Kairuki aeleza sababu wawekezaji kutimka

Ukimruhusu mwekezaji awekeze nchini kwa kutolipa capital goods tax na corporate tax kwa miaka kumi ni bora zaidi kuliko kutokuwa na huo uwekezaji let say anawekeza kwenye kiwanda kitakacho zalisha ajira za watu 1000.

Mwekezaji huyo atanunua umeme, atanunua maji, atanunua mafuta ya magari, atanunua consumables mbalimbali na vitu vyote hivyo vitasaidia mzunguko wa pesa sokoni. Kingine nikuwa wafanyakazi watakao ajiriwa watalipa kodi ya PAYE na pia watakuwa na pesa(income) ya kununua mahitaji yao mbalimbali na kwa hiyo kushamirisha biashara za watu wengine kama za vyakula, mavazi, nyumba za kupanga, watalipa bills za umeme na maji, watapeleka watoto shule, hospitali nk.

Kwa ufupi serikali inatakiwa kutazama vikwazo vya uwekezaji ili kuongeza wawekezaji na kupanua uchumi badala ya kuweka vikwazo vingi ambavyo havitusaidii sana kukuza uchumi wetu.


Pia tunajua tunahitaji pembejeo, trecta, irrigation equipment, dawa, mbolea, elimu ya kilimo kwa wakulima.

Hivi vitu tunaweza kuviruhusu kwa zero tax.

Serikali inaweza kuwapa tax holiday for 10 years plus guarantee to buy 1000 trecta kila mwaka.

Haya matrekta yatasaidia kulima, kutoa mazao ya wakulima shamba ambapo barabara hazipitiki
kuyaleta mjini.

Baada ya miaka mitano unawauzia wakulima haya matrekta.
 
Kwa kiasi kikubwa katika utawala huu, vitendo vya rushwa na urasimu vimepungua. Urasimu na rushwa uliokuwepo katika Awamu iliyopita ulikua mkubwa sana lakini bado wawekezaji walikuwepo wengi, mishahara ilikua ikiongezeka na ajira kibao.

Mh. Waziri jaribu kuupitia tena huo utafiti ulioletewa.
 
Nakubaliana na wewe ubabe mwingi na visasi. Unakuta mtu ana investment kubwa lkn hawalioni hilo wanamtreat kama anafanya biashara kwenye briefcase. Wanadai kodi ambazo ni kubwa mno halafu hamna justification.
Kuna double standards nyingi kwenye namna wanavyowasimamia wafanyabiashara na uelewa wa biashara zenyewe.
Huku TRA ndio balaa....kwenye mabaraza wanasema mfanya biashara asifungiwe biashara....kwenye mikoa wanafunga accoubt za wafanya biashara tena kwa ubabe tu. Najiuliza, kuna mamlaka ngapi zinazoendesha mambo Tanzania? Kufunga account si ndio kufunga biashara na kuchochea njia za mkato za kufanya biashara?
Tanzania, ukishaajiriwa na serikali ina maana hakuna kujari lolote linaloendelea?
 
Nasubiri tuanze kusikia wakiwashusha vyo au kuwafukuza kabisa.. naamini wanatajiwa majina n.k.
 
Rushwa iko kwa wapinzani pia, rushwa haina chama

..lakini ccm mmekuwa mkijitapa kwamba awamu hii mmekomesha rushwa.

..Jiwe ndiyo kikwazo kwa wawekezaji kuja nchini.

..kwanza yeye mwenyewe ana tuhuma za rushwa kama kashfa ya uuzwaji nyumba za serekali, pia ni kiongozi anayechukia sekta binafsi, na ana tabia ya kutofuata sheria.

..muenendo na matamko ya Jiwe ndiyo chanzo cha wawekezaji kughairi kuja Tz.
 
Hawa watu mbona wanayumbisha bongo na akili zetu adi tunachoka yani wanatupigia kelele. Tangu awamu hii iingie madarakani wanasema rushwa, ufisadi, uzembe kazini na urasimu umamalizwa na serikali ya jemedari dakitare John Joseph Pombe Magufuli mara hii tena watumishi wa umma wamekua watafuna rushwa wakubwa na warasimu kiasi cha wawekezaji na wafanyabiashara kutimka mita 100? jamani nyie watu jamani taratibu.
 
Hakuna cha CEO wala waziri wala katibu Mkuu, hapo ni suala la sheria zetu siyo rafiki taasisi nyingi zinatoza tozo hata kabla hujaanza biashara, mfano NEMC ukitaka kuwapeleka kwenye eneo lako lazima uwalipe pesa ya ushauri, uwalipe posho ya na usafiri, Mkemia mkuu naye vivyohivyo ili hali wanalipwa mishahara.

Halafu naona kama tumeajiri watu wengi mpaka wasiohitajika. Ili waendelee kuwepo, lazima walazimishe mambo kama.haya tunayoyaona.
Ingekuwa busara kufanyia utafiti muundo qa wizara na taasisi zake ili kuongeza ufanisi
 
Tatizo hata siyo rushwa...

Tatizo lipo kwenye sera za uwekezaji, sasa zimekua na masharti magumu na yasiyokua na tija...

Lingine vibali vya uwekezaji, work permit, residential permit na vibali vingine vimekua vinatolewa kwa ukiritimba sana zama hizi...

Tatizo ni serikali yenyewe...



Cc: mahondaw
 
Nakubaliana na wewe ubabe mwingi na visasi. Unakuta mtu ana investment kubwa lkn hawalioni hilo wanamtreat kama anafanya biashara kwenye briefcase. Wanadai kodi ambazo ni kubwa mno halafu hamna justification.

Funny enough, they dont care hata kama ukifunga biashara.
Mishahara na rushwa zinazoendana na nafasi walizonazo zinawapa kiburi.
Ingekuwa muhimu kuwa na perfomance agreement na wafanyakazi wa umma, kama ilivyo private sector. Halafu waanze kutafuta feedback kwa wateja using independent institutions. Sio TRA wanaulizana wenyewe kwa wenyewe
 
Back
Top Bottom