JWTZ yampiga mkwara Lowassa

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,734
405
Kwenye Gazeti la Dira ya Mtanzania la leo kuna taarifa kuwa makamanda wa JWTZ wamempiga mkwara mzito 'Kapteni' Lowassa kwa ile kauli yake ya wiki iliyopita kwamba JWTZ ipo tayari kuingia vitani na Malawi iliyoambatana na kutoa taarifa za utayari wa jeshi letu kwa vita hiyo. Kwa mujibu wa makamanda hao,mtu mwenye mamlaka ya kutoa kauli kama hiyo ni Rais pekee.
 
Kiherehere kwenye utu uzima kibaya sana!
Pasco wa JF unasemeaje aibu ya model wako wa 2015?...Si ataipiganisha nchi kwa sifa huyu tukimchekelea?
 
Kwenye Gazeti la Dira ya Mtanzania la leo kuna taarifa kuwa makamanda wa JWTZ wamempiga mkwara mzito 'Kapteni' Lowassa kwa ile kauli yake ya wiki iliyopita kwamba JWTZ ipo tayari kuingia vitani na Malawi iliyoambatana na kutoa taarifa za utayari wa jeshi letu kwa vita hiyo. Kwa mujibu wa makamanda hao,mtu mwenye mamlaka ya kutoa kauli kama hiyo ni Rais pekee.

Safi sana. I like this!
 
Kwan mmesahau kwamba nchi yetu kila mtu anaruhusiwa kutoa tamko,waraka,taarifa,??????sasa tanzania imekua nchi ya matamko na waraka,,,,,
subirini taarifa ya olympic anaweza akaisoma yeye kwa media maana imefanyika nje ya nchi
 
Kweli Malawi wanatisha kijeshi, maana hata vita haijaanza makamanda wetu wameshaanza kuogopa, sasa wameamua kumgeuka aliyewapa amri!!
 
Kimbelemble chake cha kutaka urais kinamfanya ashindwe kufikiri sawasawa.
Safi sana JWTZ.
 
Acheni hizo nyie wenye majungu yasiyo na mwanzo wala nyuma, Lowassa aliyasema hayo kama nani?
Its like you are doing INSANITY doing the same thing, in the same way expecting different results
 
Hivi kwa akili ya kawaida inawezekana hao makamanda wakatoa taarifa hiyo kwenye gazeti hilo????
Kweli sisi ni watanzania lakini hivi mnalijua jeshi letu vizuri au ndiyo kwa vile tupo jamvini basi kila kitu twende.
Jeshi letu siyo kama mnavyofikiria kwani ni highly disciplined and dedicated to protecting this country na mkitaka kuthibitisha ukweli huu [mungu apishe mbali] ngojeni muone kwenye mgogoro wowote ule unaotishia mipaka yetu and you will be surprised.
 
tungoje mvua ya MABOM toka Thailand hapo inatkiwa tenda ya kununua Mgwanda na RISASI hazitoshi TANZANIA _AKILI TUPU piganeni watu wapate ulaji

Huwa nikikumbuka mpango wa EL kuleta watalaam wa kutengeneza mvua, huwa nakosa imani kabisa na huyu baba
 
Jeshi letu limekuwa la kisiasa mno kiasi kwamba linashindwa kujitenga na kauli za kisiasa na wanasiasa. Sioni hata mantiki Jeshi kutoa hiyo kauli (kama kweli wametoa) kwani Jeshi kuingiza na kujiingiza kwenye siasa kunavifanya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kuwa dhaifu na kupoteza uzalendo.
 
Back
Top Bottom