Kabuye: Kuna nini Jimboni kwako mbona hawaitishi Uchaguzi ?

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Wana JF heshima zenu wakuu .

Leo baada ya kuona Ngeleja kaanza kutoa matamko ya kugawa Umeme Mbeya vijijini huku akijua kwamba kuna moto waja nimekumbuka juu ya Jimbo la Ndugu Pharacy Kabuye .Sijui nimepatia jina lake ama la lakini bado najiuliza kwa nini hadi leo NEC hawajaitisha uchaguzi ? Kuna shida gani na wanakwama wapi ? Maana najua hakuna rufaa iliyo katwa baada ya kutenguliwa .Je tunaweza kuona uchaguzi wa Mbeya vijijini haraka kuliko kule kwa Kabuye ? Naombeni mtizamo wenu wakuu .
 
This time wanataka kununua shahada zote kabla hajatangaza uchaguzi wa marudio maana tarime imekuwa fundisho.

Hivi vyama vya siasa haviwezi kuishitaki tume ya uchaguzi kwa kukiuka taratibu za uchaguzi?????? maana wananchi wa jimbo hilo wanakoseshwa haki yao ya kuwakilishwa na kusikilizwa maoni yao kupitia mbunge wao.
 
Nina imani si kazi ya Vyama kuitaka haki hii ila ni haki ya Watanzania wa Muleba kwenda Mahakamani na kufungua kesi ya kunyimwa haki .Shahada hawawezi kununua wakazimaliza .Mambo ya Tarime kama CCM yataka kuwajibu basi basi they must deliver na si kununua shahada .
 
Ni kweli vyama haviwezi kufanya hiyo kazi lakini nani atawaorganise hao watu???

Je kituo cha Demokrasia wamefanya nini kuhakikisha demokrasia ya watu wa Muleba imetimizwa??? Vyama vya vuguvugu (pressure groups) mko wapi????
Mwanasheria mkuu na other law enforcers mko wapi watu wanakosa haki yao ya msingi????
 
Bowbow umemtaja Mwanasheria did you mean Mwanyika ama ? Hakuna vyama vya vuguvugu Nchi hii wote ni watu wa maslahi binafsi .Ila vuguvugu la kwe ni toka kwa wananchi wa Muleba wenyewe wakiamua inakuwa hivyo kama ilivyokuwa Tarime .
 
Kabuye kakata rufaa kupinga maamuzi ya mahakama kuu sasa mnataka uchaguzi ufanyike kivipi?

Get organised before being carried away sons.....
 
Wakuu sinasikia kua kuna sheria inayozuia uchaguzi mdogo, mika miwili kabla ya uchaguzi mkuu, au?

Maana bada ya Tarime, niilmuuliza Mkulu mmoja wa CCM aliyekua huko Tarime, kwamba vipi Mwibara na Biharamulo, akaniambia kwamba ukifanyika sasa hivi CCM itakula hewa, lakini haiwezi kufanyika miaka miwili kabla ya general elections kwa hiyo haitkuwepo, Mkuu Lunyungu vipi imekaaje hii?
 
Nina imani si kazi ya Vyama kuitaka haki hii ila ni haki ya Watanzania wa Muleba kwenda Mahakamani na kufungua kesi ya kunyimwa haki .Shahada hawawezi kununua wakazimaliza .Mambo ya Tarime kama CCM yataka kuwajibu basi basi they must deliver na si kununua shahada .

Pheres Kabuye hakuwa mbunge wa Muleba. Alitoka jimbo la Biharamulo Magharibi (Biharamulo Mashariki ni kwa John Pombe Magufuli).
 
Wana JF heshima zenu wakuu .

Leo baada ya kuona Ngeleja kaanza kutoa matamko ya kugawa Umeme Mbeya vijijini huku akijua kwamba kuna moto waja nimekumbuka juu ya Jimbo la Ndugu Pharacy Kabuye .Sijui nimepatia jina lake ama la lakini bado najiuliza kwa nini hadi leo NEC hawajaitisha uchaguzi ? Kuna shida gani na wanakwama wapi ? Maana najua hakuna rufaa iliyo katwa baada ya kutenguliwa .Je tunaweza kuona uchaguzi wa Mbeya vijijini haraka kuliko kule kwa Kabuye ? Naombeni mtizamo wenu wakuu .

Sina hakika kama Kabuye alikata rufaa ila kama kuna mtu ana taarifa sahihi atupatie. Lakini nadhani kuna suala la kisheria hapa. Vingenevyo isingewezekana kuchelewesha uchaguzi mdogo kwa muda wote huo.
 
Kabuye kakata rufaa kupinga maamuzi ya mahakama kuu sasa mnataka uchaguzi ufanyike kivipi?

Get organised before being carried away sons.....

Asante Masatu kwa taarifa hiyo muhimu maana hata mimi nlikuwa sipati jibu. Vipi kuhusu Jimbo la Mwibara? Na kwenye aliyeshindwa mahakamani kakaa rufaa? Any clue?
 
Naomba kuuliza Kabuye ni yule mbunge aliyetoa mfano wa wabunge wengine wako kama kuku kulala hapohapo na wanakunya hapohapo?
 
Wakuu sinasikia kua kuna sheria inayozuia uchaguzi mdogo, mika miwili kabla ya uchaguzi mkuu, au?

Maana bada ya Tarime, niilmuuliza Mkulu mmoja wa CCM aliyekua huko Tarime, kwamba vipi Mwibara na Biharamulo, akaniambia kwamba ukifanyika sasa hivi CCM itakula hewa, lakini haiwezi kufanyika miaka miwili kabla ya general elections kwa hiyo haitkuwepo, Mkuu Lunyungu vipi imekaaje hii?

Mkuu FMES
CCM hii ina janja sana mkuu .They have been buying time na si zaidi ya hapo .Kabuye kwa taarifa nilizo nazo hajakata rufaa ni baada ya wananchi kusema aache kuhangaika ila wao watamfanyia maajabu ambayo itakuwa ni kuikataa CCM tena kwa mara nyingine.Narudia kwamba kwa habari za ndani na jimboni pale Kabuye ni mteule tu na wananchi wanangoja kipyenga watangaze yale yale ya Tarime and the same goes for Mwibara .Yaani kanda ya ziwa ni kazi kubwa kwa CCM kushinda na hasa baada ya kumpa Chenge dhamana kubwa ya uaminifu wakati wananchi wanajua ni mchafu .Kama huamini wacha wangoje utaona.
 
Back
Top Bottom