Joshua Loitu Kijana wa Kitanzania, hajulikani aliko tangu vita ya Israel na Hamas ianze

Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,221
1,788
"Ombi la Dharura kwa Joshua Loitu Mollel - Tafadhali Tusaidieni na Tuombe

Joshua Loitu Mollel, mwanafunzi mdogo kutoka Morogoro, Tanzania, aliianzisha safari yake kwenda Israel tarehe 18/9/2023, akiendeleza ndoto yake ya kujifunza Kilimo katika Shamba la Nachal Oz Holdings, Chuo cha IBIM. Alijiunga na jamii yenye shauku ya Nahal Oz, iliyopo karibu na mpaka wa Gaza, akiwa na matumaini ya kujifunza na kuchangia katika kilimo,kwa manufaa ya Taifa

Tangu tarehe 07/10/2023 Joshua hapatikani hewani wala kwa njia yoyote,jitihada za familia kupitia ubalozi kumtafuta hazijazaa matunda.

Familia na wapendwa wa Joshua wanahuzunika sana kwa kutoweka kwake na wanahofia usalama wake. Hatujui nini hasa kimempata Joshua hivo tunaomba kila mmoja wetu amuweke Joshua kwenye sala na dua na maombi


Ikiwa una habari yoyote kuhusu mahali au hali ya Joshua, tafadhali wasiliana nasi kwa simu.

+255768648844 Jina: Loitu Mollel Jina: Balozi Alex KALLUA Simu1: +972533037359 Simu2: +97253-303-7359


Tusimame pamoja, tukivuka mipaka, tamaduni, na imani, ili kuhakikisha kurudi salama kwa Joshua Loitu Mollel.

#Joshualoitu #MgogoroWaIsraelNaGaza #TuombeNaJoshua

IMG-20231022-WA0007.jpg
 
Magaidi Siyo Watu Ni Kama Wanyama Mimi Niko tayar Hata kwenda Huko kupambana Nayo..yalituletea ujinga kibiti tuliyafumua..Gaidi Gaidi tuuu.
 
Serikali yetu ya Tanzania ipo kimya haitoi muendelezo kuhusu mipango ya kuwasaidia raia waliopo Israel mbali ya 9 ambao wamerejea nchini , raia wa kiTanzania nje ya nchi ni kama mayatima balozi zetu hazitoi ushirikiano wala taarifa za wabaki au waondoke.

Government Facilitates Voluntary Relocation of Zambians from Israel​

By editor
Foreign Affairs Minister Stanley Kakubo on phone with his Chinese counterpart Qin Gang Foreign Affairs Minister Stanley Kakubo on phone with his Chinese counterpart Qin Gang

The government has successfully coordinated the voluntary temporary relocation of 77 Zambians from Israel, according to Foreign Affairs and International Cooperation Minister, Stanley Kakubo. This group of relocated individuals includes 72 students.

Minister Kakubo revealed these developments during a media briefing held in Lusaka. He also disclosed that there are currently 172 known Zambians in Israel, with 143 of them being students pursuing their studies.

Importantly, Minister Kakubo reassured the public that there have been no casualties among the Zambian community residing in Israel, emphasizing the government’s commitment to the safety and well-being of its citizens abroad.

In an effort to facilitate efficient and well-organized relocation, the Foreign Affairs and International Cooperation Ministry has invited relatives of Zambians residing in Israel to a meeting at the ministry’s headquarters. This consultation aims to address any concerns and provide support during the relocation process.
Source : Lusaka Times
 
SUA hawafundishi kilimo?
Huwa kuna programme inasimamiwa na SUGECO ambayo huwaunganisha wahitimu wa SUA na mashamba makubwa ya mboga mboga na matunda huko Israel. Hii yote ni kwa ajili ya experiencial learning !
 
Back
Top Bottom