Kadhi's court: A voice from a Muslim woman

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
So far kwenye mjadala unaondelea wa kuanzishwa tena Mahakama ya Kadhi nadra sana kukuta michango ya wanawake hasa wale wa Kiislamu. Lakini kuanzishwa tena kwa Mahakama ya Kadhi itakuwa na impact kwa wanawake hasa wale wale Kiislamu. Hivyo basi, katika mijadala inayoendelea ni vibaya kusikia mawazo ya wanawake hawa kwenye mjadala wa kuazishwa tena kwa Mahakama ya Kadhi.

Mwandishi wa makala hii, Salma Maoulidi, ni mwanamke wa Kiislamu. Ametoa maoni yake kuhusiana na mjadala wa kuanzishwa tena kwa Mahakama ya Kadhi. Kama unaweza kumsoma, basi soma umjibu kihoja na siyo kuropoka. Kama huwezi au huna hoja sepea kwenye zile threads zako. Kuna umuhimu wa kuwa na proper debate kwenye hili suala kwa kuyashirikisha makundi yote.

Kama unaweza kusoma, Salma Maoulidi kajadili masuala kadhaa muhimu. Mojawapo ni jinsi Mahakama ya Kadhi inavyotumika kama "political strategy" kupata kura za Waislamu. Kwanza kabisa, mwaka 1991 au 1998 kama sijakosea, wabunge ambao siyo Waislamu kwenye Bunge la Tanzania walitengeneza mswada wa kuanzishwa tena kwa Mahakama ya Kadhi. Hata hivyo, mswada huo haukupitishwa kuwa sheria.

Mwaka 2005, Mwenyekiti wa TLP Augustine Mrema akaja motion ya kuanzishwa tena Mahakama ya Kadhi. Alifanya hivyo ili kupata kura kutoka kwa Waislamu katika uchaguzi wa mwaka 2005. Kuona hivyo, CCM wakaiteka hoja na kuiweka kwenye kampeni za uchaguzi wa mwaka 2005 kuwa wakishinda wataanzisha Mahakama ya Kadhi. Nia yao ilikuwa ni kupata kura za Waislamu.

Uchaguzi wa mwaka 2010 mambo yalikuwa hivyo hivyo. Wakati tukielekea kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 mambo yanaelekea kuwa vile vile. Maneno kibao, lakini matendo hakuna kisa kutafuta kura za Waislamu. Lakini kuanzishwa tena au kutoanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi lazima ijadiliwe na makundi yote kwa undani badala ya kuendelea kutumiwa na wanasiasa as a political strategy kupata kura za watu wa dini fulani. Narudia tena; kama huna hoja au huelewi lugha pita kimya kimya mpaka kule Celebrities Forums. Hapa tunajadili hoja, siyo watu.

================================================================================


Rights, the law and religion: Islamic courts in East Africa

By Salma Maoulidi

2009-12-23, Issue 463

http://pambazuka.org/en/category/features/61238


INTRODUCTION

After a lengthy process, Kenya's draft constitution is finally out for discussion. A contentious issue during the Kenyan constitutional review process has been the question of Kadhi's (Islamic) courts.[1] In anticipation to this development, Muslim leaders across Kenya met to discuss the question of the constitutional status of Kadhi courts in the Kenyan constitution. It is, however, not just in Kenya that the question of Kadhis court is being thrashed out. Increasingly, it is assuming a regional character.

In Tanzania too there has been a raging debate over the introduction of the Kadhi's courts in the legal and judicial system. Like in Kenya, the most vocal and visible opposition against Kadhi's courts assumes a religious character, with the church being at the forefront of those most hostile to its introduction. But the motion to reinstate Kadhi's Courts in Tanzania was first introduced by an opposition leader, the Honourable Lyatonga Mrema of the Tanzania Labour Party (TLP), undoubtedly as a political strategy to win Muslim support in the 2005 General Elections. The ruling party is said to have appropriated the motion, turning it into a campaign pledge to make the same a reality in exchange for the Muslim vote. Not surprisingly, as the 2010 elections loom, the issue is gaining renewed vigour.

Religious forces have kept the matter very much alive in various spaces, including pulpits, newspapers and blogs, intensifying the pressure on the government to concede on the issue. Using a variety of advocacy channels, some Islamic bodies institutions have embarked on a media advocacy strategy aimed at consolidating Muslim opinion over the introduction of the Kadhi's court. Dismissive remarks by the Prime Minister Mizengo Pinda during the 2009 budget session on the issue of the Kadhi elicited a harsh reaction from Muslim quarters. To appease the situation, the chief mufti, Sheikh Shaaban Simba, formed a committee to advise and negotiate with the government over the matter. In response, the prime minister also formed a committee to engage with the Muslim Council.

Concrete proposals to introduce Kadhi's courts failed to come up during the recently concluded parliamentary session in November. In the meantime, the government has directed the Law Reform Commission to collect views and make recommendations on the matter. Women's voices are noticeably absent from the discussions. From available reports, there is no female representation on this crucial body, advising on the most intimate aspect of family and social relationships.

This absence of women's interest in the ongoing discussion is not only a physical absence but also an absence of gender considerations in the overall content of the proposals in substance. Largely, the voices of women have been sidelined or muffled by political forces informing the debate. Yet, it is they who stand to loose the most from what is being proposed. Indeed, the overwhelming interest in Kadhi's courts does not seem to be a preoccupation of Muslim women, but of sections of the Muslim community who seek political advantage both from political parties and in the larger community. Otherwise, it consumes most those sections of the community who stand to benefit the most from the existence of Kadhi's courts.

WHY KADHI'S COURTS?

The jurisdiction of the Kadhi's court involves questions of Muslim law relating to personal status, marriage, divorce and inheritance of and between Muslims who in most cases are citizens of a free nation. Voices for the introduction of the Kadhis Court cite ready examples of countries who are already implementing the system e.g. Zanzibar, Kenya and Egypt among others. The majority of Muslims supporting the reinstatement of the courts do so because they believe it guarantees them a degree of autonomy over an aspect of their life in conformity with religious dictates. Few go on to actually analyse the workings of these courts. Moreover, few examine in detail the experiences of specific groups, like Muslim women or non-Muslim women, before such courts.

