Kagasheki amulika vitalu vya uwindaji, awataka wasijidanganye kumrubuni kwa fedha

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=3]na Asha Bani[/h]WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Balozi Khamisi Kagasheki, amesema hatawavumilia watendaji wa wizarani kwake ambao wanamiliki vitalu na kwamba tayari ameanza kuwafuatilia kwa hatua zaidi.


Kagasheki alisema hayo jana jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa mkutano na wadau wa uwindaji wa utalii, ambao miongoni mwao ni wapiga picha.

Alisema tayari ameshapata majina ya watumishi sita wanaomiliki vitalu lakini wanavikodisha kwa wawekezaji wengine, hivyo ikithibitika ukweli atawatimua.


“Watu wanasema oooh! Kagasheki anafukuza watu, lakini jamani tuelewane, kwa mtindo kama huo ni lazima kufukuzana, kwa kuwa watumishi kumiliki vitalu vya uwindaji ni kinyume cha sheria ya utumishi wa umma.


Nina mfano hapa, kuna mwindaji mmoja yeye alishindwa kuendesha kitalu. Endapo mtu anashindwa sheria inamtaka arudishe lakini yeye alimtafuta mwindaji wa kigeni na kutaka kumlangua kwa dola 600,000 za Marekani,” alisema Kagasheki.


Aidha waziri huyo pia alitoa rai kwa wawindaji hao kuacha fikra kwamba kutokana na fedha zao watazitumia katika kumlubuni yeye ama mtumishi yeyote kwa masilahi yao, akisema kwa upande wake hatakubali.


“Ninyi mna fedha nyingi, lakini hata kama ni hivyo kwangu hapana, ila tutakuwa tunakaa pamoja, tunakunywa kahawa pamoja lakini kuhusu kunilubuni kwa fedha hapana, na nikigundua imefanyika hivyo kwa mtumishi yeyote, hatua zitachukuliwa pia,” alisema.


Aidha, alionya kwa baadhi ya wawindaji ambao wanaomba vitalu vingi lakini wamekuwa na tabia ya kufanya ulanguzi katika makampuni ya kigeni kwa bei kubwa, akisema atapambana nao kwa kuwa fedha hizo zinatakiwa kuingia serikalini.


Hata hivyo, Kagasheki alisema ni vema kwa watumishi wa wizara hiyo kujipanga na kufanya kazi kwa uadilifu ili kurudisha imani iliyopotea kwa wananchi katika wizara hiyo.


“Jamani haki ya Mungu nasema kutoka moyoni mwangu tutakuja kuonana wabaya kabisa, hii wizara ilitakiwa kuwasaidia wananchi, lakini kutokana na kuwepo kwa watu wasio na huruma na uzalendo, kumekuwa hivyo, pato linalopatikana haliridhishi hata kidogo,” alibainisha Kagasheki.


Kuhusu pato la wizara hiyo, Kagasheki alisema kwa mwaka jana dola bilioni 1.6 za Marekani ziliingizwa nchini, ambapo kwa upande wa uwindaji dola milioni 13.7 za Marekani ziliingia, kiasi alichodai ni kidogo kulingana na umuhimu na ukubwa wa sekta hiyo.


Alisema wawindaji wanataka kuwafanya watu kama ‘majuha’, huku akitolea mfano kuwa ni aibu kwa mamba mmoja kuwindwa kwa dola 1,700 za Marekani, huku katika nchi ya Uswisi mkanda mmoja peke yake wa ngozi ya mamba unauzwa dola 1,200.


“Yaani ukiacha hiyo mikanda, mikoba ya wanawake huuzwa dola 13,000 za Marekani, sasa kwa nini sisi tushindwe kufanya hivyo, tunahitaji rasilimali zetu zitunufaishe?” alihoji Kagasheki.


Alibainisha kuwa ni vema kuangalia sheria na kuzibadilisha, kwa kuwa hazisaidii huku akiitaja sheria namba 39, kifungu (a,b ) ambacho asilimia 25 au 35 ya pato linalotokana na uwindaji ndilo linabaki, wakati iliyobakia inaondoka.


Alisema kutokana na hali hiyo, inatakiwa asilimia iwe 50 kwa 50 ili wananchi, serikali na wawekezaji wote wale matunda hayo.


Chanzo: Tanzania Daima
 
Huyu Jamaa pamoja na kutaka kuhamishia familia yake yote NEC; Anafanya kazi nzuri WIZARA YA MALIASILI na UTALII
 
Chonde chonde Waziri Kagasheki, waokoe watanzania na raslimali zao zinazopotea. Kama mtu ametaka kukodisha kitalu kwa dola 600,000 je serikali ingepata ngapi kwa vitalu vyote vinavyokodishwa?? Ni afadhali kuacha kukodisha vitalu hivyo mpaka tuwe tayari. Nyerere alisema jamani. Mbona wanatuona sisi wajinga sana?? Lakini Mh. hii isiwe nguvu ya soda
 
Waziri Kagasheki angewataja hao wamiliki wa vitalu vingi badala ya kukasirika, awanyang'anye hivyo vitalu.
 
Huyu Jamaa pamoja na kutaka kuhamishia familia yake yote NEC; Anafanya kazi nzuri WIZARA YA MALIASILI na UTALII


Ushaur
i wa bure kwa Mh. Kagasheki Wizara hii ni ngumu kuliko unavyofikiri Zungumza kidogo tenda zaidi. Kama unawajua wenye vitalu huna haja ya kutuambia tafuta ushahidi wa kutosha wafukuze kazi. Pitia historia ya Mawaziri walioingia na wakatoka salama, sikutishi nakutakia kazi njema ila usiwe mwepesi wa kusema kwani si wote waliofukuzwa hapo wana makosa wengine ni mbuzi wa kafara. Kuna msemo katika Biblia unasema " Ajiteteaye kwanza huonekana kuwa ana haki; Lakini jirani yake huja na kumchunguza' tu;iambiwa hapo nyuma kuwa wauza madawa ninawafahamu ninawapa muda mbona kimya........
 
Huyu naye ni msanii tu. Nini hatima ya wale aliosimamisha kwa kashfa ya kuuwawa kwa faru? Wapi taarifa ya tume alounda kuchunguza? Unaweza walishamkatia kitu kidogo akawarudisha kazini.
 
Huyu naye ni msanii tu. Nini hatima ya wale aliosimamisha kwa kashfa ya kuuwawa kwa faru? Wapi taarifa ya tume alounda kuchunguza? Unaweza walishamkatia kitu kidogo akawarudisha kazini.

Kwako kila mtu msanii.
 
Back
Top Bottom