Kadi ya CCM yamponza Slaa... Sasa ashinikizwa kujiuzulu nafasi yake!

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
10 DECEMBER 2012

Kadi ya CCM yamponza Slaa *Sasa ashinikizwa kujiuzulu nafasi yake *Wanachama wadai kukosa imani naye

Na Mwandishi Wetu

MJUMBE wa Mkutano Mkuu Taifa CHADEMA, mkoani Mbeya, Bw. Edo Mwamalala, amemtaka Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Willibrod Slaa, kujiuzulu wadhifa wake kwa madai ya kikidhalilisha chama chao kwa kuendelea kumiliki kadi ya CCM.

Bw. Mwamalala aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea jinsi alivyoguswa na kitendo cha Dkt. Slaa kukiri hadharani kumiliki kadi ya CCM wakati anajua dhamana kubwa aliyopewa katika chama hicho.

Alisema katiba ya chama hicho sura ya tano, ibara ya kwanza kifungu kidogo cha sita 5.1.6 kinachosema, mwanachama wa chama hicho hapaswi kuwa mwanachama wa chama kingine cha siasa baada ya kujiunga CHADEMA.

Alisema Dkt. Slaa ameanza kuwapa mashaka wanachama wa chama hicho na wengine kuamini huenda huenda yupo CHADEMA kwa kama kibaraka wa CCM anayetumiwa kwa mambo mbalimbali.

"Hivi karibuni Dkt. Slaa amekiri kumiliki kadi ya CCM na kudai kuitunza kama kumbukumbu, halii hii inaonesha bado anatumukia vyama viwili vya siasa kwa maana ya CCM na CHADEMA.

"Umefika wakati wa kiongozi huyu kuwajibishwa na chama, katika mfumo wa vyama vingi, kiongozi wa chama lazima awe mfano kwa wengine hivyo kitendo hiki kinaleta mashaka makubwa," alisema.

Alimtaka Mwenyekiti wa chama hicho Bw. Freeman Mbowe, kuchukua hatua badala ya kuliacha jambo hilo hewani na kama atashindwa kulishughulikia, viongozi wengi zaidi ndani ya chama hicho wanaweza kujitokeza na kusema wanamiliki kadi za CCM.

"Hili ni jambo la hatari sana, wanachama wataamini chama chetu kinaendeshwa na vibaraka wa CCM, haiwezekani Katibu Mkuu wa chama awe anamiliki kadi ya chama tawala.

"Wapo ambao watajitokeza kunikejeli na kudai nimetumwa lakini mfumo wa demokrasia, unatoa fursa kwa kila mtu kueleza kile anachokiona ili kujenga siasa bora nchini," alisema.

Alisema Dkt. Slaa amekosa uadilifu, sifa za kukitumikia chama hicho na kuongeza kuwa yupo tayari kuchukiwa kwa kueleza ukweli wa kile anachokiamini kama mwanachama.

Bw. Mwamalala alisema kama chama hicho kitashindwa kuchukua hatua zozote, atapeleka hoja binafsi katika Mkutano Mkuu kutaka Dkt. Slaa ajadiliwe na kuchukuliwa hatua.

"Wakati Dkt. Slaa anondoka CCM, alipaswa kuwaachia kadi yao, sisi wenye mapenzi mema na CHADEMA, hatuko tayari kuona tunaishi ndani na kadi ya chama ambacho tunataka kukiondoa madarakani katika Uchaguzi Mkuu 2015," alisema.

Oh wow KAMA ni KWELI NAPE NNAUYE anastahili Zawadi ya MELI toka kwa SERIKALI ya CCM...Wamapiga CHINI MPINZANI wa URAIS 2015? Oh... Sasa na ZITTO KABWE atachekelea.... ataingiza U-CCM ndani ya CHADEMA kiulaini...

+ MIMI ninavyoona kuwa na KADI za CHAMA FULANi sio ITIKADI kuwa wewe ni MPENZI;
Angalia CCM ilisema ina Wanachama zaidi ya MILIONI TANO; Walioipigia kura baada ya kuchakachua Milioni 2,034,500 watanzania wenye uwezo wa kupiga kura na waliojiandikisha ni 18 Million
 
Dkt. Slaa amekiri kumiliki kadi ya CCM na kudai kuitunza kama kumbukumbu.Kwangu mimi hakuna tatizo kubaki na kadi ya magamba kama alivyosema ni kwa ajili ya kumbukumbu.
 
Tumechoshwa na hii stori ya kadi.

Umechoshwa?! Mbona huchoshwi na kelele za ufisadi zinazopigwa na CDM! Usichoke ndo ukweli Padri Slaa bado anipenda CCM. Slaa aliingia CDM sio kwa lengo lakuiondoa madarakani CCM, wala si kwa mapenzi alonayo kwa CDM! Kilochompeleke CDM ni bada ya kutoswa ubunge katika CCM. Uroho wa mdaraka, hbado anaipenda CCM, na akitoswa tu CDM anarudi CCM na.kadi yake anayo. Yeye na Shibuda hawana tofauti, sio wapinzani.ni wachumia tumbo tu.

