Juma Nkamia: JamiiForums inachafua na kuwagawa Watanzania

Status
Not open for further replies.
Mtandao ni nini? Jamii ni nini? Mtandao wa jamii ukoje na una sifa gani?

Huyu bado anaishi chini ya jiwe gani?

Yuko Kandhahar gani huko? Anakaa kijiwe na ma Pashtun gani?

Watu mpaka leo wanataka ku legislate freedom of speech on the internet bongo? Wameshindwa Communist Party of China na Vladimir Putin, mtaweza bongo?

Ishauri Ikulu iache kutumia email za yahoo ambazo hazina hata https encryption kwanza, na wizara zisituaibishe kwa kutumia IIS zenye matobo kuliko Swiss cheese.

Unaweza kusaidia kitu.

Freaking nincompoop who does not understand the inevitability of technology.
hahaha Kiranga umeua mkuu.nimeingia Urban Dictionary: nincompoop kucheck maana ya hilo neno nikaishia kucheka sana.sina shaka hata huyo mkaa mia akigundua maana yake atajicheka zaidi.
 
  • Thanks
Reactions: PSM
Anaijua technology ya Cloud Flare huyu mkuu......hahaha!



Mtandao ni nini? Jamii ni nini? Mtandao wa jamii ukoje na una sifa gani?

Huyu bado anaishi chini ya jiwe gani?

Yuko Kandhahar gani huko? Anakaa kijiwe na ma Pashtun gani?

Watu mpaka leo wanataka ku legislate freedom of speech on the internet bongo? Wameshindwa Communist Party of China na Vladimir Putin, mtaweza bongo?

Ishauri Ikulu iache kutumia email za yahoo ambazo hazina hata https encryption kwanza, na wizara zisituaibishe kwa kutumia IIS zenye matobo kuliko Swiss cheese.

Unaweza kusaidia kitu.

Freaking nincompoop who does not understand the inevitability of technology.
 
Yupo now TBC1

Kikubwa ataka UFUNGIWE NA SERIKALI

Cha kusikitisha sana Bwana Alhaj Juma Nkamia Kadai ni mtandao ambao hauna sifa ya kuitwa mtandao wa kijamii kwani unaandika uwongo na mambo ya kufikirika na utashi wa mtu

kwani mtandao wa kijamii ni nini maana yake, si watu wanaandika utashi wao?
 
hahaha Kiranga umeua mkuu.nimeingia Urban Dictionary: nincompoop kucheck maana ya hilo neno nikaishia kucheka sana.sina shaka hata huyo mkaa mia akigundua maana yake atajicheka zaidi.

Mpuuzi haelewi information age ni nini.

Wachina (uongozi wa kisiasa) na ujanja wao wote, wameweka bonge la firewall ku filter internet access.

Lakini kila siku watu wanapenya.

Hiyo serikali ya bongo ambayo nusu ya wafanyakazi wake wanahitaji msaada kuwasha computer ndo wataweza kufanya nini?
 
Mhe. Nkamia Kawakosea nini wana JF? si kila mtu ana uhuru wake wa kutoa maoni kwa mujibu wa Katiba? mbona mnakosa ustaarabu kama paka wa baa?:disapointed:
 
Jamii forum ingekuwa inasifia uozo unaofanyika serikalini na kuegemea upande wa chama tawala nafikiri angeisifia lkn kwa kuwa haiegemei huko aliko ndo maana anaichukia,huo ndo unafiki wa viongozi wetu,muda wote wanataka kusifiwa na si kukosolewa,inabidi tubadirike na kukubali mapungufu tuliyonayo na kuyarekebisha,hapo ndo tutakuwa na maendeleo ya kweli,kufungia mtandao hujafanya kitu hasa kwa ulimwengu huu wa technolojia watu wataibua kitu kingine na ndo kinaweza kuwa kibaya zaidi bora ya kilichokuwepo,mfano mzuri aangalie jinsi chama tawala kilivyochangia kuisambaratisha NCCR mageuzi enzi za Lyatonga Mrema na Matokeo yake Chadema ikaibuka,au mfano watu walivyokuwa wakitetea ufisadi hadi bungeni matokeo yake siri ilivyowekwa viwanja vya Mwembe Yanga aibu ikawafika,tubadilike jamani na kuepuka lugha za chuki na kuona vyote vinavyohoji madudu ya wakubwa ni vibaya,tutaishi kwa unafiki mpaka lini?
 
Asemayo ni kweli tupu kuhusu uchochezi, kama JF itaendelea hivi nitashangaa sana Serikali kuifungia Radio Imaan na Radio eema na kuiacha JF, kama hizo radio mbili zilikuwa zikichochea udini iweje zifungiwe JF iachiwe? sometimes mpaka roho inauma ukiona dini za wengine zinavokashifiwa humu, mpaka unajenga chuki na dini fulani kwa sababu tu ya comments za watu humu, kweli JF inatakiwa ijirekebishe la sivyo TUNAOMBA KWA KINYWA KIPANA SERIKALI IIFUNGIE ili nayo ijirekebishe !
 
Asante Juma Nkamia kwa kuitangaza JF, hii imewapa wananchi wengi kujua kuwa kuna mtandao wa jamii unaitwa Jamii Forums. Karibu watanzania wote hapa ndo ukombozi wa nchi hii unapoanzia
 
Hehehe mbwa naye kaamua kubweka leo!!!! Bahati mbaya hajui hata mwenye mbwa mfupa wa JF alikosa mbwa wa kumrushia ili ashughulike nao maana mbwa wake wote ni vibogoyo.
 
Huyu mimi siwezi kushangaa nikisikia kapata ubunge kwa kujipendekeza na anazidi kujipendekeza.

Tatizo mara nyingine mtu anaweza kujipendekeza kwa kufikiri wakubwa zake wanafurahi kusikia maneno kama haya kumbe hata hao wakubwa zake wanakuwa embarassed kusikia wabunge wao wana such a narrow-minded approach on freedom of speech.

Jamiiforums kama serikali ya bongo ingetaka kuifunga tungejua wakati ule wakuu kina Max walivyoshikwa na Warumi.

Ikulu yenyewe haikupenda uchafu ule, maana inajua siku wakigusa JF kesho yake radar za dunia nzima zitaelekea JF.

Mara tu Human Rights Watch wamewasha mtochi, mara dissident gani wa Motor City kaanzisha campaign kum shame Kikwete...

Nani anataka upuuzi huo?

Ndo maana Kikwete anasema waachieni watu wafurahie uhuru wa kujieleza.

Wanaweza hata kumtania Kingunge Ngombale Mwiru kwa utani mzuri.
 
Haha haaa, NKAMIA noma , lazima leo watu watatapika nyongo sana humu JF, ila kasema ukweli kabisa na matusi yanayoendelea kutokana na kauli yake hiyo ni dhahiri kuwa JF siyo mtandao wa kijamii bali mtandao wa chama.

Wewe umekuja kutafuta nini kama huoni mafao au faida ya Jamii Forums. Utaiponda vipi wakati wewe ni registered member au unaonyesha jinsi gani unafanya mambo bila kufikili. Tuonyeshe ni wapi unaulizwa chama chako unapojiunga na JF?
 
Yeye huwa anatafuta nini huku kwenye Mbwa, aache mbwa waongee kivyao yeye aendelee kuongea na mwenye mbwa!
 
Mbwa koko kamwe hawezi kuwa tishio kwa JF akatafute sehemu nyingine ya kubweka lakini siyo JF.
 
Huyu mheshimiwa anaweweseka na bado ataweweseka sana kwa sababu kuu zifuatazo:
1. kuwaita wenzake mbwa, kondoa kusini hawamuelewi na hawata muelewa
2. kukuosa unaibu-waziri michezo, hbr na utamaduni bado haamini.
3. elimu ya kuungaunga nalo ni tatizo. sasa yuko udom 1st year.
4. kufukuzwa simba sports club kama msemaji na pia kipigo cha juzi.
5. n.k
 
Mhe. Nkamia Kawakosea nini wana JF? si kila mtu ana uhuru wake wa kutoa maoni kwa mujibu wa Katiba? mbona mnakosa ustaarabu kama paka wa baa?:disapointed:

Sasa kama kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni, na yeye katoa maoni JF ifungiwe, na sie tunatoa maoni kwamba anaishi pangoni bado, wote tunatoa maoni na kutekeleza haki yetu ya kikatiba, tatizo liko wapi?

Paka wa baa ni huyo Nkamia anayejipendekeza kwa watawala arushiwe makombo ya wanachokula mezani mwao.

Ustaarabu ni kuheshimu uhuru wa kikatiba wa Watanzania kujieleza.

JF wanaitumia mpaka wakuu wake serikalini, tumeona Dr. Tibaijuka kaja kwa shamrashamra kubwa hapa.

Maafande washasema wanataka kuja kufanya uchunguzi JF, apparently JF ni source of intelligence bongo.

Sasa huyo Nkamia anataka kuwakosesha platform ya kuwasiliana na wananchi na kupata intelligence.

Anajua anachosema?
 
Mimi nashindwa kuelewa, yule waziri mwenye dhamana ya usalama wa ndani ya nchi wakati akitoa aidha hotuba wa bajeti yake au akichangia hoja bungeni aliwahi kuisifu JF bungeni huku akiwashauri baadhi ya wabunge wa upinzani wawe wanasoma mitandao ya jamii na JF ikiwemo. Sasa huyu so called mwandishi wa habari anafikiri bado tuko kwenye zile enzi ya ndiyo mzee.

Wakiifunga JF, servers bado zitaendelea ku-hold information na zitafunguliwa Websites zingine kwa kutumia the same servers. Mtu mwenye ubongo wa kuku only thinks kama hayo ya Nkamia (Nka-hundred)...sijui ana kamia nini!! Wasilete ile vita yao na Mwanahalisi hapa JF maana wanajeshi wa IT tuko wengi kuikabili hiyo vita. Wasijaribu kabisa, nasisitiza tena...WASIJARIBU KABISA.
 
Aibu kwa mwanahabari kuchochea kufungwa kwa chombo cha habari!

Akili haioni hata endapo chombo hakiendi sawa kuitwa kukanywa? kusahihishwa? kuandikiwa barua za onyo......lakini akili inakimbilia kubariki kufungwa kwa vyombo vya habari!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom