Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,064
- 22,757
Sikiliza bwana mdogo, EPA ilianza hivi hivi, mara oh pesa za EPA si za Umma. Katolewa kafara Balali. Safari hii, oh pesa za escrow si za Umma. Katolewa kafara Mgimwa. Unakumbuka rada? Mtu kakiri mwenyewe eti kawekewa dola milioni kwenye account akiziita vijisenti! Leo hii mwizi kawa mheshimiwa anatuandalia katiba mpya! Unakumbuka Kagoda ama ulikuwa hujazaliwa? Unakumbuka Meremeta/Buhemba? Mara oh miradi ya Jeshi haihojiwi! Toka lini Jeshi likafanye biashara? Unakumbuka mapanki ya samaki? Unakumbuka biashara ya silaha Congo? Unakumbuka balaa ya Bulyankulu? Wananchi wanafukiwa mgodini, je nani aliwajibishwa?Unaushaid gani kama kaiba mkuu
au na wewe umemezeshwa na kafulila
Mkuu mmi ni tofauti sana na wengi eti sio kisa kasema yeye kafulila na mimi nikurupuke tu nianze kumshabikia lazma nianze kufanya uchunguz kwanza
Aah nilitaka kusahau, unakumbuka REDCO au tuseme Richmond/Richmonduli? Unakumbuka Dr. Mwakyembe alivyoisetiri serikali? Kwa sasa ni Waziri baada ya kuonjeshwa machungu ya kaburi! Unakumbuka ya Mererani? Aliyekuwa balozi wetu Afrika Kusini akikokota trela ya makaburu kuja kuchuma kwenye shamba la bibi? Je unayo habari za Nyabirama na Nyabigena huko Tarime? Wananchi na wanyama wakiathirika na maji ya sumu? Je ya Tulawaka na ya Geita? Vipi ya falme za kiarabu kuivamia Loliondo na kupakia wanyama wetu hai usiku wa manane? And the list goes on and on...! Wakati haya yote yakitendeka na mabilioni yakiliwa na mafisadi, wewe mimi kuruta, uliyejiunga na JF juzi na huyo massange wako, mnaleta upuuzi wenu humu kutetea msivyovijua, mkome...rudini huko huko pangoni mlikotoka.