Jussa aipongeza kamati ya maridhiano

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
Jussa+bwawani.jpg

Mh Ismail Jussa amewapongeza wanachi kwa kujitokeza kwao kwa wingi sana katika kongamano lilofanyika leo Bwawani. Pia ameipongeza kamati ya maridhiano kwa kitendo cha kuwakatisha tamaa wale wote wasioitakia mema Zanzibar.

Pia amemuomba MwenyeziMungu kumpa umri mrefu Mzee wetu Hassan Nassor Moyo mpaka siku Zanzibar itakapokuwa huru na kwenda kupachika bendera yake Umoja wa Mataifa na kuweza kutambulika kuwa ni nchi huru.

Amesema kuwa yeye binafsi hatachukua maamuzi yoyote yatakayokwenda kinyume na chama chake hapa amekusudia kuwavunja moyo wale wasiojua kwa nini amejiuzulu unaibu Katibu Mkuu jana ila lengo lake nikupata wasaa nzuri wa kuongeza nguvu katika wimbi la kuitetea Zanzibar ndani ya Baraza la Wawakilishi

Amesema ikiwa kuna makundi ya watu wenye nia ya kuvuvuruga maridhiano yaliopo basi watavurugikwa wao kwa uwezo wa MwenyeziMungu alisistiza kuwa kwa sasa tunataka Zanzibar yenye mamlaka kamili kitaifa na kimataifa na sio Muungano huu wenye kuleta faida kwa upande mmoja tu

Amesema tunapodai nchi yetu hatutangazi vita na Tanganyika wala isipokuwa ni kutaka kuirudisha Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ikifuatiwa na Muungano wa Mkataba tu ndio jambo pekee kwa sasa wanalolitaka Wazanzibari.

Aidha amesema iwapo tume ya kukusanya maoni itajaribu kuchakachua maoni ya wazanzibar dhidi ya nchi yao basi baraza la wawakilishi litasimamia kidete kuilinda na kuitetea zanzibar na kuyalinda maoni ya wanachi waliotowa.

Stori kwa hisani ya Hamed Mazrui via Face book
 
vunjilia mbali muungano mrudi kwenu na wabunge wenu ambao huku bara hata magari hawana wanaishia kukodi tax na suti za kaunda. SIRI YENU WAARABU WA CUF tunaijua.
 
Back
Top Bottom