Jukwaa la Katiba watoa Tamko zito dhidi ya Mauaji ya Mwangosi na Raia

Deus F Mallya

JF-Expert Member
Jul 28, 2011
705
440
TAMKO LA JUKWAA LA KATIBA TANZANIA DHIDI YA MAUAJI YA MWANDISHI DAUDI MWANGOSI
'‘Mauaji Ya Waandishi Na Wananchi YatavurugaMchakato Wa KupataKatiba Mpya Tanzania!''


JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tumepokea taarifa za kuuawa kinyama kwaMwandishi Daudi Mwangosi wa Channel 10na Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa Habari mkoani Iringa (IPC) kwa mshtukona masikitiko makubwa. Kama ilivyokwishaelezwa na wengi, kifo cha mwandishi huyu ni cha kwanza cha aina yake katika tasnia ya habari nchini na kinatishia si tu uhuru wa kutoa maoni na uhuru wa habari kwa ujumla wake, bali pia kifo hiki na vingine vya siku za karibuni vinauweka mchakato wa Katiba Mpya njia panda. Vitendo vya mauaji ya raia vinazidi kushamiri siku hadi siku. Wapo wananchiwanaouawa na watu wanaoitwa wenye hasira kali kwa tuhumaza uhalifu. Wapo raiawanaouliwa na majambazi na wahalifu wenginekwa sababu ya ulinzi duni katika maeneowanayoishi. Aidha, wapo pia wananchi wanaopoteza maisha yao kila siku kwa tuhuma za kwamba ni wachawi.Ukiacha hao, idadi kubwa ya watanzania wanaishi na ulemavu wa ngozi wamepotezamaisha kwa kukatwa viungo au kuuliwa kabisa kwa imani za kishirikina. Hali sasa imefikia kuwa mbaya hadi kuna watanzania wanajisikia salama zaidi wakiwa mwituni kuliko majumbani. Yote haya yanasikitisha sanakwa ujumla wake! Haki ya kuishi inayowekwa na kulindwa na ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeanzakuingia dosari katika Tanzania.Ukiacha mauaji yanayofanywa na watu wasiojulikana au miongoni mwa raia, yamekuwepo pia mauaji yanayozidi kuongezeka ya raia yanayofanywa na wawekezaji au matajiri nchini. Zipo kesi kadhaa za mauaji ya namna hii.
Hayo nayo yamekuwa yakitokea kwa sababu ya ulinzi mdogo ambao wananchi wanao kutoka kwa vyombo vya ulinzi na
usalama nchini. Jeshi la Polisi, ambalo ndio lenye dhamana ya kulinda watu na mali zaohaliwezi kukwepa lawama katika aina zote hizo za mauaji. Itakumbukwa pia kuwa ajali za magari, mabasi na meli zinagharimu sanamaisha ya watanzania katika siku za karibuni. Kwa kiasi fulani, hata kukithiri kwa ajali hizi nako kunahusishwa na mwenendo mbovu wa usimamizi wa vyombo vya usafiri unaofanywa na idara mbalimbali za serikali ikiwemo kikosi cha usalama barabarani. Roho zawatanzania zinazidi kupotea kutokana na udhaifu mkubwa unaosababishwa na rushwa na mambo mengine ya ukosefu wa maadili katika vyombo vya usimamizi wa haki. Mauaji ya raia yanayofanywa moja kwa moja naaskari wa Jeshi la Polisi nayo yanazidi kuongezeka sanakiasi cha kutishia amani na utulivu wa nchi yetu. Aidha, mauaji yanayohusishwa na siasa nayo yanazidi kuongezeka na kuzidisha chuki ya kisiasa ambayo ni mbaya sana kwa ustawi wa nchi yetu. Kwa mfano katika miezi ya Karibuni, kumekuwepo matumizi ya nguvu kuzidi kiasi kwa raia wanaokuwa wakipanga na kufanyamaandamano au mikusanyiko yenye lengo la kujadili au kupinga jambo fulani. Matokeo yake, kumetokea majeruhi na mauaji ambayo
yamesababishwa na vurugu ambazo zinatokana na Jeshi la Polisi kudhibiti vitendo halali vya wananchi. Kwasababu hiyo, JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tunatoa witoufuatao kwa Jeshi la Polisi na idara nyingine za serikali zenye dhamana ya kulinda usalama wa raia, malina mipaka ya Nchi yetu:

