Zurie
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 1,835
- 4,671
KAHAMA: Zaidi ya wafanyakazi 1,300 wamekosa ajira, huku Kodi ya Sh. Bilioni 28 ikikosekana baada ya Mgodi wa Dhahabu wa Buzwagi kufungwa rasmi.
Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa mgodi huo unaomilikiwa na Acacia, umefungwa kwa kushindwa kuzaliwa kiwango cha madini hayo kilichotarajiwa.
Kufungwa kwa mgodi huo pia kumeikosesha Wilaya ya Kahama jumla ya Sh. Bilioni 1.7 zilizokuwa zikilipwa kila mwaka, ikiwa ni mrabaha.
Uongozi wa mgodi huo umeeleza kuwa uzalishaji wa dhahabu katika eneo la mgodi umeshuka kutoka gramu 1.35 hadi 1.00 (kwa kila kilo moja ya mchanga/mawe inayochimbwa) kwa mwaka jana. Mgodi huo ulianzishwa mwaka 2009 kwa mtaji wa wawekezaji unaokaribia Sh. Trilioni moja.
Tayari mgodi huo umeanza kuuza baadhi ya mali zake yakiwamo magari, mashine, majengo na vifaa vingine. Mnada mkubwa wa kuuza mali za mgodi huo utafanyika mapema mwezi Machi, 2018.