Jumuiya ya Vijana CCM (UVCCM) iko wapi?, walahi marekebisho makubwa ni ya lazima

Deo Shy

Member
Oct 18, 2016
98
300
Mwezi wa December Jumuiya ya Vijana CCM (UVCCM) watakuwa katika mchakato wa kuchagua viongozi wa juu wa Taifa. Chonde chonde vijana hiyo ni nafasi nyingine adimu ya kuirudisha jumuiya katika uimara wake kama ilivyokuwa enzi za Sukwa Sukwa, Guninita ama Nchimbi.

UVCCM kwa sasa haina dira, viongozi wa juu wa jumuiya hiyo wapo wapo tu. Hata Rais wetu mpendwa alipokuwa Kigamboni kuongea na wanavyuo aliliona hili. Jumuiya ya sasa ni kama iko bubu. Jumuiya imeoza (samahani kutumia neno kali, ila ndio ukweli). rushwa iko nje nje, rushwa za ngono nje nje, kiuchumi jumuiya iko hoi ile mbaya, vichwa vya viongozi walio juu vimechoka, vinawaza anasa tu nk.

Sasa basi viongozi wa chama na wajumbe wote, ni ombi letu mtuletee vijana wenye vichwa vizuri. tunahitaji vijana wasomi, wenye uwezo mkubwa, wasio na makundi, na wenye nia ya kututoa hapa tulipo. Tunahitaji watu wenye maono ya kutuvusha hapa tulipo. Na watu wa namna hii wapo na watapatikana iwapo tu kama upendeleo hautakuwepo...

Sasa ebu fikiria ETI hawa ndio viongozi waliopendekezwa na vikao vya awali vya UVCCM chini ya Sadifa....... miongozi mwa 23

1. Mwakibinga: Sasa Mwakibinga ana uwezo gani jamani... ebu tuacheni mchezo tafadhali Sadifa. elimu yake kwanza mashaka... please jamani lets be serious

2. Ayoub Tesha: Duuh kuna mengine ya kucheka kweli.... Sasa Ayoub Tesha awe Mkt wa UVCCM Taifa kweli?. tUACHENI MCHEZO

3. Jackson Kangoye: Huyu naye ETI anapigiwa upatu na Sadifa kuwa Mkt wa UVCCM Taifa. Kangoye ni moja wa watu ambao ni weupe sana kichwani, hana uwezo hata kidogo wa kuiongoza UVCCM..... please jamani we need brain people over there. tuacheni utani

4. Kheri James: Ebu mwambie huyu jamaa aandike paper ya kuomba mkopo au msaada ADB kwa ajili ya kuwawezesha vijana nchini. hayo mambo ya kiuchumi ndio tunataka kwa hichi kipindi cha miaka 5. Kheri James ana vyeti vya kufoji mpaka sasa ana kesi ya kujibu.... na uwezo wake ni mdogo katika ngazi ya Taifa.... asifikiri kuongea Star Tv basi unaweza kuongoza uvccm. UVCCM ni taasisi yenye POA zake, hivyo lazima apatikane mtu mwenye uwezo kichwani

5. Abdul Van Mohamed. Huyu naye ETI anajiona anauwezo wa kuongoza Jumuiya... Duuuuh kweli Jumuiya imekuwa kokoro. Hana uwezo wa kuliongoza jumuiya, please wajumbe tusikubali kuligeuza jumuiya sehemu ya majaribio

Sote tumejifunza jinsi Sadifa alivyotuangusha. tunakiri tuliteleza kuchagua mtu BOGUS. Hivyo ni rai yetu tusirudie tena na tena kufanya dhambi kama hiI..... Na hawa ndio wagombea wa Sadifa na Shaka
 
Mbona unawachamba tu bila kutoa mapungufu yao au unaempendekeza anafaa tumjue
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom