Kada wa CCM wilayani Kinondoni ajivua gamba

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
[h=2][/h]JUMATANO, AGOSTI 15, 2012 06:08 NA AZIZA HASSAN, DAR ES SALAAM

MJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Godfrey Chikandamwali, amejivua gamba. Wakati wa kukabidhi barua yake katika Ofisi za Tawi la la CCM lililopo Sinza E, Kata ya Sinza, ulizuka mtafaruku baina ya Katibu wa tawi hilo, Muhidini Mavufa na Chikandamwali.

Katibu wa huyo alikuwa anashangaa ujio wa waandishi wa habari na kusema yeye si msemaji wa tawi.

“Sielewi barua hiyo ina nini na mimi si kwamba sitaki kupokea barua kwa kuwa barua ni kitu cha kawaida na unaweza kuleta muda wowote na God hajakosea kuleta barua hapa, ila alichokosea ni kuja na waandishi wa habari na mimi si msemaji.

“Pia God ni mwanachama wetu na sina taarifa kama kuna mgogoro wa aina yoyote katika tawi letu na wana CCM, lakini nashangaa kaniletea barua, waziache hapa nitazisoma kwa muda wangu nini kilichopo hapa ndani ya barua.

“Kwanza unajitoa kwa sababu ulikosa kura wakati uliomba uongozi, ungepata usingejitoa, umeishiwa ndio maana umeamua kujitoa CCM,” alisikika mwanachama mmoja aliyekuwamo katika ofisi hizo.

Kwa upande wake, Chikandamwali, alisema amefika katika ofisi hiyo ya tawi lengo likiwa ni kujitoa uwanachama ili aishi kwa amani.

“Nashangaa nafika hapa kukabidhi barua Katibu anataka akatae na kuniambia nipeleke Makao Makuu ya Kata, lakini Katiba ya CCM inasema ulipojiunga uanachama ndio utakapojitoa, kama mimi na mke wangu ulivyofanya,” alisema Chikandamwali.

Alisema amekuwa alihujumiwa katika uchaguzi wa mwaka 2009 alipogombea uenyekiti wa mtaa akashinda katika kura za maoni na baada ya hapo jina lake likakatwa na kupewa mtu aliyeshika nafasi ya pili.

“Niligombea na kupata kura za uenyekiti na udiwani mwaka 2010, lakini wana CCM wakanihujumu, wakanizushia kesi nikaambiwa mimi jambazi namiliki silaha, mara nimebaka pia nimekuwa nikifanyiwa hujuma katika biashara zangu,” alisema Chikandamwali.

 
CCM - Jumba la Majungu - lazima Uwe ndani ya CULT ukiwa Nje... Utafedheheshwa
 
Mimi nasema ni bora uwe mtanzania usie mwanachama wa chama chochote cha siasa kuliko kuwa mwanachama wa CCM. Ni kujitafutia kifo.
 
Huyo Chikandamwali hajui mambo ya kisasa. Siku hizi huna haja ya kuhangaika na waandishi wa habari.

Yeye angepeleka tu barua yake halafu aje hapa JF kuleta taarifa na nakala ya barua, mchezo umeisha.
 
Huyo Chikandamwali hajui mambo ya kisasa. Siku hizi huna haja ya kuhangaika na waandishi wa habari.

Yeye angepeleka tu barua yake halafu aje hapa JF kuleta taarifa na nakala ya barua, mchezo umeisha.

Founders wa JF ujumbe mpepata? Publicity ya JF inatakiwa iwe Juu, sasa tumesajiliwa rasmi na tunaeleweka na tuzo tumepata sasa kwa nini tena tusijitangaze? Michango yetu maka huu wekeni bajeti ya publicity tafadhali ili watu wafahamu ofisi zenu na kuleta masuala yao hasa wale wasiokuwa na uwezo wa kuingia net.
 
Du! Mwaka huu ule mtaji wao wa wanachama milioni 5 naona sasa lazima ubakie wanachama 200 tuu

We pimbi acha ushamba tangu vyama vya upinzani vimeanza wanachama wa CCM wanaoshindwa uchaguzi ndio mtaji wao. Mfano Slaa na mke wake aliye mtelekeza. Wala msiwe na presha baada ya chaguzi za jumuia mtaletewa makapi ya kutosha.
 
We pimbi acha ushamba tangu vyama vya upinzani vimeanza wanachama wa CCM wanaoshindwa uchaguzi ndio mtaji wao. Mfano Slaa na mke wake aliye mtelekeza. Wala msiwe na presha baada ya chaguzi za jumuia mtaletewa makapi ya kutosha.
Pimbi ni wewe ambaye unakaa na vizee vya ccm mpaka unanuka uzee ndio maana una mawazo ya kizee
 
hata wote mkijitoa akabaki nape peke yake bado ccm itaendelea kuwa chama chenye nguvu.

cdhani kama kama kweli akibaki m1 chama bado kitakua na nguvu, nadhani hujalifikiria vzuri hili!.uckumbatie maji kama jiwe kaka, kua flexible, penda mabadiliko, camon!!!
 
Jamani Chadema punguzeni speed ya kuchukua makada wetu, wengine ajira zetu zinategemea uwepo wa magamba na Nape akiwa mtendaji wetu mkuu.
 
Huyo Chikandamwali hajui mambo ya kisasa. Siku hizi huna haja ya kuhangaika na waandishi wa habari.

Yeye angepeleka tu barua yake halafu aje hapa JF kuleta taarifa na nakala ya barua, mchezo umeisha.

hahaa Chikandamwali bwana...namjua sana huyu jamaa..Mimi ni CHADEMA mwanzo kati Mwisho lakini huyu Chikandamwali ni mroho wa madaraka sana sana..by the way hivi ile bar yako ulofukuzwa kwa kushindwa kulipa pango imefikia wapi? kabla hujaingia kwenye mambo haya God jisafishe...kodi tu ya nyumba ume default hivi utaweza kuwa kiongozi wa watu wewe...source mimi mwenyewe maana nimepanga naye nyumba moja...Mbaya zaidi anaiba umeme tanesko na dawasco anakwiba maji
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom