Kadi ya CCM yamponza Slaa... Sasa ashinikizwa kujiuzulu nafasi yake!

hujui chama kinaathirika kiasi gani.unakimbilia mafanikio wakati gari ulilopanda linatembelea matairi matatu.
Sugua ubongo wako,ukimya wa mzee mteni na mbowe niishara ya nini????

You are a known liability all the best
 
Slaa alipo lipua yale mabomu pale mwembe yanga kwa kuwataja mafisadi hamkujua kuwa alikuwa na kadi ya ccm?! Na ikawaje mkataka kumuua kwa kuanza kumuwekea vinasa sauti hotelini kule dodoma?! Hamkujua kuwa alikuwa na kadi ya ccm?! Alipogombea ubunge na kuwabwaga mara 3 hamkujua kuwa alikuwa na kadi ya ccm?!

Tunajidili wizi wa fedha na raslimali zetu slaa kumiliki kadi ya ccm sio inshu ya maana yuko chadema na ameiweka chadema kwenye ramani nyingine ki siasa.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Slaa alipo lipua yale mabomu pale mwembe yanga kwa kuwataja mafisadi hamkujua kuwa alikuwa na kadi ya ccm?! Na ikawaje mkataka kumuua kwa kuanza kumuwekea vinasa sauti hotelini kule dodoma?! Hamkujua kuwa alikuwa na kadi ya ccm?! Alipogombea ubunge na kuwabwaga mara 3 hamkujua kuwa alikuwa na kadi ya ccm?!

Tunajidili wizi wa fedha na raslimali zetu slaa kumiliki kadi ya ccm sio inshu ya maana yuko chadema na ameiweka chadema kwenye ramani nyingine ki siasa.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums


CCM ya sasa hivi ni hamnazo wa viwango vya kipekee. Wangekuwa na akili timamu wangeshagundua wanachokifanya (CCM) sasa hivi ni kumtangaza Dr Slaa rasmi kuwa yeye ndiye tishio la mafisadi na kwamba yeye (Dr Slaa) ndio kifo cha CCM. Na siku zote nimekuwa naamini CCM pamoja na vyombo vya dola wamekuwa makatibu waenezi wazuri sana wa CHADEMA. Hii ya card is a classic example ya 'own-goal' strategy toka CCM.

Na kama imewachukuwa zaidi ya miaka 15 kugundua kuwa Dr Slaa bado ana card ya CCM, je watawezaje kugundua wizi unaofanywa na makampuni ya madini, simu na wapeleka makontena HongKong? Watu wazembe kiasi hiki wanafaa kuongoza nchi?
 
Na nyie ccm msituchoshe bure na card oh card. Sasa sisi wananchi tunataka kujua lini hela za uswiss zitarudi kuwasaidia watoto yatima omba omba barabarani as if nchi ni masikini mno, hela za epa, pembe za ndovu na biashara kichaa ya kuuza wanyama wetu, migodi kuwapa wageni ili hali wananchi wanapata shida ya kupindukia na hata kufikia kuwahamisha maeneo yao ili mradi mwekezaji apate pa kufanyia kazi zake ewee mungu rudi sisi wananchi wako tunaangamia utarudi lini. Watu wanajijali matumbo yao tuu ili mradi waishi vizuri hawajali damu za watoto zinazomwagika na kukosa huduma muhimu mungu njoo njoo haraka tunakuhitaji.

takribani wiki ya pili sasa tangu sakata la umiliki wa kadi ya ccm lilipoibuliwa rasmi na katibu mwenezi wa ccm nape nauye.
Hili sakata linaonekana kuchukua sura mpya kabisa katika uso na kioo cha siasa za chadema ndani ya nchi.
Litazua gumzo kubwa zaidi endapo hali ya kulipuuza kunakofanywa na viongozi/wazazi wa chadema kutabaki hivi hivi bila kauli yoyote.lakini wahenga walisema njiti moja ya kiberiti inaunguza nyumba yenye uzuri wa dhahabu na mwonekano wa theruji.
Maswali yangu kwa wana jf wenzangu makini(great thinkers) kuhusiana na sakata hili.

1.kwanini baba mzazi/mzee wetu edwin mtei yupo kimya kabisa kabisa na hili sakata linaloelekea kuleta dhoruba ya kisiasa ndani ya chama?
Note:mzee edwin mara kadhaa amekuwa mstari wa mbele kukosoa/kutoa onyo kwa swala lolote lile linaloonekana kuhalipo sawia ama kwa wakati au kwa mfumo mzima wa chama.

2.kwanini freeman mbowe hajajitokeza kuzungumzia sakata hili ili hali anaona wazi linakoeleka si kuzuri.leo bavicha mwanza wamefukuta,kesho?juzi tuliona mjumbe wa mkutano mkuu akifukuta?keshokutwa je????
Haya wajumbe wakiungana kutaka mkutano mkuu wa dhararu kama katiba inavyowaruhusu?mbowe umechukua innicitives gani kwenye kunusuru swala hili lisikiathiri chama?

3.wana jf,je kunahaja ya kila jambo kukimbilia kuishutumu ccm?pili uchambuzi wetu wa makosa/ama kujikwaa kwa viongozi wetu wa chadema umejikita atika mlengo gani?
Frankly speaking wana jf.
Hili sakata la kadi ya ccm kwa dr.slaa lingekuwa ni kwa viongozi hawa(mbowe,zitto,shibuda,lissu,arfi) tunge toamaoni gani?
4.john heche tutegemee lini ukitoa tamko kuhusu swala hili?kumbuka rekodi yako ya nyuma kuwafokea viongozi flani wa chadema.nitafurahi ukisimama na kutoa neno kuhus hili hasa ukizingatia bavicha mmesha washa moto.
Naomba tujadili kwa kukwepa mapenzi ya viongozi wetu mmoja mmoja,tujikite kwenye mstakabali wa chadema
 
Wewe umetumwa sijui umeshapata shilingi ngapi kwa leo hii ila ujue utalipwa hapa hapa duniani ivi unajua kwa kupokea hela zako hizo za kuandika uchochezi unaangamiza vizazi vingapi? Na siku ya kihama utajibu nini. Na mtu angekuambia huishi tena zaidi ya miezi miwili utafanyaje? Watu embu amkeni msikubali kutumiwa bila kujua hatima ya maisha yako na kiizazi chako. Ona misri ona cyria na kungineko.
utaishia hapo tu..ukiambiwa uongeze neno huna.akili za kuazima matumizi yake yakubahatisha
 
10 DECEMBER 2012

Kadi ya CCM yamponza Slaa *Sasa ashinikizwa kujiuzulu nafasi yake *Wanachama wadai kukosa imani naye




Na Mwandishi Wetu

MJUMBE wa Mkutano Mkuu Taifa CHADEMA, mkoani Mbeya, Bw. Edo Mwamalala, amemtaka Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Willibrod Slaa, kujiuzulu wadhifa wake kwa madai ya kikidhalilisha chama chao kwa kuendelea kumiliki kadi ya CCM.

Bw. Mwamalala aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea jinsi alivyoguswa na kitendo cha Dkt. Slaa kukiri hadharani kumiliki kadi ya CCM wakati anajua dhamana kubwa aliyopewa katika chama hicho.

Alisema katiba ya chama hicho sura ya tano, ibara ya kwanza kifungu kidogo cha sita 5.1.6 kinachosema, mwanachama wa chama hicho hapaswi kuwa mwanachama wa chama kingine cha siasa baada ya kujiunga CHADEMA.

Alisema Dkt. Slaa ameanza kuwapa mashaka wanachama wa chama hicho na wengine kuamini huenda huenda yupo CHADEMA kwa kama kibaraka wa CCM anayetumiwa kwa mambo mbalimbali.

“Hivi karibuni Dkt. Slaa amekiri kumiliki kadi ya CCM na kudai kuitunza kama kumbukumbu, halii hii inaonesha bado anatumukia vyama viwili vya siasa kwa maana ya CCM na CHADEMA.

“Umefika wakati wa kiongozi huyu kuwajibishwa na chama, katika mfumo wa vyama vingi, kiongozi wa chama lazima awe mfano kwa wengine hivyo kitendo hiki kinaleta mashaka makubwa,” alisema.

Alimtaka Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Freeman Mbowe, kuchukua hatua badala ya kuliacha jambo hilo hewani na kama atashindwa kulishughulikia, viongozi wengi zaidi ndani ya chama hicho wanaweza kujitokeza na kusema wanamiliki kadi za CCM.

“Hili ni jambo la hatari sana, wanachama wataamini chama chetu kinaendeshwa na vibaraka wa CCM, haiwezekani Katibu Mkuu wa chama awe anamiliki kadi ya chama tawala.

“Wapo ambao watajitokeza kunikejeli na kudai nimetumwa lakini mfumo wa demokrasia, unatoa fursa kwa kila mtu kueleza kile anachokiona ili kujenga siasa bora nchini,” alisema.

Alisema Dkt. Slaa amekosa uadilifu, sifa za kukitumikia chama hicho na kuongeza kuwa yupo tayari kuchukiwa kwa kueleza ukweli wa kile anachokiamini kama mwanachama.

Bw. Mwamalala alisema kama chama hicho kitashindwa kuchukua hatua zozote, atapeleka hoja binafsi katika Mkutano Mkuu kutaka Dkt. Slaa ajadiliwe na kuchukuliwa hatua.

“Wakati Dkt. Slaa anondoka CCM, alipaswa kuwaachia kadi yao, sisi wenye mapenzi mema na CHADEMA, hatuko tayari kuona tunaishi ndani na kadi ya chama ambacho tunataka kukiondoa madarakani katika Uchaguzi Mkuu 2015,” alisema.




Tupatieni tathmini ya kujivua gamba imefikia wapi

je fedha ya EPA imerudi na mmegawana vipi au imepelekwa wapi

Je mbona umeme unakatika kila mara

je miradi ya Buzwagi, meremeta, kiwira na miradi tata, mmechukua hatua gani

Je fedha za rada zimekuja lini na zimefanya nin

je kwann watz maskini ili hali ni nchi tajiri kwa mali asili duniani

je mmerudisha mbuga yetu ya Loliondo mliyouza kwa waarabu

Je Kinana amerudisha meno yetu ya tembo na amechukuliwa hatua gani

je Mangula naye amelipa fedha za EPA na kwann naye anatuhumiwa kuhusika na uhujumu uchumi wa nchi

jamani wengine ongezeni list ili ccm watupe majibu

je kwani tiketi ya basi, treni na ndege huwa zinarudishwa kwa nani. je nani amerudisha kadi ya CCJ kwa nani n.k.
 
Tusifike mbali sana,Mtei kuwa kimya kutoa tamko ni ishara ya nini?Ukizingatia sakata hili ni kubwa sana kwa uhai wa chama.Vijana na wazee wameshaanza kupepesa macho kusikia nini kinatokea.
Mzee mtei tafadhali kulikoni???
102lABDA MAMA YAKO NA VIJANA WA MALOWITANI SIO VIJANA SISI TUNAOJUA TUNTEMEKE AKA INVISIBLE HUTUPATI NCHI HII SIO YA WALE WALIOZALIWA MLANGO WA NYUMA WENYE MABABA WA TATU
 
ni kawaida yako...povu likikuisha tutajadiliana kwa utulivu,kwa sasa endelea kubwabwaja

ni kwamba umetoka usingizini tuu, na papara za magamba nani hajui.hata bungeni huwa wanakurupuka kama wewe baadaye ndio waziri mkuu anawaambi akw asauti ya kubembeleza CDM walikuwa sahihi,i;a hawakusema kwa heshima tuu, basi magamba yana relax.


In reality ukiona tunajadiliana kwa utulivu ,ujue kwa kiasi fulani ubongo wako umeanza kuwa activate temporarily kabla hauja dischrge haraka tena.
 
kwani kenge huwa aajitambulisha kwenye msafara wa mamba???pia labda hujui ni namna gani dr.slaa ameingia chadema na mkao wake ulikuwaje ndnai ya chama hadi mwaka 2007.
Slaa amevaa nguo za ccm akiwa chadema meeting kwa sababu ya historia yake na namna alivyoweka siasa zake moyoni mwa ccm.
Hey,utakapo tajiwa tarehe aliyolipia kadi ya ccm ndipo uataamini babu akili yake inaliwa na virus wenye biological name josebia

shida ulikaririshwa, mambo mengi Nape alijibiwa na kuulizwa maswali akasepa.Sasa kama wewe ndio kiporo kama wassira na Komba, na ndio umemka lazima ujibu kama rehearsal yenu ilivyokuja.

Kwa taarifa yako , hata ingelipia muda huu, hakuna gamba mwenye ushahidi kuwa ni Dr. alilipia kwa hela yake na si magamba wame simulate zoezi a ulipaji, wakidhani ndio njia rahisi ya kuhujumu democrasia.

Thread inayohusu upuuzi wa CCM hii hapa
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-zao-ni-aibu-mbaya-ni-fikra-nyembamba-12.html
 
Na nyie ccm msituchoshe bure na card oh card. Sasa sisi wananchi tunataka kujua lini hela za uswiss zitarudi kuwasaidia watoto yatima omba omba barabarani as if nchi ni masikini mno, hela za epa, pembe za ndovu na biashara kichaa ya kuuza wanyama wetu, migodi kuwapa wageni ili hali wananchi wanapata shida ya kupindukia na hata kufikia kuwahamisha maeneo yao ili mradi mwekezaji apate pa kufanyia kazi zake ewee mungu rudi sisi wananchi wako tunaangamia utarudi lini. Watu wanajijali matumbo yao tuu ili mradi waishi vizuri hawajali damu za watoto zinazomwagika na kukosa huduma muhimu mungu njoo njoo haraka tunakuhitaji.

wana Cyclic reasoning, hawawezi toa hapa..Kaa popote CCM watarudi ktk same point over and over.Nape kajibiwa na maswali kashinda jibu, sasa wanamiwngiza idiot mwingine amabaye naye hajui ni wa kueleweshwa, kisha anakuja mwingine tena.Hii ndiyo CCM haiwezi kuja na jibu lolote reasonable kwa vile huwa hawafikirr kabisa kama vile hawakujaliwa hilo baad aya kuingia CCM

INGIA CCM VUA USTAARABU NA FIKRA-Kama unavyovua viatu sehemu takatifu.CCM wanakuvua fikra na ubongo.
 

Padri hapo amekujaje? Tatizo hapo mkuu naona una udini udini udini,maskini wee!


Ehh kumwita Padri nimeshakuwa mdini? Yaani kumwita mtu kwa kazi yake aliosomea ni au kwa cheo chake ni udini? Mbona sijakusoma! Hivi Ponda tukimwita Sheikh Ponda ni udini? Na Kilaini, tukimwita Askofu Kilaini ni udini? Au Slaa sio Padri?
 
Kwa hiyo wewe hiyo ianakuhusu nini? Hypuyo Jk unayemhusudu amefumbia macho mali za umma zinaporwa. mishahara kiduchu, ajira hakuna, hizi mali zingenga shule, barabara, madaraja, na wote tungenufaika.
Kwa hiyo kupora wake za watu ni sawa tu kwa vile haikuhusu?
Mtawahusudu na majambazi.

Kama bara bara zinazojengwa huzioni na hata kazi huna, wa kujilaumu ni wewe mwenyewe.
 
Hiki ni chama cha kidemokrasia,nategemea kuona haki ya kutolewa matamko inatendeka sawia kabisa.
John heche tunahitaji kuina unatoa tamko hapa,kwa sababu u mstari wa mbele kabisa kupinga viongozi wengine ndani ya chama

Bila kumtaja Heche hunyi? Bavicha utaisikia tu we mpambe wa Zitto
 
Last edited by a moderator:

Takribani wiki ya Pili sasa tangu sakata la Umiliki wa Kadi ya CCM lilipoibuliwa rasmi na katibu mwenezi wa CCM nape Nauye.
HILI SAKATA LINAONEKANA KUCHUKUA SURA MPYA KABISA KATIKA USO NA KIOO CHA SIASA ZA CHADEMA NDANI YA NCHI.
LITAZUA GUMZO KUBWA ZAIDI ENDAPO HALI YA KULIPUUZA KUNAKOFANYWA NA VIONGOZI/WAZAZI WA CHADEMA KUTABAKI HIVI HIVI BILA KAULI YOYOTE.LAKINI WAHENGA WALISEMA NJITI MOJA YA KIBERITI INAUNGUZA NYUMBA YENYE UZURI WA DHAHABU NA MWONEKANO WA THERUJI.
MASWALI YANGU KWA WANA JF WENZANGU MAKINI(GREAT THINKERS) KUHUSIANA NA SAKATA HILI.

1.Kwanini Baba Mzazi/Mzee wetu Edwin Mtei yupo kimya kabisa kabisa na hili sakata linaloelekea kuleta dhoruba ya kisiasa ndani ya chama?
NOTE:Mzee Edwin mara kadhaa amekuwa mstari wa mbele kukosoa/kutoa onyo kwa swala lolote lile linaloonekana kuhalipo sawia ama kwa wakati au kwa mfumo mzima wa chama.

2.Kwanini Freeman Mbowe hajajitokeza kuzungumzia sakata hili ili hali anaona wazi linakoeleka si kuzuri.LEO BAVICHA mwanza wamefukuta,Kesho?Juzi tuliona Mjumbe wa mkutano mkuu akifukuta?Keshokutwa je????
Haya wajumbe wakiungana kutaka mkutano mkuu wa dhararu kama katiba inavyowaruhusu?Mbowe umechukua innicitives gani kwenye kunusuru swala hili lisikiathiri chama?

3.WANA JF,JE kunahaja ya kila jambo kukimbilia kuishutumu CCM?Pili uchambuzi wetu wa makosa/ama kujikwaa kwa viongozi wetu wa CHADEMA umejikita atika mlengo gani?
FRANKLY SPEAKING WANA JF.
Hili sakata la Kadi ya CCM kwa Dr.slaa lingekuwa ni kwa viongozi hawa(MBOWE,ZITTO,SHIBUDA,LISSU,ARFI) tunge toamaoni gani?
4.JOHN HECHE tutegemee lini ukitoa tamko kuhusu swala hili?Kumbuka rekodi yako ya nyuma kuwafokea viongozi flani wa chadema.Nitafurahi ukisimama na kutoa neno kuhus hili hasa ukizingatia BAVICHA mmesha washa moto.
Naomba tujadili kwa kukwepa mapenzi ya viongozi wetu mmoja mmoja,Tujikite kwenye mstakabali wa CHADEMA

Fukuteni tu na hiyo kadi kama mnadhani ina msaada kwenu, wote mnaoona hiyo kadi ni ishu ya muhimu sana kwenu na inawachomachoma mkiwa CHADEMA ondokeni muwaachie wanaojua chama na uanachama ni nini sio kila siku kulialia kadi, kadi, kadi, kadi, afu eti mnataka Mbowe na Mtei watoe kauli kisa upuuzi wenu. ngoma yenu ya wapumbavu mtaicheza wapumbavu wenyewe, you will not drag into this people with their sound minds!
 
Propaganda za watu wengine Bwana! Eti 'Dr Slaa ni pandikizi' la CCM! Hizi ni kampeni za magamba na zinawasuta moja kwa moja.

Kama ni 'pandikizi' wao basi anaifanyia Chadema kazi nzuri sana ya kuwabomoa magamba wenyewe.

Dr Slaa alifanikiwa kupunguza kura za Jk kutoka asilimia 80 hadi asilimia 61 ktk uchaguzi wa 2010, na ripoti ya juzi juzi ya REPOA nayo yataja kuwa umaarufu wa CCM unapungua sana.

Yote haya ni kutokana na juhudi za huyo mtu sasa wanamwita 'pandikizi' wao! Pandikizi gani anaewamaliza wenyewe? Hebu nielewesheni hapo. Naomba Watz tusiburuzwe na propoaganda za kipumbavu za magamba, kwani kwa Dr Slaa imekula kwao, na hili wanalifahamu, kina Nape hawapati usingizi.
 
Propaganda za watu wengine Bwana! Eti 'Dr Slaa ni pandikizi' la CCM! Hizi ni kampeni za magamba na zinawasuta moja kwa moja.

Kama ni 'pandikizi' wao basi anaifanyia Chadema kazi nzuri sana ya kuwabomoa magamba wenyewe.

Dr Slaa alifanikiwa kupunguza kura za Jk kutoka asilimia 80 hadi asilimia 61 ktk uchaguzi wa 2010, na ripoti ya juzi juzi ya REPOA nayo yataja kuwa umaarufu wa CCM unapungua sana.

Yote haya ni kutokana na juhudi za huyo mtu sasa wanamwita 'pandikizi' wao! Pandikizi gani anaewamaliza wenyewe? Hebu nielewesheni hapo. Naomba Watz tusiburuzwe na propoaganda za kipumbavu za magamba, kwani kwa Dr Slaa imekula kwao, na hili wanalifahamu, kina Nape hawapati usingizi.

Nimeipenda hiyo. Magamba na vibaraka wao ndani ya CDM wana kampeni za kijinga sijawahi kuona. Big up DR Slaa -- 'upandikizi' wako wailetea Chadema mafanikio makubwa.

Na bado magamba watabuni kila mbinu - watazidi kujichamba hadi watashika ki*****!!
 

Hilo neno la 'pandikizi' definition yake inatoka ktk vichwa vya akina Nape ambao hawawezi kutazama zaidi ya urefu wa pua zao!

Inasikitisha kwa kweli. Yaani Nape anataka wafuasi wa Chadema waamini kwamba Dr Slaa ni 'pandikizi' wa CCM na hivyo ang'olewe? Pandikizi anayewamaliza CCM na asiyewapa usingizi? huenda labda ni pandikizi hostile -- yaani aliyeasi!

No Nape! Try another strategy! Please do!
 
Hii nzuri sana , 2010 wakati tunakusanya michango ya kampeni za CDM , mapandikizi wetu ndani ya ccm ndiyo waliyotuchangia sana. Nakumbuka kuna mtu mwenye cheo ccm alinipa Mbuzi niwachinje ili kutunisha mfuko
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom