Kada ataka Lowassa, Chenge watoswe CCM... Amtaja Karume kuchochea vurugu Zanzibar

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

.Amtaja Karume kuchochea vurugu Zanzibar

Na JOHN MALINGUMU

WAKATI malalamiko dhidi ya baadhi ya vigogo wa CCM kupandikiza wagombea wao na kutumia rushwa ili washinde uchaguzi ndani ya chama hicho kikongwe yakiwa yamepamba moto, kada mmoja wa chama hicho, Cyprian Musiba, ametaka watuhumiwa wa ufisadi akiwamo Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, kufukuzwa chama.

Akizungumza na KULIKONI wiki hii, Musiba ambaye alipitishwa jina lakekukuwania ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho (NEC), amesema watuhumiwa hao wanakizamisha chama.

Katika maelezo yake hayo, Musiba pia amekitaka chama hicgo kumoa onyo Makamu Mwenyekiti wa CCM na Rais (mstaafu) wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, kwa tuhuma za kuwa nyuma ya vurugu za Zanzibar.

Kada huyo ametaka Lowassa na baadhi ya wanachama wa chama hicho wakiwamo waliowahi kuwa wabunge kufukuzwa kwa sababu ya kuhusishwa na kuvuruga uchaguzi kwa kuchochea matumizi ya rushwa.

Akizungumza na Kulikoni, Musiba ambaye amejinasibu kufanya utafiti kuhusu watu hao anaotaka wafukuzwe na wengine kuonywa anasema; "Namuomba Mwenyekiti wa CCM-Taifa na Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete pamoja na vikao vya juu vya chama kwa maana ya Kamati ya Maadili na Usalama ya CCM, Kamati Kuu ya CCM na Halmashauri Kuu ya CCM, kuwanyang`anya kadi za uanachama Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, Andrew Chenge, Hussein Bashe, Beno Malisa, Martin Shigela, Nassor Moyo, Mansour Yusuf Himid, Mahamud Thabit Kombo, Vedasto Mathayo na Lameck Airo, kuwanyang'anya kadi za uanachama."

Katika hatua nyingine alitaka vikao hivyo vya juu vya CCM vitoe onyo kali kwa Rais (mstaafu) wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Amani Abeid Karume. Kwa mujibu wa Musiba, sababu za Karume kupewa onyo ni kudaiwa kuwa miongoni mwa wanachama na viongozi wanaoleta vurugu Zanzibar.

"Vijana na wanachama wengine wengi wanamuunga mkono Kikwete na kwa hiyo, akifanya maamuzi sahihi ya kufuta chaguzi hizi zilizolalamikiwa kwa rushwa pamoja na kuwanyang`anya kadi hawa wanachama wasio waadilifu atakuwa amefanya jambo kubwa sana na la msingi ambalo ni la kihistoria katika chama na taifa kwa ujumla.

"Hawa (wanaopaswa kufukuzwa) ndiyo chanzo cha matatizo yote ndani ya CCM na serikali. Wamekuwa wanashirikiana na wapinzani kuidhoofisha Serikali ya CCM pamoja na CCM yenyewe kwa maslahi yao, kwa sasa wameingia makubaliano na baadhi ya vyombo vya habari wakiwamo wamiliki kuhakikisha hawawaandiki wala kuwatangaza vibaya, isipokuwa watangazwe vizuri tu kuelekea uchaguzi wa 2015 wakiwa wasafi, wamekuwa wanapita misikitini, makanisani, katika taasisi za umma na binafsi wakijisafisha na kutoa hela ambazo ni haramu.

Musiba alisema genge hilo la wanasiasa anaotaka wanyang'anywe kadi wamekuwa wakishirikiana na wafanyabiashara aliowaita haramu, wasiolipa kodi.

Katika hatua nyingine anafichua kile alichodai mpango wa siri wa kuzidi kumchafua Kikwete akisema; "Kumekuwa na mpango wa kumchafua Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete na familia yake kupitia mitandao ya kijamii kama facebook, twiter na u-tube.