Ubaya CDM ni wabaguzi sana, kama ishu hii ya kumiliki kadi ya CCM ingekuwa kwa Zito, basi angekuwa ameshalazimishwa ajiuzulu kwa maandamano! Wabaguzi wakubwa! Sasa muondoeni huyo Padri kama mnaubavu?
 
Dkt. Slaa amekiri kumiliki kadi ya CCM na kudai kuitunza kama kumbukumbu.Kwangu mimi hakuna tatizo kubaki na kadi ya magamba kama alivyosema ni kwa ajili ya kumbukumbu.
na mimi nakubaliana nawe kabisa. kama kadi iko kama souvenir sioni shida; kama anailipia na kutoa michango ya uanachma wa ccm kwa mujibu wa katiba ya ccm, hiyo ingekuwa ndo hoja ya kupigia kelele mzee ajiuzulu!
 
Chadema, sasa ni muda muafaka wa kuanzisha chuo cha mafunzo ya siasa na sera za chama. Vinginevyo safari itakuwa na bumps nyingi. Anyway hili jambo ni dogo lakini linaweza kuwa kubwa kwa baadhi ya mental levels.

Sasa tusonge mbele. Hakuna haja ya kujadili kwa sababu dr slaa hana na wala hatapata tatizo lolote kwa hizi tuhuma.
 
Umechoshwa?! Mbona huchoshwi na kelele za ufisadi zinazopigwa na CDM! Usichoke ndo ukweli Padri Slaa bado anipenda CCM. Slaa aliingia CDM sio kwa lengo lakuiondoa madarakani CCM, wala si kwa mapenzi alonayo kwa CDM! Kilochompeleke CDM ni bada ya kutoswa ubunge katika CCM. Uroho wa mdaraka, hbado anaipenda CCM, na akitoswa tu CDM anarudi CCM na.kadi yake anayo. Yeye na Shibuda hawana tofauti, sio wapinzani.ni wachumia tumbo tu.

Ubaya CDM ni wabaguzi sana, kama ishu hii ya kumiliki kadi ya CCM ingekuwa kwa Zito, basi angekuwa ameshalazimishwa ajiuzulu kwa maandamano! Wabaguzi wakubwa! Sasa muondoeni huyo Padri kama mnaubavu?

UKO CCM kwa sababu kikwete ni mwislamu, 2015 atagombea lowassa utarudi CUF!.. CDM akigombea Zitto utataka kote. Mwanamke mwenye tabia hii anaitwaje vile?
 
Kadi ya CCM aliyopewa EDDO Dodoma alipotaka kurudi CCM na Shitambala aliirudisha kwa nani?.. Vocha anazopewa na Nape na Mwigulu atazilipa lini? Hela za kina Nape alizopewa kuandaa press conference na kugharamia mizunguko yake DSM atarudisha lini?
 
mkuu umechoshwa wewe sie wengine hii ni habari mpya...kiongozi wa chadema anaienzi kadi ya ccm.

kwani yeye nnape, mwakyembe, samwel sitta wakiwa km waanzilishi wa chama cha ccj je kadi za ccj walizirudisha au ndo mnatubabaisha tu, tnaomba mjibu juu ya ufisadi wa epa, utoroshaji wa wanyama thru kia, au mnatusaaulisha taratibu
 
Mkuu umechoshwa wewe sie wengine hii ni habari mpya...kiongozi wa Chadema anaienzi kadi ya CCM.

Wassira, Ngawaiya, Aman Warid, Msabaha, Guninita, Bagenda, Lamwai walirudisha lini kadi za upinzani? Acheni UDINI! najua kama kawaida yako nikisema UDINI unaruka futi mia!
 
Hata Musa wakati anawasafirisha wana wa Israeli toka Misri kuelekea nchi ya ahadi, alikutana na changamoto nyingi kutoka kwa wana wa Israeli,wakimuonyesha kutokuwa na imani naye na kusahau kwamba ndiye aliyewavusha bahari ya Shamu ili wasiuawe na majeshi ya Misri.

Mafanikio haya tuliyonayo Chadema asilimia kubwa yametokana na juhudi za Dr Slaa.
Na huyu ndiye mtu pekee wa CHADEMA ambaye ccm inamuogopa, na ambaye anaweza kubadili historia ya nchi hii.
 
Hivi inakuwaje? wanyama pori wanaibiwa kwa kutumia ndege ya jeshi la nchi ya kiarabu mbele ya vyombo vya ulinzi na usalama, Viongozi wa jeshi wasijue, viongozi wa polisi wasijue, viongozi wa usalama wa taifa wasijue, viongozi wa serikali na raisi wasijue!!!!!!!!. Cha kushangaza wanaogundua uhuni huu ni gazeti - RAIA MWEMA!!!!!.. Je, usalama wetu na mali zetu uko wapi?... AAh sorry! tunajadili NAPE kuanzisha chama akiwa ndani ya CCM? Hivi katiba ya CCJ kaweka wapi vile? Kadi ya NAPE MOSES NNAUYE wa CCJ iko wapi vile?..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom