Jumapili kama ya leo ilikuwa mwanzo na mwisho kwenda kanisani na sitatoa sadaka kamwe!

Mpwayungu Village

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
14,304
29,843
Ilikuwa ni asubuhi na mapema mama angu mzazi alienda Kwa jirani yetu kuomba simu ili anipigie. Nilipigiwa simu kwa namba ngeni na mimi kanuni yangu ni kuwa namba ngeni huwa sipokei lakini hii siku ilikuwa ya tofauti sana kwangu maana simu ilikuwa inapigwa non stop ni mwendo wa ringing almost masaa matatu, kama saa Tatu na nusu hivi nikasema ebu nipokee simu. Ilikuwa ni mama angu mzazi akiongea Kwa sauti ya chini yakutetemeka kama yupo kwenye barafu akasema jino limemsumbua tangu juzi hajalala hospitalini kijiji chetu cha mpwayungu haina huduma ya kutibu jino Kwa kung"oa walimshauri dawa ya jino kung'oa aende mjini akaling"oe

Baada ya kusikia hivyo mimi nikamwambia Nina haraka ya kwenda kanisani ngoja nikitoka maana simuelewi anataka nini (kumbe nilimwelewa kila kitu ila nilitia kiburi). Kanisa langu nilikuwa nasali Kwa mzee wa upako ubungo riverside, nilienda na kitu kama laki na nusu nakumbuka siku hiyo ilifanyika harambee kanisani ya kufanya changizo kumtolea mchungaji wetu Antony lusekelo ili aende marekani Kuna semina ya mambo ya dini wanaenda kupikwa vizuri. Nilijishtukia tu nimenyanyua mkono ni kapewa mic nikasema nitachangia laki moja. Umati wote ulipiga makofi na Ala za mziki juu

Muda wa sadaka nilitoa kama elfu ishirini nikarudia home Nina buku tano tu baada ya nauli na kunywa Chai magengeni nikawa na buku tatu tu mfukoni. Simu yangu nikiwa kanisani huwa naweka silence mode na siku hiyo tulichelewa kutoka tulitoka saa kumi kasoro Kuja kucheki simu yangu Ina missed call 47. Namba almost tatu tofauti tofauti nikaona ni vyema ni watafute ajabu ni kuwa kila namba nikipiga walisema alikuja mama ako kuomba kupiga saizi yupo nyumbani amesema atakuja jioni kukujalibu tena

MIMI nikajisemea ni kheri asipige maana hapa Sina pesa tena, jua likazama usiku wa saa mbili hivi nikapigiwa simu sikupokea, kesho yake tena sikupokea, siku iliyofuata ikawa kimyaaaa, Enzi hizo Kuna vikazi nilikuwa nafanya Kariakoo nipo busy kweli nikaona simu ya Anko wangu nilipopokea tu akaniambia kesho niwepo kijijini mpwayungu, kuuliza nini shida akasema niende Kuna tatizo kubwa sana. Kuja kucheki Kuna meseji za pole kama saba hivi kutoka kwa ndugu jama na marafiki wa nyumbani, kumbe ilikuwa ni msiba wa mama angu mzazi ,

Nilitokwa na hisia Kali sana huku mfukoni Sina nauli pesa yote nimetoa kanisani, nikasema yameshatokea Sina cha kupoteza Kuna jamaa angu huwa tunafanya kazi pamoja nikaomba aniazime kama elfu ishirini tu nirudi home Kuna msiba akasema hata yeye hana, kujaribu ndugu zangu hawana maana wote wapo Vijijini, yani ilifika hatua niliomba pesa mpaka barabarani nikaonekana kituko vinginevyo kesho sitaenda kumzika mama angu.

Last option Mishale ya saa mbili hivi usiku ikawa nikwamchungaji wangu baba wa kiroho Antony lusekelo, nilipiga simu yake Mara ya kwanza hakupokea nikapiga Mara ya pili akapotea msaidizi wake nikasema huyu huyu namwambia, niliambulia pole tu ila pesa alisema hana maana wana majukumu mengi ya safari ya kwenda marekani, nikajitambulisha mara ya mwisho ni mimi yule kijana niliechangia laki moja ya safari ya mchungaji akasema Asante nibarikiwe , duuh inamana wameshindwa kunikopesha hata elfu kumi tuu nikasema hapana Ngoja niende kwake.

Nilipofika kwake sikufanikiwa kumkuta, Ile nageuza tu nirudi nyumbani nikaona gari yake Prado nyeusi inanimurika taa Kwa mwanga Mkali sana. Nikasema Asante Yesu baada ya kufika getini Mungu yumwema niliona dreva wake kafungua Kioo akasema wewe Nani nikajitambulisha baada ya hapo nikasema Nina shida na mchungaji, nilibahatika kuongea na mchungaji ili anisaidie nauli akasema nimtafute kesho usiku huu ana mambo mengi halafu kachoka kweli kweli. Niliondoka mdomo umekauka sina hamu.

Saa saba usiku nikiwa kwenye mawazo makali sana nikaona simu inapigwa nyumbani wamekwama pesa ya jeneza imepelea kama elfu 40 nitume haraka kesho asubuhi linunuliwe.

INAENDELEA
 
Sasa wewe tajiri wa jf ulishindwa nini kuwapigia simu matajiri wenzako wa chamwino wakaenda kumchukua mama yako wakampeleka benjamin mkapa kumng'oa jino?

Huwa unatukana walimu, lakin ungekuwa ticha ungenkatia bima mama na wala asingekutafuta tena isipokuwa ungempigia wewe kila ukiona ujumbe toka nhif kuwa kadi xxx mama mpwayungu tajiri imetumika milembe mental hos xxx!

Tajiri jifunze kuwa na heshma, usiwadharau wenzako.

Halafu tiba ya kinywa na meno hela ndogo tu mapokezi 25k, kuchunguza, kusafisha, kupaka dawa nk ni kama 165,000 tu tena hospt ya kibingwa na rufaa za kanda!

Tajiri unakosaje laki 5 kumtibu mama yako?

Mungu akusamehe.
 
Ilikuwa ni asubuhi na mapema mama angu mzazi alienda Kwa jirani yetu kuomba simu ili anipigie. Nilipigiwa simu Kwa namba ngeni na mimi kanuni...
20230221_201037.jpg
 
Cha kukupa pole na kuomba Mungu awasaide ni umaskini wa home kwenu,.
Ukiona elf 40 inakosekana ujue ni poverty ya kiwango Cha lami,
Hatukuchek hapana Ila tunakuombea kwa Mungu umaskini uondoke sio tu upungue ,

Kwa Hili hatuwez kukulaumu, ila kwa swala la jino , sijui hupokei no mpya
Aaah apo mzee unazingua , hyo misimamo ya kijinga Sana
 
Sasa wewe tajiri wa jf ulishindwa nini kuwapigia simu matajiri wenzako wa chamwino wakaenda kumchukua mama yako wakampeleka benjamin mkapa kumng'oa jino?

Huwa unatukana walimu, lakin ungekuwa ticha ungenkatia bima mama na wala asingekutafuta tena isipokuwa ungempigia wewe kila ukiona ujumbe toka nhif kuwa kadi xxx mama mpwayungu tajiri imetumika milembe mental hos xxx!

Tajiri jifunze kuwa na heshma, usiwadharau wenzako.

Halafu tiba ya kinywa na meno hela ndogo tu mapokezi 25k, kuchunguza, kusafisha, kupaka dawa nk ni kama 165,000 tu tena hospt ya kibingwa na rufaa za kanda!

Tajiri unakosaje laki 5 kumtibu mama yako?

Mungu akusamehe.
Ni miaka kumi iliyopita maisha yangu yalikuwa mabovu sana sana, Mungu ashukuliwe saizi si kama jana
 
Wewe jamaa nikilaza wakutupwa. Yaani mzazi wako anakosa hata tecno ya 15000 anaomba omba kwa majirani. Wewe unaenda kupeleka pesa yote kanisani. Ungemtumia hata 5000 ungepungukiwa nini kwenye hiyo 100k
Kama nikweli unacho zungumza laana ya mama ako iendelew kukutafuna kila uendako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom