JWTZ walalamikiwa kunyanyasa wananchi Ngara

TinyMonster

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
248
154
Askari wa jeshi la wananchi JWTZ wilayani Ngara wanadaiwa kuwanyanyasa wananchi wa wilaya hiyo. Inadaiwa wanajeshi hao wamekuwa wakiwanyanyasa wananchi hao kwa kigezo cha kuwaita wanyarwanda. Mwezi uliopita Waziri wa Mambo ya ndani Mh Shamsi Vuai Nahodha baada ya kutembelea wilaya hiyo na kujionea mgogoro uliokuwepo kati ya wakulima wa wilayani humo na wafugaji waliovamia vijiji vilivyo mpakani wakitokea nchini Rwanda na kusababisha vifo vya wakulima kadhaa liamuru jeshi la wananchi kufanya safisha safisha katika mapori ya wilaya hiyo ambako kunadaiwa wafugaji hao wamekimbilia, lakini matokeo yake wanajeshi hao wamekuwa wakienda vijijini na kuwakamata wananchi wasiokuwa na vitambulisho vya mpiga kura na kuwaita wakimbi na ili kuwaachia inabidi watoe kitu kidogo. Pia wamekuwa wakikamata ng’ombe wa wafugaji wa wilayani humo na kulazimisha wananchi hao kutoa shilingi 50,000 kwa kila ng’ombe na wanaposhindwa inadaiwa wanawashikilia na kuwauza.



Sasa wanajamvi ninachojiuliza, Hawa ndugu zetu waliopewa kazi ya kulinda mipaka yetu kama wanaanza kufanya madudu tuliyozoea kuyaona kwa jeshi la Polisi.. hivi tutakuwa wageni wa nani nchi hii?
 
wanafanya mazoezi, chadema si wamevaa kombati bwana? Mpaka kieleweke. Kazeni buti jw,. Nchi ni yenu
 
mjinga ni wewe usiejua wenye nguvu ni nani, eulikulia kijijini na kusomeshwa na pesa za bodi na kisha unatuhumu serikali iliyokupa fursa hiyo kwa mikopo hiyo, bad manners!
 
du.... Hujui hata unaloliongea :bange: limekuharibu huko nyuma hukuwa hivyo
 
Back
Top Bottom