1.1. Jeshila Polisi liache kutumia nguvu kuzidi kiasi katika matukio yote ya kulinda mikutano na matukio ya hadhara. Tujuavyo sisi, Jeshi la Polisi linalotumia risasi za moto, mabomu ya kivita, maji ya kuwasha na gesi ya kutoa machozi dhidi ya raia ambao hawajabeba hata fimbo za kuchungia mifugo. Ni Jeshi lisilojiamini na linaloonesha woga wa ajabu. Kwa hadhira kama za Nyololo, Morogoro, Mbeya, Dar es Salaam na nyinginezo miezi yaKaribuni, Jeshi la Polisi lingeweza kuwatuliza wananchi kwa kutumia filimbi tu. Matumizi ya nguvu na kumwagia maji ya kuwasha hata wazee wastaafu wanaodai haki zao inaweza kuwa ndio laana inayopelekea Polisi kusikia furaha kuua kila mara. Ipo kanuni ya kimataifa inayowataka Polisi kutumia nguvu kidogo sana inayolingana tu na nguvu ya umma wanaokabiliana nao katika kutuliza ghasia.

2.Wakati huu wa mchakato wa kutengeneza Katiba mpya ya Tanzania na hata baada ya hapo, Jeshi la Polisi lijiepushe kuingilia shughuli za Kisiasa kwa kuziunga mkono au kuzivuruga. Mikusanyiko mingi ambayo imepelekea mauaji wakati polisi ikijaribu kuivunja ni matukio yaliyolenga kupata majibu ya kisiasa na siyo ya kipolisi. Wajibu wa Jeshi la Polisi
katika wakati kama huo ni kulinda na kuwezesha wananchi husika kueleza madaiyao kwa uhuru na bila kuvurugwa na kundi jingine lolote la watu wasiopendezwa na madai ya kundi husika. Tabia inayozidi kushamiri ya Jeshi la Polisi kutaka kujibu au kuzima hoja za Kisiasa au kiuchumi kwa mtutu wa bunduki, mabomu, maji ya kuwasha na virungu ni tabia ya Jeshi kutaka kuingilia kazi isiyo yake na ndio maana inawashinda. Aidha, kama Polisi wangekuwa niwataalam wa Siasa, wangegundua kuwa wanachokifanya ni kuahirisha matatizo na si kuyatatua!

3. Jeshi la Polisi na vyombo venye dhamana ya ulinzi vijitambue upya kuwa vina wajibu wa kulinda raia, mipaka na mali zao si vinginevyo. Mauaji yanayoendelea nchini ni uporaji wa haki ya kuishi na haki nyingine nyingi chini ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniana ile ya Zanzibar.Aidha, Jeshi la Polisi na serikali kwa ujumla wana wajibu wa kuhakikisha na kudumisha ustawi wa wananchi kwa mujibu wa ibara ya 8 (1) (b) nahawana mamlaka ya kuua raia. Ikumbukwe kuwa mamlaka yote kikatiba katika Tanzaniayako kwa wananchi na serikali pamoja na Jeshi lake la Polisi watapata madaraka na mamlaka hayo kutoka kwa Wananchi. Nani amewapa Polisi mamlaka ya kuua watanzania? Nani amewapa Jeshi la magereza mamlaka ya kuwapiga na kumwaga damu za Waandishi? Nani amewapa askari wanyamapori mamlaka ya kupiga risasi hovyo nakuua ng'ombe mbele ya wenye maliyao?

4.Athari za matukio ya mauaji na fujo zinazosababishwa na Jeshi la Polisi kutawanya waandamanaji au mikusanyiko mingine ni kubwa sana katika kuathiri vibaya hamasa ya wananchi kwenye Mchakato wa Katiba. Mpaka sasa, tayari watu wengi wameingia wasiwasi na wameamua kutoshiriki mikutano ya kutoa maoni ya Katiba inayoendeshwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba nchini. Endapo Jeshi la Polisi halitaacha kuua na kutishiaraia kwa kila wanachokifanya, mchakato wa Katiba utavurugika kabla Katiba mpya haijapatikana. Kwa mwenendo wa sasa, Jeshi la Polisi litakuja kupiga mabomu na kuua hata wananchi watakapokuwa katika Mabaraza ya Katiba wakijadili na kupinga baadhi ya vipengele vitakavyoingizwa katika rasimu ya Katiba. Pia, itafika wakati wananchi watataka kuandamana kwa amani kuunga mkono au kupinga mambo Fulani katikaKatiba. Kwa hali ilivyo, Jeshi la Polisi litaona hiyo ni fursa ya kutumia mabomu na risasi kuzuia wasiseme wanayotaka kusema. Hii ni hatari kubwa sana!

5. Mikusanyiko, maandamano na shughuli za mikutano ya Siasa ni matendo halali na haki ya kila mtanzania kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano, 1977 ibara ya 8, 20 na 21. Suala la kutoa taarifa kwaJeshi la Polisi kwa mujibu wa sheria ya Jeshi la Polisi ni suala la kuwajulisha tu kwa lengo la kuwaweka tayari endapo kutahitajika msaada wa Jeshi la Polisi wakati wa shughuli kamahiyo. Tabia iliyoota mizizi ya Polisi kujiona kama wamepewa taarifaili watoe au kukataa kibali ni uelewa finyu wa Katiba na sheria za Nchi. Ipo haja ya kuongeza uelewa wa wasimamizi wetu wa sheria ili wawe na uelewa mpana wa sheria na ibaraza Katiba wanazozisimamia badala ya kujiona kama wana wajibu wa Msajili wa vyama vya Siasa wa kuratibu shughuli za vyama. Mikutano, mikusanyiko, mihadhara, maandamano na mijadala ni haki ya Kikatiba ya Kila mtanzania binafsi na kwa makundi. Kwa kuwa haki ya kuishi iliyoporwa kwa MwandishiDaudi Mwangosi ndio haki kubwa kuliko zote, JUKWAA LA KATIBA TANZANIA tunataka jambo hili lisiishiekuunda Tume za uchunguzi pasipo kufanyia kazi mapendekezo yake. Aidha, kwa kuwa uchunguzi unaofanywa hauhusiani na kilichomuua ndugu Mwangosi wala kundi gani limemuua, tunapendekeza busara itumike kwa viongozi wa Jeshi la Polisi, kuanzia Kamanda wa Polisi Mkoawa Iringa kuachia ngazi ili kupisha uchunguzi huru wa Tume itakayoundwa na Mheshimiwa Rais ikihusisha na kuongozwa na mhimili wa Mahakama. Taarifa ya uchunguzi ipelekwe Bungeni na Mheshimiwa Rais kwa ajili ya kujadiliwa na ushauri wa kibunge. Kamati iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi tunaitamka rasmi kuwa batili kwa kutumia kanuni ya sheria za kiasili inayosema kuwa mtu au kundi hawezi kuwahakimu wa kesi inayomhusu mwenyewe. Bila kufanya hivyo, tunapata wasiwasi kama Tume ya namna hiyoinaweza kufanya kazi yake kwa uhuru. Kuachia ngazi kwa Kamanda wa Polisi mkoani Iringa kutakuwa ishara kuwa Jeshi la Polisi linahitaji kuwa makini zaidi katika kufanya kazi yake ya kulinda amani, mali na maisha ya watanzania. Kwa sasa, zipo hisia kuwa Jeshi la Polisi lipo juu ya sheria na Katiba, jamboambalo tunapenda kulikanusha vikali!

Mwisho, tunapenda kutoa rai kwa serikalikutangaza rasmi kuwa itachukua jukumu la kutunza, kusomesha, kulisha na kuhudumia familia aliyoiacha Daudi Mwangosi kuanzia sasa kwa muda wa miaka 20 watakapoweza kujitegemea wenyewe. Itakuwa ni fedheha kuiona familia aliyoianzisha Marehemu Mwangosi ikisambaratika kwa sababu kichwa cha nyumba hiyo kimesambaratishwa na bomu la Polisi ambalo kodi yake Mwangosiilichangia kulinunua. Kufikia hapa, tunapenda kutangaza rasmi kuwa msiba huu nimsiba wa KIKATIBA na tunaomba ufahamike hivyo kwa umma wote wa watanzania na kote duniani.

Mungu ailazeroho ya Marehemu Mwanahabari Daudi Mwangosi mahali pema peponi Amina!

Imetolewana kusainiwa kwa niaba ya JUKWAA LA KATIBA TANZANIA,
Deus MKibamba
Mwenyekiti
Alhamis, 06 Septemba 2012
 
Deus,hii serekali si ya kuendelea kutolea matamko ,huu ni muda muafaka wa kwenda mahakama za kimataifa kusaka haki kwani kabla ya uchaguzi mkuu tutashuhudia mauaji mengi sana,je mtaendelea kutoa matamko?
 
Ila wamechanganya sana habari. Inaonekana kama walikuwa wanaogopa kuishutumu moja kwa moja serikali. Swala la marehemu Mwangosi (RIP) ni tofauti kabisa na hivyo vifo vingine. Maana ameuwawa na chombo tulichokipa dhamana ya kusimamia usalama wetu akiwa anatekeleza majukumu yake halali.
 
Kuna tume mbili zimeundwa, tuwe na subra wandugu.

Wanasema siyo tume ni kamati, kisheri mwenye mamlaka ya kuunda tume ni raisi tu, hata bunge nao wanamalaka ya kuunda kamati ya bunge ambayo ina nguvu ya kisheria za kibunge. Lakini hii ya Mchimbi ni kama kamati za harusi tu inafanya kazi ya kunufaisha na kukidhi matakwa yake binafsi
 
Kweli najisikia raha na amani nikiwa mwituni kuliko kuwa kwa hawa mbwa wa mwema
 
Deus Kibamba na wanaharakati wa haki za binadamu fungueni mashtaka the Hague kusiana na maaji haya ya polisi kwani matamko hawa jamaa na waliowatuma wameshaweka pamba sikioni na kujifanya hawasikii kitu na hatishiki wala kuogopa matamko. Kukata kiburi chao peleka the Hague wakapate haki yao la sivyo mauaji ya wanyonge wasio na hatia yataendelea kufanya na hawa pilisi wetu kila leo kwa kisingizio cha siasa wakati majambazi yamejaa tele mitaani wanakula nayo vya wizi
 
Tatizo langu nikishamdharau mtu hata aongee nini huwa namuona bado ni mpumbavu tu, huyu Deus Kibamba mimi nilishamdharau siku nyingi sana sawa na Nape Nnauye. ni mganga njaa tu na Augustne Mrema wake.
 
Kuna tume mbili zimeundwa, tuwe na subra wandugu.

Tume zipi? nani mwenye mamlaka ya kisheria kuunda tume? Bado tuambiwe ni tume ngapi ambazo ziliwahi kuundwa na kutekelezwa mapendekezo yake? Hadithi za kusadikika za kuundwa tume watanzania hatutaki.. Tunataka usalama wetu!.. Haiwezekani tunaowalipa mishahara kwa kodi zetu wanatugeuka na kutuua.. Au mabomu yaliyonunuliwa kwa kodi zetu yatusambaratishe kikatuli... Hapa tume haina nafasi..
 
Deus,hii serekali si ya kuendelea kutolea matamko ,huu ni muda muafaka wa kwenda mahakama za kimataifa kusaka haki kwani kabla ya uchaguzi mkuu tutashuhudia mauaji mengi sana,je mtaendelea kutoa matamko?

Naandaa tamko langu.
 
Back
Top Bottom