Aliyekuwa kada wa Chama Cha Wananchi CUF, Julius Mtatiro amedai chama chake cha zamani huenda kikapoteza mwelekeo zaidi endapo Mwenyekiti wake anayetambuliwa na Msajili, Profesa Ibrahim Lipumba atakabidhiwa mamlaka na mahakama.
Mtatiro ambaye alihudumu kwenye chama hicho kwa zaidi ya miaka 10 amesema kuwa endapo chama hicho kitaendelea kuwa mikononi mwa Lipumba kina hatihati ya kupoteza idadi kubwa ya wabunge wake na madiwani hasa upande wa Tanzania bara.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mtatiro ameandika, "kwa miaka takribani 20 Lipumba amekuwa Mwenyekiti wa CUF asiye na mafanikio kabisa, amekuwa mgombea urais kupitia CUF kwenye chaguzi za 1995, 2000, 2005 na 2010 na kila uchaguzi kura zake zikishuka kama ndege iangukavyo kutoka angani".
Aidha Mtatiro amesema kuwa Lipumba amekosa ushawishi miongoni mwa makundi muhimu na hakuwahi kuthubutu kujenga ushawishi kwa taasisi za kijamii, hata kama kusingelikuwa na mgogoro katika CUF.
"Ikiwa Lipumba atatangazwa kuwa Mwenyekiti halali wa CUF, CUF itakufa kuanzia hapo, itakufa kwa maana ya kubakia chama kama vile vyama vya kina Kiraracha na wengine, haitakuwa na mashiko Bara wala Zanzibar", ameongeza Mtatiro.