Legal anthropologists like Erin Stiles and Susan Hirsh give us a glimpse of the experiences of women in Islamic Courts in Zanzibar and Mombasa respectively, even though their work is limited to their particular research interest. Additional information can be obtained from legal aid bodies and the experiences of legal activists like myself, whose particular preoccupation is working on issues affecting Muslim women or women impacted by Islamic laws. Just as the government feels it is important to consult and listen to mostly male religious bodies, it should equally invest in the experiences of individuals and organisations who actually work on these issues, not just those who moralise about them.

IMPORTANT CONSIDERATIONS IN REINTRODUCING KADHIS COURTS

Without doubt reintroducing the Kadhi's Court raises the possibility of denying a section of the community their constitutional, legal and human rights in the most fundamental area of human relations – the family. Moreover, religious courts will create classes of women – Muslim and non-Muslim; married and non-married – which will further discriminate among classes of women. This reality struck home about 20 years ago when I had just graduated from law school and was approached by two widows, former partners of a Muslim man named Marijala, after they were unceremoniously denied the right to inherit; or share in jointly acquired matrimonial property after the man they had cohabited with in a relationship that is defined as matrimonial died.

One of the women, though Muslim, could not inherit because the late husband was found to have only performed cultural rites in respect of their relationship. The other widow was a Christian, who the courts decided could not inherit from a Muslim, even if such a union is recognised under the law of marriage. Much as we tried to argue their case, the court dismissed their claims in deference to the opinions of Muslims sheikhs. I remember thinking then how odd this reasoning was. Indeed, how could a man, though Muslim, but who voluntarily and happily chose to live with these women, the mothers of his children, on terms agreeable to him and them, be suddenly converted by his relatives and court to become an impeccable and observing Muslim in death so that he would disown his consorts?

This may not have been the wish of the deceased but countless women meet this fate because under existing laws and prevalent interpretations of personal laws – whether religious, cultural or legislative in origin – women do not have equal status before the law, in flagrant contravention of national constitutions. Accordingly, the wife and daughter rarely benefit on an equal basis with their male peers in any type of matrimonial or family property settlement.

This was brought home to me this Ramadhan when a friend's neighbour in Zanzibar died, leaving behind three daughters and no son, and a profitable hotel business. To our shock and horror their uncles began harassing the children and staff, claiming that the wealth – including the hotel business – belongs to them. Officials from the department in charge of inheritance issues confirmed that in the Shafi School, which is prevalent in East Africa, should a man be survived by daughters and no son, her paternal uncles undercut the daughters in inheritance shares, something that would not happen if they had a brother.

The uncles did not have any constructive plans for the business or the children. I tried to find out if the girls could settle with their uncle by paying them the share of the inheritance. I proposed that they could be paying an amount from the income of the business over a specific time since this would also guarantee their livelihood as well as that of staff working at the hotel. The officials were not interested in such settlements but rather saw it expedient to close the business and sell it, so as to pay each heir their inheritance share. This case has left me deeply troubled and stunned, and more so the premise of its rigid reasoning.

Certainly, on its face, the rules for distributing inheritance shares contravene the Zanzibar Constitution, which prohibits any discrimination on the basis of sex. Further, it restricts the application of the Shari'ah, if contrary to the constitution. In practice, however, government institutions go on to apply predetermined formulas for inheritance and other matters without due regards to the principles of equity and justice. In the above case, female children were discriminated against in inheritance entitlements, solely because they are women, while male children are favoured in the same because they are male. It is this open favouritism that prompted the uncles to be vindictive towards their deceased brother, who had no son to protect the women under his care! Of course, during his life-time, they could not dare approach him or his affairs.

Possibly, under traditional ‘fiqh' (jurisprudence), the rationale for awarding the uncles a hefty share in the absence of a male heir was to offer the girls the protection from want, a male guardian was required to afford them. But what happens if the uncles have no intention of taking care of their nieces? Or what if the nieces are in a better position financially, or are older and their uncles still young, and the nieces are in fact the ones taking care of their uncles? Or as happened in the Zanzibar case, what happens if the families are estranged, such that the girls have never had a relationship with their uncles during their father's lifetime and the circumstances of his death makes reconciliation impossible?

Death is but one instance where the status of women in precarious. Divorced women too suffer dispossession at the hands of their estranged husbands. In many cases, a husband can, through a pronouncement of talak, unilaterally end a relationship and many claim it as his prerogative. To date there is no effort to check this arbitrariness, as if women have no interest in the continued subsistence of the matrimonial relationship.

Efforts to address this injustice have stalled because it concerns women and their ability to acquire and control resources. Those who benefit from the arrangement cry ‘religious observance' at the slightest hint of reforms, effectively putting the practice beyond reproach. God, in the Qu'ran, warns believers against ascribing injustice to the Almighty (Qu'ran 2: 224). If this is so how we need to ask under what leagal and religious basis can we continue denying women equitable shares of wealth, benefits and property jointly acquired during marriage?

Perhaps a more fundamental question with regards to the application of Islamic Law remains the active denial of women's equal human status by the use of sacred text even though the Qu'ran is clear that man's humanity is equal to woman's humanity. It is not surprising that when reading translations to the Qu'ran, as well as its exegesis, the text is assumed to speak to men. Thus, men become the subject of the text and women the other. Accordingly, most authors, scholars and jurists explain the text with the male as the norm with all the prerogatives, and in so doing, a woman becomes but an object of the grand plan between God and Adam to the exclusion of Hawa (Eve) and other lower beings. It is, therefore, not a coincidence that the rights of women are viewed relative to those of men and not separate from men or on an equal basis with men.

UNPACKING DOMINANT DISCOURSES OVER THE SACRED

Conversely, the inevitability of Kadhi's courts is couched in sacred terms where they are an obligation under God's law, as they are the avenue through which the Shariah can be interpreted and applied. Generally, it has been hard to advocate for reforms of Islamic Law because of the perception that Shariah is divine and thus immutable. Numerous scholars in Islamic law criticise this position, arguing that it is hard to pinpoint what constitutes the body of law that is termed Islamic Law. Religious officials tended to describe Islamic Law in general terms and would include provisions from the Qu'ran, the Sunna, Ahadith, the Fiqh of different ‘madhhab' and local interpretations and practices of matters deemed religious.

This concern with preserving their heritage, avers Dr S. Parves Manzoor, has limited the ability of Muslims to envision a universal moral order consonant with the themes of ‘khalifa' (representatives) and ‘amana' (trust), with dire consequences to Muslims. Since the 10th century Muslim jurists have confined themselves to the study and elaboration of the work of early jurists, not in its reformation to reflect subsequent human and social developments. As a result, notes Asma Barlas, much of the religious knowledge Muslims regard as canonical today is the product of a method that is described as linear, atomistic, and hermeneutically flawed. However, because of how religious knowledge and authority came to be structured in Muslim societies historically, most Muslims continue to regard these interpretations and this methodology as Islamic and obligatory.

In addition, the dichotomy between secular and Islamic law gives particular challenges to Muslims with regards to upholding citizenship rights where all citizens are presumed equal before the law. Scholars like Professor Abdullahi an Naim speak to this dilemma where Muslims try to assert their religious identity and to coexist within a wider social reality. In this respect, the distinction made by the late Sudanese scholar, Mahmoud Taha is helpful. He describes Shariah as the law prescribed by God to regulate all aspects of public and private life, but distinguishes this from the law which came to be known as Shariah, which was created through the interpretation of jurists of the fundamental sources of Islam mainly the Qu'ran and Sunnah during the eighth and ninth century AD. He argues that historical Shariah law as known to Muslims today was based on texts of the second stage of revelation, which was responding to the emerging and evolving needs of the Medina community at a particular point in time.

Rapaport too challenges the dominant assumption and shows how the early Islamic state intervened, albeit indirectly, in social and economic transactions. Equipped with greater manoeuvrability, jurists were able to introduce reforms in family law, such as supporting marriage stipulations in the marriage contract or maintenance awards upon divorce. Hence, the development of Islamic legal codes, mainly fiqh, is more akin to current notions of upholding the rule of law, so as to avoid arbitrariness on the part of judicial officers and in no way meant to seal the possibilities of novel legal reasoning.

The religious establishment in Tanzania further argues that the Kadhi's courts are a historical legacy, having existed in Tanzania until 1965 before they were unilaterally abolished by the independence government. Thus, although not always vocalised, the search for religious and political legitimacy fuels the debate over the Kadhi. Therefore, calls for its reinstatement should be understood as a continuation of Muslim demands for restitution against perceived injustices they faced as a group under colonial and the independence governments, including the disbanding of key religious institutions and the persecution of key Muslim religious figures, especially during Nyerere's leadership. A key aspect of this incursion is the loss of legitimacy among Muslim institutions, which Kadhi's courts are somehow championed to restore.

BROADENING THE SCOPE OF THE ANALYSIS

But does in suffice to argue for a system solely on the basis of what it should be and not what it is or its established outcomes? Numerous scholars, jurists and activists advance core principles in Islam to advance outcomes that are more just, equal or equitable, compassionate and merciful. The concept of ‘maslaha', for example, has been explored by a number of Islamic thinkers at different times to address changes in the political and social environment. ‘Maslaha' refers to public good/interest, wellbeing and welfare. It serves as a vehicle for legal and social change in that it looks into the intent or purpose of the law (‘maqasid shariah'). There are different models of ‘maslaha' developed by jurists at different times, some building on previous models, while others break new ground. Reformist jurists who invoked ‘maslaha' presented Islamic law as a comprehensive legal system that is flexible and adaptable, not immutable.

In recent times, this concept has allowed the state to legislate rules to facilitate governance and to confer rights across groups. This concept was in operation in recent legislative changes in Muslim majority countries like Morocco, Turkey and Iran. In upholding the divine purpose much larger than mundane preoccupations, ‘maslaha' shifts between the concepts of benefit and harm (‘mafsada') to determine the outcome of actions or reforms. Two main approaches are discerned in achieving legal certainty – formal or substantive legal rationality where legal rationality depends on the application of strict legal procedural rules while substantive rationality is concerned with the ethical purpose of the law. Importantly, universally, the concept is used as a mobilising force to unify the ‘umma' and improve its status.

Social and gender justice are core principles under the Tanzanian Constitution. Indeed, the government is accountable for the well being of its citizen (Art 8 (b) and (c) of the Constitution). The Tanzanian constitution is committed to eradicate all forms of oppression, threats, discrimination, corruption, injustice and favouritism. The government is obligated to provide equal opportunity to all citizens, irrespective of sex, ethnicity, religion or status. Accordingly, all policy initiatives must ensure that individual dignity and rights are valued and respected; and human rights are promoted in line with the Declaration of Human Rights and similar national, regional and international commitments.

But the legal framework in Tanzania, as is the case in most African countries, is yet to recognise the full personhood of the woman, emphasising the need to advocate for an egalitarian legal system based on citizenship rights. Across the board – in official, religious or judicial quarters – women's rights are still very much confined to traditional notions about women's position and entitlements. The revolutionary reading of gender ushered in by the Convention on the elimination of all forms of discrimination against women; the Vienna declaration on human rights; and the African charter on people's and human rights on the rights of women are not yet a reality.

Patriarchal notions of male supremacy in the family is the basis of such disparities, the logic being that a woman will be taken care of by the men in her family. This outlook creates a perpetual class of dependants who are adults – sane, able and competent to administer their own affairs. Yet, it is a position that many want to uphold, arguing it constitutes a religious edict, not because of a sense of responsibility towards those ‘under their care', but because they benefit from the status-quo. Indeed, there are countless examples that indicate that in practice, few women enjoy the protections that are arguably implied in men having bigger shares of inheritance. If the opposite was the case, then cases of maintenance and neglect would not top the charts of public institutions concerned with people's welfare, religious or otherwise.

In Tanzania, as elsewhere, there exists a dominant discourse on Islam and women that leaves women, as well as sympathetic men, few avenues to demand for full citizenship rights even within religious paradigms that are progressive. Similarly, many women, human rights activists and interested observers have been silenced over matters involving the religious, for fear of offending religious sensibilities. Others feel they do not have the requisite arguments and expertise to challenge discrimination legalised on the basis of the religious or cultural. But is there no room in Islam to usher in change consonant with universal human rights ideals?

MAKING A CASE FOR REFORMING THE LEGAL AND RELIGIOUS FRAMEWORKS

As advocates for women's rights, human rights and social justice we cannot afford to be disinterested in these discussions. Our primary interest is to ensure that the legal framework in Tanzania finally recognise the integrity and individuality of women as human beings and award them the protections that are due to every citizen. Nowhere is this more pressing than in the realm of personal relations. Also, it is to broaden the debate on rights and to introduce more progressive human rights and religious opinions to offer an array of possibilities under which women's rights can be conceived at an individual level and within the family.