"Kumekuwa na kundi la vijana wanaotumwa na baadhi ya wanaCCM mafisadi kwa kushirikiana na baadhi ya watu nje ya CCM kuitukana na kuidhalilisha CCM na serikali yake, lakini pia vijana hao hao wakifanya kazi ya kuwasafisha mafisadi pamoja na wapinzani ambacho tayari wameingia makubaliano kutochafuana na mafisadi wa CCM, wakiwamo hata wafanyabiashara wakubwa na baadhi ya waaandishi wa habari kuhakikisha mafisadi wa CCM waliokuwa wanatajwatajwa kwa rushwa na ufisadi hawawasemi tena kwa ufisadi na rushwa bali wawasafishe tu kwa kila hali.

"Watanzania wenzangu na wanahabari nachukua muda huu kumuomba Mwenyekiti wa CCM Taifa kwa mamlaka yake kutengua baadhi ya matokeo ya CCM ambayo yamekuwa yanalalamikiwa karibu na kila mwanachama, mshabiki na mpenzi wa CCM lakini pia hata wananchi wa kawaida.

"Miongoni mwa maeneo ambayo ninaomba matokeo yatenguliwe ni pamoja na NEC Monduli kwa sababu kilichofanyika hakiendani na kanuni za CCM kwa mbunge kuomba kuchaguliwa pamoja na kwamba kanuni inakataa hata kama aliomba kibali kwa chama na mkoa, lakini habari zilizopo ni kwamba hakuwahi kuomba kibali katika ngazi ya CCM wilayani wala mkoani na katika kibali hicho hatukuwahi kusikia katibu wa CCM mkoa wa Arusha akizungumzia hilo.

Matokeo mengine ni ninayoomba yatenguliwe ni, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa pamoja na Makamu wake na zile nafasi zote za kuwakilisha vijana kwenda katika NEC, pamoja na Baraza Kuu la Vijana na nafasi nyingine zote zilizohusu umoja wa vijana kwa kuwa rushwa ilitawala kupitiliza, mbali na rushwa, viongozi walioshinda asilimia kubwa ya vijana wa nchi nzima inawapinga kutokana na uwezo wao kuwa mdogo kulinganisha na siasa za wakati huu ambazo zinahitaji sana uwezo wa kubuni na kufikiri na kupambana kwa kila hali.


"Namwomba mwenyekiti atengue matokeo ya Umoja wa Wanawake wa CCM kwa kuwa huko nako kulitawaliwa na rushwa kubwa ambayo haina kifani. Lakini pia tunamuomba mwenyekiti na vikao vya juu vya chama kutengua matokeo yote yaliyolalamikiwa katika ngazi ya kuomba ujumbe wa Mkutano Mkuu Taifa kutokea wilayani pamoja na ujumbe wa NEC kutokea wilayani.
 
Oh Wohaa HIVYO itakuwa VIZURI... Lakini Mwandishi Amesahau kuwa Mtukufu Rais Pia kateua KATIBU MKUU wa CCM Mwenye MIGUU MINGI kama OCTOPUS.. Mguu Mmoja Unavuta KATIBA ya CHAMA CHA MAPINDUZI; Mguu Mweingine Unavuta KATIBA ya CHAMA CHA MAFISADI; Kushoto anahusika na Wajanja KUZIVAMIA MBUGA zetu za WANYAMA na kupora NDOVU; HAPA na PALE ana USAFIRI wa MELI kuzipeleka kwenye SOKO HONG; Mguu Mwingine anapita MIKOANI kuimarisha CHAMA kwa...??? it is a SHAME!!!! Hakuna atakaye ULIZA swali hilo...

MTUKUFU RAISI kapandikiza familia yake zaidi ya WATU WANNE; Nani atauliza au KUTENGUA UAMUZI huo?

Mwandishi Anaonyesha JINSI pia alivyo BIAS....
 
Back
Top Bottom