Juliana Shonza Akichangia Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Maji Katika Mwaka Mpya wa Fedha 2024-2025 Bungeni

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,033
974
"Nampongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Maji, Jumaa Aweso kwa kazi nzuri anayoifanya ya kumsaidia Mheshimiwa Rais katika ajenda yake ya kumtua Mama Ndoo kichwani. Moja ya sifa aliyojaliwa Aweso ni usikivu. Niliposimama mwaka 2023 kuchangia bajeti ya Maji, nilizungumzia umuhimu wa Wizara kuongeza bajeti ili waweze kukarabati miundombinu ya Maji ambayo imechakaa kama Mwenge, Ichenjezya yanayopatikana katika Mkoa wa Songwe ambayo ilikuwa ni mibovu" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

"Nimesimama kumshukuru Mhe. Aweso, umetuletea fedha Shilingi Bilioni 1.7 na sasa hivi mabomba yanatandazwa kule Mlowo, Vwawa wananchi wanapata Maji safi na salama"

"Tulimshauri Mhe. Aweso kuhusu Mita za malipo ya kabla, jambo hili lilikuwa ni muhimu sana, wananchi walikuwa wanateseka kwa kubambikiziwa bili za maji, leo Waziri ameanza kulifanyia kazi. Ameanza kwenye mikoa ya Tanga, Arusha na mikoa mingine. Nimevutiwa zaidi na namna ulivyotoa nafasi kwa Wataalam wetu wa ndani, umeondoa ile kasumba kuwa kila kitu lazima tuagize nje. Mita zimenunuliwa humu ndani zinazotengenezwa na Wataalam wa ndani. Niombe taasisi zingine ziige mfano kwasababu zitasaidia kukuza ujuzi wa ndani wa nchi yetu na kulinda thamani ya fedha yetu. Tunaomba muongeze kasi ya usambazaji ili mikoa ambayo bado ikiwepo Mkoa wa Songwe waweze kupata hizo mita za Malipo kabla kama maagizo ya Mheshimiwa Rais yalivyo"

"Nampongeza Rais Samia Suluhu Hassan, Wanawake wa Mkoa wa Songwe tunasema ndiye Balozi namba moja wa ajenda ya kumtua Mama Ndoo kichwani, tumeshuhudia Mapinduzi makubwa katika sekta ya Maji"

"Leo hii mikoa yote ya Tanzania imepata mitambo ya kuchimba visima vya maji. Katika Mkoa wa Songwe mtambo haukufika ukakaa tu, tumeshachimba visima 65 ndani ya Mkoa wa Songwe. Meneja wa RUWASA ameenda kwenye Wilaya tatu bado Wilaya moja ya Ileje ili wananchi waweze kuondokana na kero ya Maji"

"Rais Samia Suluhu Hassan kwenye bajeti ya 2024-2025 ametoa visima 900 kwenye majimbo yote 180. Hili ni jambo kubwa sana, Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais wetu kwasababu anatekeleza kwa vitendo ajenda yake ya kumtua mwanamke Ndoo kichwani"

"Wanawake wa Mkoa wa Songwe tuko pamoja naye Rais Samia Suluhu Hassan na tunamuunga mkono sana. Mwaka 2025 kura zote ni kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan"

"Tulikuwa na changamoto kwenye nchi yetu, fedha za miradi zinapelekwa lakini ukiangalia tija ya hizo fedha haionekani. Ndani ya Miaka michache ya Dkt. Samia Suluhu Hassan tumeshuhudia Mapinduzi makubwa ya usimamizi wa fedha za miradi na Benki ya Dunia (World Bank) wamekuwa ni mashahidi, wameonyesha namna gani Tanzania tuko vizuri kwenye kusimamia fedha za miradi"

"Naomba Mheshimiwa Waziri wa Maji, Aweso, sisi katika Mkoa wa Songwe, umesema kwa fedha za Benki ya Dunia, mikoa Imeongezeka Kutoka mikoa 17 hadi mikoa 25 na Mkoa wa Songwe upo ndani. Tunao mradi wa kutoa maji Tunduma kwenda kusambaza kwenye miji ya Mbozi, Tunduma, Vwawa na Mlowo, ni miji ambayo ina changamoto kubwa sana ya Maji"

Waziri wa Maji, Aweso Tunaomba utasaidie kwasababu Mkandarasi ameshapatikana Tunaomba fedha zije mradi uweze kutekelezwa na usainiwe ndani ya Mkoa wa Songwe kama ambavyo mmekuja kusaini mradi wa Mafumbo ndani ya Wilaya ya Mbozi"

"Hatuwezi kusahau kuwapongeza watu wa RUWASA, wanafanya kazi nzuri sana, Meneja wa RUWASA Mkoa wa Songwe anafanya kazi nzuri sana. Unapomkamua Ng'ombe Maziwa ukumbuke kumlisha. Mkoa wa Songwe hatuna gari la maji, tuna gari moja tu ambalo anatumia Meneja wa RUWASA, hilo hilo wanatumia Wahandisi wa Wilaya, linaenda SITES, anakuja nalo Dodoma, hivi yuko Dodoma maana yake kule Songwe hakuna gari. Aweso ni msikivu ila mwa hili uwe msikivu zaidi, utupatie gari, magari ya kutosha ndani ya Mkoa wa Songwe"

"Maslahi ya watumishi, watumishi wa RUWASA tangu wahamishwe kwenye Halmashauri Maslahi yao hayajaboreshwa, Taasisi zingine Maslahi yao yaliboreshwa lakini hawa wa RUWASA Maslahi yao ni duni. Mheshimiwa Waziri changamoto ni nini? Kama ni suala la kuthibitishwa Tunaomba wathibitishwe ili Maslahi yao yaweze kuboreshwa"

"Suala la Ofisi, nimeenda kumtembelea Meneja wa RUWASA, kwa kweli nimesikitika sana, amejibanza kwenye kachumba kamoja kwenye Ofisi ya Wilaya, hakuna Ofisi kabisa. Ukimuona hapa Dodoma amebaa Suti lakini hana Ofisi. Niombe, ujenge Ofisi ili RUWASA wafanye kazi kwenye mazingira mazuri, lakini kwenye Wilaya ya Momba na Wilaya ya Songwe hawana Ofisi naomba waweze kupatiwa Ofisi" - Mhe. Juliana Daniel Shonza, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Songwe

Juliana Shonza.jpg
 
Wabunge km hawa wa viti vya kupewa wanatakiwa wasiwepo bungeni, vwawa maji yanatoka yana matope anaisemea vwawa ipi?
 
Back
Top Bottom