The intention is not to bash or discredit Islam as is the trend currently, but to encourage the development of a more progressive ‘fiqh'. In this regard, Mohammed Kamali posits that usul fiqh's failure to encourage ‘ijithad', demands that new and more pragmatic approaches should be explored. Influenced by Muhammad Rashid Rida, Kamali advocates for a methodology of harmonisation, which utilises the resources of ‘usul fiqh' and the guidelines they offer for contemporary ‘ijithad', whereby ideas of dignity of mankind (‘karama'), the right to live honourably, equality, justice and freedom of choice comprise basic rights of human being.

Certainly, religion does have special significance in the society but religious law does not operate in isolation. Social expectations of men and women today differ considerably from those of men and women over one thousand or one hundred years ago. Our context is of the 21st century, yet we justify applying ‘fiqh' rules conceived in the 7th and 8th century, forgetting that such rules applied in a particular cultural and social context! As Muslims, how can we interpret legal rules so that they are more relevant to the present situation and also evidence the divine intention of upholding justice for women and men?

Moreover, instead of applying legal rules mechanically, the challenge is how to reflect the situation pertaining and not a preset outcome. Surely, the concept of justice should not just be relegated to the hereafter, as is commonly invoked to appease or silence women who contest blatant gender disparities, but it should be relevant to the present and actualised via universal, civil, legal, moral and ethical norms. For that reason, neither the state nor the courts should adopt a blanket assumption for an automatic application of religious and cultural law over personal law matters, as if women and men have no choice over the matter in life or in death.

© Salma Maoulidi, November 2009

*Salma Maoulidi is a member of the Gender and Education Office of the International Council of Adult Education, member of Femnet a Pan African Women's Advocacy Network and member of Sahiba Sisters Foundation, a community of women's learners operating in 13 regions of Tanzania.


Sources: Rights, the law and religion: Islamic courts in East Africa

Mohamed Said FaizaFoxy, mahakama ya kadhi, Pasco, Manyerere Jackton, MTENGETI, PhD, Shardcole, BONGOLALA, ISO M.CodD, win8, Sangarara, laki si pesa, THE BIG SHOW, JokaKuu, Ritz, adolay, Mpangawangu, Kibona, Victoire, Bouncer, lusungo, Feedback, Chipukizi, Ulukolokwitanga, Mtamile, sifongo, Happy Feet, chambalo kafao, kerubi afunikaye, Adili, Barubaru, HNIC, Ibn Khalidoun, mwananchi wa pemba, Hiram Abiff, wabara, Punjab Singh, RockSpider, BAK, TUJITEGEMEE, Chakaza, uaminifukazi, Hiram Abiff, Nanren, Tyta, TECHMAN, Gavana, Ngalikivembu, incharge, manumbu1, wabara, iJamii, hassan mood, Abdul Mohammed, frema120, Mag3, Freeland, Kitaturu, okaoni, Sibonike, illuh, SMU, jogi, chamlungu, WildCard, KISHADA, Gullam
 
Last edited by a moderator:
Maoni ya mchangiaji mmoja kutoka uzi mwingine kuwa suala ni pana na linataka hoja za maana na wasomi wanaojua wanaishauri vipi serikari kuliko wapiga makelele wa JF.

"Politics is too serious a matter to be left to politicians"- Charles de Gaulle

Pongezi kwa serikari kama kweli hili swala la 'mahakama ya kadhi' limetolewa bungeni kwa sasa maana kama lingepita au kukataliwa sidhani kama kungekosekana minong'ono ya udini kwa pande mbili korofi husika kwa muda mrefu.

Mpaka sasa ukisoma hoja za watu wengi wanaopinga mahakama ya kadhi sidhani hata kama wanaielewa vizuri, sasa sijui unapinga vipi kitu usichokifahamu vizuri zaidi ya kuwa mtu uliekosa hekima na unamwongozo wa chuki. Isitoshe hizi sababu za kupingwa kwa namna ya kejeli ndio kinakowafanya waisalamu nao wadhani sauti yao inakandamizwa na lazima waipate hiyo mahakama ya kadhi all for the wrong reasons from both sides.

Tatizo letu kama jamii tuna very poor communication strategy utakuta wale wanaoitaka mahakama ya kadhi wanaona umuhimu wa kuwashawishi waumini wao tu kwenye majumba ya ibada, badala ya jamii nzima ambayo inabidi waigharamie hiyo indulgence.

Sasa ushaiwishi wa aina hiyo serikari ikipitisha mahakama ya kadhi na kuna watu wasio ielewa is bound to cause favouritism arguments ukizingatia na demands zingine ambazo kwakweli wahusika are not realistic in practice of what they want in harmony not just our constitution but international human rights.

Mbali na hayo kuna hoja ambazo ni muhimu na azijajadiliwa kabisa na waislamu wenyewe kwenye kushawishi kuhusu mahakama ya kadhi wala atuja sikia upande wa wataalamu kuhusu swala zima na longterm impact kwa taifa.

Mfano hata kama kweli waislamu wameweza washawishi waumuni wengine umuhimu wa mahakama ya kadhi kwao na somo likaeleweka linakuja swala la uendeshwaji wake. That's when the real debates begins maana its one thing to tolerate ones beliefs but tolerance also has its limitations na ukivuka hiyo mipaka mbele ni mgogoro.

Kwa hivyo mtu anaweza kuona umuhimu wa waislamu kuwa mahakama ya kadhi lakini je yupo tayari kuilipia pia na wangapi hawaoni tatizo kulipia uendeshwaji wake kwenye jamii? Sasa kama serikari ikisema italipa kwa sababu ina mamlaka aina maana yule ambae hakupenda hela yake isitumike ataacha kulalamika leo au kesho hilo swala litakuwa na maswali ya muda mrefu sana kwenye jamii. Kama waisalamu kutwa kulalama kuhusu MoU za dini zingine ilihali wao pia wanaweza fanya na wameshindwa au hawaoni umuhimu wake na hoja yao ya kutaka mahakama ya kadhi ina misingi ya malalamiko hayo kwa swala ambalo jipya, huko mbele tutakubali mangapi mapya kuwaridhisha wana makundi?

Maana kwa upande wa hoja za waislamu wengi ukisoma hoja zao ni wakati was serikari kuweza ku-balance, lakini sio pound-to-pund, no-ho bali wanataka jambo jipya kabisa tena lenye demand za kubadilisha katika kwa mantiki ya swala lao wao privately, huko mbele tutabadilisha mangapi kwenye kujaribu ku-balance maswala ya watu to accomodate their ways of lives na wengine wavumilie; even in a positive view serikari itaunda body ngapi za usimamizi?

Mwisho wa tolerance ni kujua hapa nikiachia nitavunja kile ambacho nasimamia mimi na wewe serikari tayari unakatiba ambayo aina dini, unajenga nchi kwa nadharia ya kuwa auna dini lakini umewaacha wananchi wachague wanachotaka kuamini bila ya kuidhalilisha dini ya mwengine, sasa ukishaanza kukubali dini kucheza na katiba yako huko mbele ujue ni fujo.

Kwa ufupi hili swala ni pana na linataka hoja za maana na wasomi wanaojua wanaishauri vipi serikari kuliko wapiga makelele wa JF, wale wanaotaka mahakama ya kadhi lazima wajenge hoja ambazo serikari aitaweza compromise namna zake kwa wengine na huko mbele serikari ijue itadhibidi vipi wengine bila kelele za upendeleo.

Vitu vingine bora tuachane navyo tu si kwa sababu fulani mbona anayo kwani formation zao za jamii sawa na sisi wengine hata wao kwao hawakai meza moja nchini kwao kisa udini, ukabila, ethnicity; sasa na sisi tupo hivi? Hili swala linataka kujadiliwa na muslims scholars (sio masheikh uchwara), wasomi wa mambo ya jamii na watungaji sheria (sizungumzii wabunge bali those with qualifications) hili solution ipatikane kwa compromise sahihi if it possible.
 
EMT, ninavyoelewa kwa ufinyu wangu wa akili na kulingana na hizi nukuu hapa chini inaonekana hukumu itakayotolewa na Mahakama ya Kadhi nchini Kenya si supreme. Je walalamikaji, pamoja na wote kuwa Waislaam, wanayo haki ya kukataa kesi yao kusikilizwa kwenye Mahakama ya Kadhi na hiari ya kuchagua mahakama ipi ishughulikie kesi yao? Je nitakuwa sahihi nikisema kuwa kama inatokea mlalamikaji moja hakuridhika na hukumu ya Mahakama ya Kadhi anaweza kukata rufaa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani?

  1. Kadhi's Courts in Kenya deal with Islamic matters. The court is composed of a Chief Kadhi and at least three other Kadhis or as may be prescribed by Parliament. Each kadhi's court is subordinate to the high Court.
  2. Kadhis' courts only determine cases related to personal status, marriage, divorce or inheritance for people who profess the Muslim religion and who voluntarily submit to the jurisdiction authority of the Kadhis' courts.
  3. For a kadhi's court to have jurisdiction over any person, parties to the dispute must profess the Islamic faith. A Kadhi is proficient in Islamic law.
 
EMT, ninavyoelewa kwa ufinyu wangu wa akili na kulingana na hizi nukuu hapa chini inaonekana hukumu itakayotolewa na Mahakama ya Kadhi nchini Kenya si supreme.

Ibara ya 162(1) ya katiba ya Kenya inasema kuwa "The superior courts are the Supreme Court, the Court of
Appeal, the High Court and the courts mentioned in clause (2).

Clause 2 inasema kuwa "Parliament shall establish courts with the status of the High Court to hear and determine disputes relating to- (a) employment and labour relations; and (b) the environment and the use and occupation of, and title to, land.

Kwa hiyo, utaona hapo Mahakama ya Kadhi is not one of the superior courts as superior courts are only the Supreme Court, Court of Appeal, and High Court.

Je nitakuwa sahihi nikisema kuwa kama inatokea mlalamikaji moja hakuridhika na hukumu ya Mahakama ya Kadhi anaweza kukata rufaa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani?

Ibara ya 169(1) ya Katiba ya Kenya inaitambua Mahakama ya Kadhi kama moja ya subordinate courts.

Ibara ya 165(6) inasema kuwa "The High Court has supervisory jurisdiction over the subordinate courts and over any person, body or authority exercising a judicial or quasi-judicial function, but not over a superior court."

Obviously, ataweza kukata rufaa Mahakama Kuu kwa sababu appeals against decisions made by subordinate courts zinaenda Mahakama Kuu. Any decision can be directly appealed to the High Court.

Mojawapo ni hukumu ya Mahakama Kuu (CIVIL APPEAL NO. 15 OF 2013) ambayo ni Appeal from the decision in Civil Case No. 148 of 2012 of the Kadhis Court at Mombasa.


Je walalamikaji, pamoja na wote kuwa Waislaam, wanayo haki ya kukataa kesi yao kusikilizwa kwenye Mahakama ya Kadhi na hiari ya kuchagua mahakama ipi ishughulikie kesi yao?

Ibara ya 169(2) inasema kuwa Parliament shall enact legislation conferring jurisdiction, functions and powers on the courts established under clause (1).

Kwa hiyo, Bunge la Kenya litakuwa limetunga sheria inayotoa jurisdiction, functions and powers za Mahakama ya Kadhi. Nadhani tayari walikuwa na Kadhis' Court Act 1967 ambayo imefavyiwa revision mwaka 2012.

Ibara ya 170(5) inasema kuwa "The jurisdiction of a Kadhis' court shall be limited to the determination of questions of Muslim law relating to personal status, marriage, divorce or inheritance in proceedings in which all the parties profess the Muslim religion and submit to the jurisdiction of the Kadhi's courts."

So, parties must consent kesi yao kwenda Mahakama ya Kadhi. Kama hakuna consent, itabidi kesi iende mahakama nyingine. Mfano, in Hamoud v Hamoud [2000] the parties submitted themselves to the jurisdiction of the Kadhi's court kuhusiana na madai yao ya nyumba na mwisho kusaini makubaliano ya kumaliza kesi.

Baadae mke akafungua kesi Mahakama Kuu asking the court to decide on the same issues again. The High Court refused to allow the wife to re-agitate the same issues. Kisheria tunasema the case was res judicata.

In short, all the parties must consent to the jurisdiction of the Kadhis' courts.
 
Ukiangalia kwa jicho la tatu na kusoma between lines hili suala la Mahakama ya Kadhi ni uthibitisho wa dalili za TAIFA linalodondoka. Ukijaribu kufuatilia historia ya nchi yetu tangu uhuru utagundua kabisa kwa hali tuliyofikia kama taifa ni mbaya sana.. Yaan kama ni Bus la abiria dereva wetu kalala usingizi wa pono,, Bus limeacha njia linaelekea kwenye maporomoko na kila abiria anajitahidi kuokoa maisha yake..

Mahakama ya Kadhi ilifutwa miaka michache baada ya Uhuru pamoja na Utawala wa Kichifu na kimila.. lakini ili tujipe ufahamu mpana kwa maslahi ya taifa letu ni lazima tujiulize maswali yafuatayo..

Moja, Ni nini malengo ya kufuta Mahakama ya Kadhi pamoja na tawala za kichifu katika utawala wa awamu ya kwanza?

Pili, Malengo yaliyokusudiwa yalitimia au hayakutimia katika kipindi hicho cha awamu ya kwanza?

Tatu, Je sababu zilizofuta hizi Mahakama na Tawala za kichifu hazina mashiko tena katika Tanzania ya sasa?

Nne, Ni kwanini Mahakama ya Kadhi tu na si tawala za kichifu?

Tano, Ni madhara yepi tutayapata kama taifa endapo Mahakama ya Kadhi ikikubaliwa au kukataliwa?

Ukitapata majibu ya maswali hayo utagundua tu ni dalili tosha ya a falling state..(Taifa linalodondoka).. Na moja ya matokeo ya tatizo hilo utaona tu iwe kwa mtu mmoja mmoja au kikundi cha watu (kama Panya road nk) wanaanza kujitafutia njia mbadala ziwe njema au ovu kujitatulia matatizo yao na kukidhi matarajio yao.!

Sitaki kuamini kwamba kwa muislam mmoja-mmoja hapa Tanzania kwake yeye Mahakama ya Kadhi ndiyo kipaumbele namba moja na sio elimu, maji, afya, makazi bora, barabara, ajira nk. Mfano afya,, wagonjwa wote iwe wakristo, waislam au wapagan wanalala chini pale Muhimbili na kama ni bahati yake akipata kitanda basi ni cha ku-share tena na mgonjwa mwingine ambaye wakati mwingine wala si wa dini yake.

Kwa hali ilivyo katika nchi yetu kwa sasa hakuna kundi linalopendelewa kwamba eti linapata huduma bora ya afya kuliko lingine... Hata hiyo hoja ya MoU inayotolewa na viongozi wa kiislam ingekuwa na mashiko endapo tu ingethibitika pale KCMC au Bugando waislam wanabaguliwa kupewa huduma kwa sababu ya iman yao.

Mimi nadhani wote kama taifa lazima tutafakari kwa mapana yake hii hoja ya Mahakama ya Kadhi.. Hili suala ni nyeti sana,, tukianza kulichokonoa huko mbele ni balaa. Mimi naamini kwa Tanzania bara hakuna mtu asiyekuwa na ndugu wa dini hizi mbili. Hata hao wanaopigia debe utashangaa wajomba au mashangazi ni waislam au wakristo.

Ni wakati mwafaka wa kila mtanzania kutafakari kwa nia njema kabisa jinsi ya kulinusuru taifa letu... Dereva tuliyemwamini atuendeshe na kutufikisha kule tunakotarajia kufika amelala usingizi wa pono kwa miaka 50.. Mabus mengine yametoka nyuma yametupita na yameshafika yalikotakiwa kufika,, hata yale yalyopata pancha na matatizo mengine pia nayo yameshatupita.. Tatizo la safari yetu kupata misukosuko si ubovu wa Bus letu (Tanzania). Bus letu ni zima kabisa ila dereva tuliyemwamini atufikishe tunakotaka kufika ndiye mbovu.. ama haijui barabara vizuri au si dereva aliyefuzu au kalewa na ni mbabe hataki kuambiwa kwamba uendeshaji wake si mzuri. Matokeo yake kauchapa usingizi kwenye uskani na Bus ndo hivyo tena hali jojo.

Rai yangu ikifika Oktoba 2015 tuungane kwa pamoja tumwondoe huyu dereva. Bahati nzuri tangu mwaka 1992 tumezalisha madereva wengine wazuri. Tuchague dereva makini, mweledi na mwenye kutambua kwa dhati kabisa malengo yetu kama taifa ni kufika kule tunakotarajia kufika ambapo sisi kama wasafiri (Watanzania) tunatarajia kuwa na elimu, afya na miundombinu bora katika jamii iliyostaarabika..

Utakumbuka tuliaminiswa na kuimba "TAZAMA RAMANI UTAONA NCHI NZURI YENYE MITO NA MABONDE MENGI YA NAFAKA...." Huko ndiko lengo la Waasisi wetu tangu tunaianza safari mwaka 1961 na baadae 1964 tulitarajia tufike....

ONDOA CCM TANZANIA IPONE

 
EMT, ninavyoelewa kwa ufinyu wangu wa akili na kulingana na hizi nukuu hapa chini inaonekana hukumu itakayotolewa na Mahakama ya Kadhi nchini Kenya si supreme. Je walalamikaji, pamoja na wote kuwa Waislaam, wanayo haki ya kukataa kesi yao kusikilizwa kwenye Mahakama ya Kadhi na hiari ya kuchagua mahakama ipi ishughulikie kesi yao? Je nitakuwa sahihi nikisema kuwa kama inatokea mlalamikaji moja hakuridhika na hukumu ya Mahakama ya Kadhi anaweza kukata rufaa Mahakama Kuu au Mahakama ya Rufani?

  1. Kadhi's Courts in Kenya deal with Islamic matters. The court is composed of a Chief Kadhi and at least three other Kadhis or as may be prescribed by Parliament. Each kadhi's court is subordinate to the high Court.
  2. Kadhis' courts only determine cases related to personal status, marriage, divorce or inheritance for people who profess the Muslim religion and who voluntarily submit to the jurisdiction authority of the Kadhis' courts.
  3. For a kadhi's court to have jurisdiction over any person, parties to the dispute must profess the Islamic faith. A Kadhi is proficient in Islamic law.


Mkuu Mag 3 umeweka point nzuri sana. Maana nilikuwa najiuliza kama kutakuwa na mahamama ya kadhi ya mwanzo, ya hakimu mkazi, ya wilaya , mkoa, kanda , taifa, rufaa na privy council. Maana justice is justice si kila mtu anaeweza kukubali injustice za dini. Na vilevile suala la nani ni supreme kwenye jamii linatakiwa kuwekwa wazi, ni dini au dola.

