Kagame: Nitagombea Urais tena mwaka 2024, Wananchi bado wana imani kwangu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
1695188119941.png

Akizungumza na Jarida la Jeune Afrique, Rais wa Rwanda, Paul Kagame amethibitisha kuwa atawania nafasi hiyo kwa mara ya 4 kwasababu Wananchi bado wana imani naye.

Kagame aliulizwa anachukuliaje uamuzi wake kwa kulinganisha na Mapinduzi yanayoendelea katika Nchi za Afrika Magharibi, ambapo alijibu Wananchi wa Rwanda ndio wenye uamuzi wa mwisho na yeye ataendelea kuwatumikia kwa kadri anavyoweza.

Kwa uamuzi huo sasa ni rasmi Kagame amefuta kauli yake ya Aprili 2023, aliyosema anatazamia kustaafu na kukabidhi Madaraka baada kuwa Rais kwa miaka 23. Kagame amekuwa Rais tangu mwaka 2000 ambapo mwaka 2015 Serikali ilifanya mabadiliko ya Katiba na kuondoa ukomo wa mihula 2 ya Utawala

===========

Rwanda's President Paul Kagame has said he will run for a fourth term in next year's presidential election.

“Yes, I am indeed a candidate,” Mr Kagame told French-language magazine Jeune Afrique on Tuesday.

Asked about what the West would think about his decision to run again, Mr Kagame said, "I'm sorry for the West, but what the West thinks is not my problem".

"I am happy with the confidence that the Rwandans have in me. I will always serve them, as much when I can."

Mr Kagame had in April said he was looking forward to retiring and handing over power after 23 years in office.

The country's ruling party, the Rwandan Patriotic Front (RPF-Inkotanyi), retained Mr Kagame as its chairman in April. He has led the party since 1998.

Mr Kagame has been president of the East African nation since 2000. A controversial referendum in 2015 removed a two-term constitutional limit for presidents.

He won the last election in 2017 with 98.8% of the vote.

Rwanda under President Kagame has enjoyed relative political stability but critics and human rights groups accuse his government of limiting political freedoms and suppressing dissent.

MWANANCHI
 
Wananchi akimaanisha Yanga? Sema huyu mwamba ana akili kuliko marais wote wa Africa Mashariki. Katika kipindi chote cha uongozi wake alizidiwa IQ na JPM tu.
Alizidiwaje wakati yeye ndo alikuwa mentor wake kiasi cha kumwekea hadi walinzi kutoka rwanda?

Kauli yako ya kwanza ibakie hivyo, jamaa lipo smart sana upstairs.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na hili ndio tatizo la viongozi wa kiafrika hawajui kutundika daruga ikiwa bado wana thamani mbele za wananchi wao. Wanataka mpaka uwezo wao wa kuongoza uishe wabaki kuwa vichekesho.

Japo alitawala kwa muda mrefu lakini Nyerere alikuwa na maono ya mbali sana. Aliachia madaraka ikiwa bado wananchi wanamuona wa maana na mpaka leo anaongelewa kwa heshima.

Huyu atakuja kuwa kama Mugabe, toka alipokuwa anapendwa mpaka kuwa kituko cha madarakani.
 
Jamaa ataachi madaraka kwa

1.Mapimduzi

2.Kifo Cha ugonjwa.

Otherwise hawezi toka hapo abadani Asilani.

Akishinda uchaguzi atasema ndio mara yake ya mwisho

Ila uchaguzi ukikaribia anapata arosto anatamani aendelee kubaki tena na tena.

Atang'oka madarakani kwa staili Ile Ile aliyoingia nayo.
 
Alizidiwaje wakati yeye ndo alikuwa mentor wake kiasi cha kumwekea hadi walinzi kutoka rwanda?

Kauli yako ya kwanza ibakie hivyo, jamaa lipo smart sana upstairs.

Sent using Jamii Forums mobile app
Upumbavu kama huu na wewe kabisa unakubaliana nao.? Yan nchi huru kubwa yenye heshima kama Tanzania ikalindwe na vimigambo hivyo vya hapo pembezon mwa kigoma
 
Nikiona ujinga unaofanyika Libya naona Kagame aendelee miaka mia au hata hapa Tanzania tungejua ujinga huu ungerejea migao ya umeme na upuuzi wote huu namkumbuka sana magufuli
Binadamu hawezi kuishi miaka unayopenda wewe kwasababu ujamleta wewe Duniani, hivyo unashauriwa kuandaa mazingira mazuri kwa kila mwananchi kuwa na afya njema akilini ili ata ukitwaliwa na yule aliekuleta Duniani then unaowaacha nchini waweze kuendeleza kile ulichokianzisha.
Siyo ujingaujinga unaotumiwa na hao ukiowataja.
 
Back
Top Bottom