Juhudi za watu katika kutafuta nafuu ya maisha

Jan 22, 2023
8
2
Kumekua na jitihada mbalimbali zikifanywa na watu katika kujiweka sawa kuendana na mifumo ya maisha kwa kufuata elimu za msingi, sekondari na za kati pia elimu ya juu na hata mafunzo ya ufundi hayo yote ili kupata sifa na vigezo vya kujiweka sawa kimaisha.

Lakini ukweli kwamba juhudi na jitihada zote zinazo fanywa na watu zinaishia kwenye mamlaka za kiserikali ambazo zimeundwa na wanasiasa ili kuhakikisha watu wanakosa nafasi na wanashindwa kutimiza ndoto zao kwa kigezo cha kwamba bodi ya mamlaka husika aija kuthibitisha kuingia kwenye mfumo.

Ili limewekwa kwa makusudi ili watu waendelee kuwa mafukara na masikini ili waweze kutawalika ndio maana sasa kila kada imekua na mamlaka za udhibiti ili kuleta vikwazo kwa watu.

Na kama zipo kwa ajili ya kuongeza ufanisi kwa nini wasiende kwenye hizo taasisi zinazotoa elimu na mafunzo wakathibitishe huko kabla aujapatiwa cheti cha kuhitimu au umahiri!!

Badala yake umemaliza na wakati wa kuomba kazi ndio wanakuja na bodi zao kukuletea mitihani na unalipa hera alafu waamue kukupa sifa ili ukapata kazi au kuku nyima kama mtu huyu alikua awezi na ajui chochote asingepatiwa cheti kule aliko soma mwanzo.

Ukweli kwamba mamlaka hizi na bodi zao zipo kwa ajili ya kukandamiza haki za watu kupitia taaluma zao na kuwatia umasikini ili waendelee kutawalika kupitia vikwazo na shida waliotengenezewa na udhibiti na watu wakate tamaa ya kufuata mifumo iliyo wekwa.
 
Back
Top Bottom