Kafariki akiwa amejifungia ndani ya ofisi yake, Mke wake alaumiwa

Man Rody

JF-Expert Member
Aug 4, 2022
1,273
2,940
Imetokea leo mchana maeneo ya kituo cha bandari Kurasini. Kuna jamaa ana ofisi yake (frame) ya kuziba pancha na kuongeza upepo ni jirani yetu kabisa na ofisi yetu ndogo (branch) ambayo huwa napita siku moja kila wiki.

Huyu jamaa ni mkimya sana sijawahi kuzoeana nae ila salamu tu na nimewahi kumuomba chenji mara kadhaa.

Sasa basi asubuhi ile nafika tu pale ofisini nje nilikuta watu wanne wanaongea wanajadili kuwa jamaa hajafungua ofisi siku ya pili, simu yake haipatikani na wana wasiwasi yumo mule ndani maana amekuwa akilala ndani ya ile frame yake kwa wiki kadhaa baada ya kukorofishana na mke wake.

Nilitoa salamu, nikasikiliza mawili matatu ya wale jamaa nikaingia ndani. Kijana wa pale ofisini akaanza kunipa mkasa mzima coz yeye anashinda pale daily. Akanieleza yule jamaa alikuwa ni mlevi sana ila wiki kadhaa alizidisha ulevi wa kupindukia na chanzo anasema alikuwa na ugomvi na mke wake hadi kupelekea kuhama kwake akaanza kulala mule ofisini. Hii ishu walikuwa wanajua watu wachache sana mana jamaa ni mkimya mno.

Basi kama mnavojua protocol za kibongo kuchelewesha mambo, jamaa baada ya kushauriana pale walimfata mwenye nyumba anaekaa nyuma ya zile frame kumshirikisha juu ya hofu yao kuwa jamaa yumo mule ndani, mwenye nyumba akaenda kwa mjumbe kaandikiwa barua wakaenda polisi ili waje nao pale wabomoe kuingia

Hizi taratibu zote zilichukua saa nyingi yaani mpaka polisi wanakuja pale ni saa 8 mchana, hili nalo lilinikera sana!

Walimkuta kweli jamaa kajikunyata sakafuni mule ndani anatoka mapovu ila bado anapumua ndio kumpandisha gari kumuwahisha hospitali ya bandari ambapo haikuchukua round akaaga uhai.

Watu wanamlaumu mke wake jamaa kufa kwa style ile kidhalili japo wote hatujui ugomvi wao ni wa nini, mwenye nyumba kapagawa anawaomba wapangaji wote wasiseme kuwa jamaa alikuwa analala pale kuepuka usumbufu wa upelelezi.

Mchana huo huo nikapokea taarifa ya mjomba wangu kapata ajali mbaya sana ya gari mkoani na kufariki hapo hapo, eeh Mungu tunaomba mwisho mwema 🤲

Haya maisha jamani, kila mtu ana mzigo wake anaotembea nao kila siku na yeye pekee ndio anajua yanayomsibu. Hakuna mwalimu bora zaidi ya muda na yote tunayopitia ni sehemu ya mafunzo.
 
Imetokea leo mchana maeneo ya kituo cha bandari kurasini.. kuna jamaa ana ofisi yake (frame) ya kuziba pancha na kuongeza upepo ni jirani yetu kabisa na ofisi yetu ndogo (branch) ambayo hua napita siku moja kila wiki. Huyu jamaa ni mkimya sana sijawahi kuzoeana nae ila salamu tu na nimewahi kumuomba chenji mara kadhaa.
Wanawake hawana Huruma wapo kwa ajili ya kuua wanaume
 
Imetokea leo mchana maeneo ya kituo cha bandari kurasini.. kuna jamaa ana ofisi yake (frame) ya kuziba pancha na kuongeza upepo ni jirani yetu kabisa na ofisi yetu ndogo (branch) ambayo hua napita siku moja kila wiki. Huyu jamaa ni mkimya sana sijawahi kuzoeana nae ila salamu tu na nimewahi kumuomba chenji mara kadhaa.
yanayomsibu..hakuna mwalimu bora zaidi ya muda na yote tunayopitia ni sehemu ya mafunzo.
WaTz kwa kupenda lawama!
 
Back
Top Bottom