Kuna wakati naona serikali inasumbuka kulalamika au kuongea kuhusu mahakama ya kadhi, kwanza sidhani kama waislamu wanahitaji kuiomba, inaweza kuendeshwa bila kuombwa, kwa mjumbe wa nyumba 10 all the way up. As long as haileti injustice kwa dada zetu.
 
Faiza bila shaka wsislam unaowazungumzia wewe hapa ni wale BAKWATA ambao wako kwa maslahi ya chama si ndio!!!??

Kama fursa yenyewe unayoiongelea ni ya muswada bungeni jamaa tayari wamenywea wameshauchomoa'
 
Waislam ni tiketi ya yeyote atakae Urais, Waislam wakikugomea huioni Ikulu. Kumbuka hilo.

Nawashauri Waislam watumie fursa tuliyonayo kuhakikisha tuyatakayo yanatimizwa.

Sasa wewe FaizaFoxy unajua wapagani na wakristo ni asilimia ngapi ya electorate? ina maana wakristo na wapagani wakikataa kumpigia mtu kura anaweza kuwa rais wa Tanzania? Au unadhani JK alipata kura za waislamu tu?

By the way, can you stand up and unequivocally say the main issue among Muslims in Tanzania is kadhi court? Wewe ni mwanamke ambaye unaonekana umesomasoma, are you an advocate of subjugation of Muslim women?
 
Waislam ni tiketi ya yeyote atakae Urais, Waislam wakikugomea huioni Ikulu. Kumbuka hilo.

Nawashauri Waislam watumie fursa tuliyonayo kuhakikisha tuyatakayo yanatimizwa.
Kamwe hili halitawezekana kwa maana waisilamu si wamoja, ukumbuke hapo kuna ishu ya BAKWATA amabayo imeanzishwa na serikali na inafadhiliwa kwa namna na moja na serikali na bado mnaipinga, kwa namna moja au nyingine hii mahakama ya kadhi itakuwa chini ya BAKWATA, je waisilamu wote mpo teyari kuwa chini ya BAKWATA?
 
EMT mada ni nzuri kama wachangiaji wataiangalia Mahakama ya Kadhi kwa kuangalia FAIDA zake na HASARA zake kwa jamii husika.Na mwisho wa siku wadau muhimu wa maamuzi haya na elimu itakayotolewa ni kwa WANAWAKE wenye imani ya KIISLAMU.Nina uhakika kuna baadhi ya WAISALAMU hasa wanawake hawajui hata namna Mahakama hii inavyifanya kazi zake.

Hivyo badala ya kuliangalia suala zima kwa mtazamo hasi basi tuliangalie kwa mtazamo chanya,na wanawake wenye Imani hii lazima wapewe elimu na uelewa ili na wao wapate kuridhia.

Pili sina sababu ya kuwakatalia waislamu Mahakama yao,ila nina uhakika wangeweza kuendelea nayo kwa kuweka vyumba au ofisi kwa ajili ya Mahakama hizi kufanya kazi na hii ingewaondolea kero yao ya muda mrefu ya mahakama hii.Lakini tujiulize waislamu wapo wamoja?Je,hakuna ambao hawaitaki?Je,Mahakama hii itaweza kuwahukumu wenye pesa zao?

Upande mwingine RUSHWA ni kidonda ndugu ndani ya JAMII yetu,Je,Mahakimu wao wakianza kupokea RUSHWA kwenye utoaji wa HAKI je,hatuoni mitafaruku ndani ya Jamii husika?

Ndiyo maana Jamii yenyewe ielimishwe juu ya hilo na hasa wanawake ndiyo wadau muhimu zaidi hapa.
 
Sijaona bado hasara ya kuwepo mahakama ya kadhi katika nchi hii,, kinachosumbua hapa ni lilelile tatizo la watanzania "UNAFIKI" hakuna namna serikali inashindwa kuandaa utaratibu hili suala likawezekana na hawa watu wakapata haki yao?? Kilichopo hapa sasa ni mashindano ya watu na chuki, na sio kutumia midahalo,majadiliano na researches ili kupata muafaka sahihi wa tatizo... Haya mabishano yasiyo na tija ndio yataleta machafuko ya kidini kwa kundi moja kuendelea kuamini halitendewi haki... KAMA KENYA,Na UK zipo kwanini hapa zishindwe??? What is CANON LAW & SHARIA LAW, nini tofauti ya hizi sheria na sheria tulizonazo??? majadiliano ya kikatiba, kisheria na busara vinahitajika hapa na si UNAFIKI,CHUKI NA UBINAFSI katika kutatua hili!!!
 
Kuna watu wajinga sana. Unaandika kwamba waislam wakikukataa huingii ikulu?
Tushajua tumlaumu nani sasa kwa kutuchagulia washenzi kama hao wapiga kura.
Unapiga kura kwasababu wewe mwislamu au mtanzania?
Udini unatoka wapi hapa? Ndio maana africa tuko nyuma maana tunafikiria kwa makalio na tuko so impetuous with motions involve imani. We dini unaijua au msindikizaji?
Hapa kuna waashabki wa dini amabo na wafananisha na wale washabiki wa waingereza ambao wako tayari kuua over soka.

Nyinyi sio waumini ni mashabiki wa dini ya kiislam.
 
EMT,

Kwanza ni vizuri ukajua yafuatayo
1. Uislam ni dini inayojitosheleza kwa kila jambo au tunasema complete surrender to the will of Allah.
2. Uislam unaongozwa na Maneno ya Allah ambayo ni Qur'an na matendo aliyofanya Rasul ambazo ni hadith.
3. Ukisoma mwongozo wa Allah utaona hakuna hata pahala pamoja waliposema kuwa MWANAMKE anaweza kuwa Kiongozi. Na ndio maana huwezi kuona mwanamke anaongoza katika swala au hata kuongoza msikiti.
4. Msemaji wa waislam ni laazima awe kiongozi.

Baada ya utangulizi huo.
napenda kukujulisha kuwa MATAKWA YA WAISLAM KATIKA KUANZISHWA KWA MAHAKAMA YA KADHWI HUKO TANZANIA NI KUTAKA MAAMUZI YATAKAYOKUWA YANATOLEWA NA MAHAKAMA HIZO YAKUBALIKE na kutambulika KISHARIA.

Na mahakama hizo zitafanya maamuzi yake katika mambo yafuatayo
1. Ndoa
2. talaka
3. Mirathi.

Na kama ulifuatilia taaarifa ya mahakama za huko tanzania katika wiki ya mahakama 1 - 3 Feb 2015 wamesema wazi kuwa kesi nyingi sana zilizopo na zinazojaza mahakama za mwanzo huko Tgk ni za migogoro ya ndoa, talaka, mirathi na migogoro ya ardhwi.

Sasa labda utudadavulie je una DATA zozote unazoweka tuwekea kuonyesha wanawake hawana migogoro hiyo ya ndoa zao, au kudai talaka au mirathi?

Mbona wenyewe katika mabaraza yao hawasemi mpaka wasemewe na watu wengine?

Katika Uislam hairuhusiwi kumuogopa mtu unatakiwa uhishimu na anestahikhi kuogopwa ni Allah tu. sasa ina maana wanawake hao wanamuogopa mwana'Adam na SIO Allah?

Kila mtu ana mtazamo wake na maoni yake. Usichukue hata siku moja mawazo ya mtu mmoja ukayafanya ya jamii nzima. Hilo ni kosa kubwa sana.

Poleee.
 
Sijaona bado hasara ya kuwepo mahakama ya kadhi katika nchi hii,, kinachosumbua hapa ni lilelile tatizo la watanzania "UNAFIKI" hakuna namna serikali inashindwa kuandaa utaratibu hili suala likawezekana na hawa watu wakapata haki yao?? Kilichopo hapa sasa ni mashindano ya watu na chuki, na sio kutumia midahalo,majadiliano na researches ili kupata muafaka sahihi wa tatizo... Haya mabishano yasiyo na tija ndio yataleta machafuko ya kidini kwa kundi moja kuendelea kuamini halitendewi haki... KAMA KENYA,Na UK zipo kwanini hapa zishindwe??? What is CANON LAW & SHARIA LAW, nini tofauti ya hizi sheria na sheria tulizonazo??? majadiliano ya kikatiba, kisheria na busara vinahitajika hapa na si UNAFIKI,CHUKI NA UBINAFSI katika kutatua hili!!!

Kwahiyo mnataka serikali iwaendesheeni dini yenu?hilo haliwezekani.
 
EMT mada ni nzuri kama wachangiaji wataiangalia Mahakama ya Kadhi kwa kuangalia FAIDA zake na HASARA zake kwa jamii husika.Na mwisho wa siku wadau muhimu wa maamuzi haya na elimu itakayotolewa ni kwa WANAWAKE wenye imani ya KIISLAMU.Nina uhakika kuna baadhi ya WAISALAMU hasa wanawake hawajui hata namna Mahakama hii inavyifanya kazi zake.

Hivyo badala ya kuliangalia suala zima kwa mtazamo hasi basi tuliangalie kwa mtazamo chanya,na wanawake wenye Imani hii lazima wapewe elimu na uelewa ili na wao wapate kuridhia.

Pili sina sababu ya kuwakatalia waislamu Mahakama yao,ila nina uhakika wangeweza kuendelea nayo kwa kuweka vyumba au ofisi kwa ajili ya Mahakama hizi kufanya kazi na hii ingewaondolea kero yao ya muda mrefu ya mahakama hii.Lakini tujiulize waislamu wapo wamoja?Je,hakuna ambao hawaitaki?Je,Mahakama hii itaweza kuwahukumu wenye pesa zao?

Upande mwingine RUSHWA ni kidonda ndugu ndani ya JAMII yetu,Je,Mahakimu wao wakianza kupokea RUSHWA kwenye utoaji wa HAKI je,hatuoni mitafaruku ndani ya Jamii husika?

Ndiyo maana Jamii yenyewe ielimishwe juu ya hilo na hasa wanawake ndiyo wadau muhimu zaidi hapa.

Tetty,

Unajuwa kuna udanganyifu mkubwa na upotoshaji mkubwa sana kuhusu mahakama hizo. mahakama hizo ni mahakama za khiari na kwa wale watakaopenda kuzitumia.

Na laazima ifahamike mahakama hizo zitaendeshwa kwa gharama za Waislam wenyewe na Sio Serikali.

Wanachotaka waislam NI KUWA MAAMUZI YATAKAYOKUWA YANATOLEWA NA MAHAKAMA HIZO YATAMBULIKE NA KUKUBALIKA KATIKA MFUMO WA SHARIA ZA JMTz tu.

Na mahakama hizo zitatolea maamuzi yake katika mambo matatu tu. NDOA, TALAKA NA MIRATHI.

Sasa tatizo lipo wapi kwa wakristo hapo au hata kwa waislam wasiopenda mambo yao hayo yahukumiwe katika mahakama hizo. wao mambo hayo watapeleka mahakamani za Serikali na watapewa maamuzi ya huko.

Binafsi sioni tatizo zaidi ya KUBANIANA NA HUSDA TU za wenyewe kwa wenyewe.

Mbona kwenye kuanzishwa kwa DESK maalum la ISLAMIC BANKING hamkupiga makelele? na kwa sasa ndizo zinazoongoza kuwa na wateja wengi na wakubwa katika mabenk yenu huko Tgk.

NI VIZURI MUKAHISHIMIANA NA KUTAKIANA KHEIR NA SIO KUVUMILIANA KAMA NCHI.

 
Katika maeneo ambao wanawake wa kiislamu hawaongei sana au kabisa ni hili la mahakama ya Kaadhi. Asante EMT kwa kuchimbua hii article.
FaizaFoxy mwenyewe ambaye namkubali kwa usomi wake amekuwa bubu kwenye mada hii toka kwa mmama muislamu na msomi mwenzake, matokeo yake anakuja na comment ya kujumla jumla..
Ningefurahi sana kusikia sauti za wamama wa kiislamu, lkn watasemea wapi?
 
Last edited by a moderator:
Nani kakwambia kuwa Serikali itaendesha au kugharamia mahakama za waaislam na Uislam?.
Au taarifa umezitoa wapi ?

Tafakur na soma kabla kuandika pumba zako.

Pole sana.

Wenzako wanadai serikali igharamie kama inavyogharamia mahakama za ardhi.

Hii ya kila mtu kuja na yake inaonesha ni jinsi gani hamjakaa pamoja na kukubaliana. Rudi Tanzania huenda ukawa wa msaada
 
Back
Top Bottom