kuna Marais 2 makamu wa Rais 3 ,waziri Mkuu ambaye hana Sauti Zanzibar , Hawa Viongozi ni wengi sana katika Muungano Kama huu ambao hauna Faida kwa Watanganyika umebaki kuwafaidisha wachache wenye mamlaka,tambua huu ni Muungano wa Ajabu uliosalia Duniani ! Watu million 44 wamegeuzwa mazoba na watu million 1.5 tu ,sasa katiba imevunjwa Zanzibar ni Nchi inakula,inakunywa inahudumiwa kwa Pesa hizi hizi za Tanganyika ,Ukweli Zanzibar wamekuwa wajanja zaidi Wamewekeza Lundo la watumishi na Viongozi na Utitiri wa Wabunge ili Kuvuna Mishahara na posho toka Tanganyika , huu ni Muungano wa ajabu Nchi lakini haina pesa ya kujihudumia unategemea Pesa ya Tanganyika.serikali moja au 3 ndio jawabu la kuokoa Pesa ya Tanganyika kwani kila Upande utajitegemea .
 
Back
Top Bottom