Joseph Kabila sio mtoto wa Laurent Desiree Kabila (?)

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
JE UNAFAHAMU JINA HALISI LA JOSEPH KABILA ANAITWA "HYPOLITE KANAMBE KAZEMBEREMBE"? NA NI MTOTO WA KUFIKIA WA LAURENT DESIRE KABILA?.

Na.Comred Mbwana Allyamtu
Sunday -26/5/2019.
Kyala Marangu, Kilimanjaro -Tanzania

Kumekuwepo maswali mengi sana ndani ya Kongo DRC na nchi nyingi Afrika juu ya uhalisia wa Joseph Kabila Kabange (JKK) kuhusishwa na Unyarwanda (Rwandese), kumetolewa taarifa nyingi za siri zinazo mtaja JKK kuwa sio mtoto wa kuzaa wa Mzee Laurent Desiree Kabila, Rais wa tatu wa Kongo DRC na kiongozi wa zamani wa kundi la uasi la AFDL, aliye uondosha madarakani utawala wa vipindi virefu wa Mobutu Seseseko Kuku Ngwendu wa Zabanga kupitia ile iliyoitwa Operation Banyamrenge/Bahima.

Joseph Kabila mwenyewe na wafuasi wake wamekuwa wakikanusha hilo na kuhusisha taarifa hizo na njama chafu za kumchafua. Mwaka 2010 kwenye maadhimisho ya miaka kumi ya kifo cha Laurent Desire Kabila, Joseph Kabila mwenyewe alitoa maelezo kuhusiana na taarifa hizo zinazo muhusisha na unyarwanda. Pamoja na maelezo yaliyokanusha ya yeye kuhusishwa na taarifa hizo bado kumekuwepo taarifa na ushahidi mwingi unaoendelea kutolewa kuthibitisha kuwa Joseph Kabila ni Mnyarwanda na sio mtoto wa kuzaa wa Mzee Kabila.

Moja ya tafiti hizo zinazo zungumzia sintofahamu hii ya Joseph Kabila ni "Walaka" uliochapishwa na jarida la "Africa Federation" jarada hilo lilipewa jina la (titled) : CONCERNING THE TRUE IDENTITY OF MR. HYPPOLITE KANAMBE ALIAS “JOSEPH KABILA” ndani ya jarida lina mtaja Joseph Kabila kuwa sio mtoto wa kuzaliwa na Kabila mzee, walaka huu unaonesha kuwa mke wa Kabila mzee aliyeitwa Sifa Mahanga alikuwa na watoto sita (6) tu ambao alizaa na mzee Laurent-Desire Kabila. Kati ya watoto hao ambao Sifa Mahanga mke wa mzee Kabila alio zaa nao ni Josephine, Cecile, Masengo, Gloria, Kiki and Maguy. Katika listi hiyo Joseph kabila hayumo.

Je, huyu Joseph Kabila Kabangee (JKK) anaye tajwa kuwa sio mtoto wa kuzaa (biological child) wa Mzee Kabila ni nani? Kimsingi huyu Joseph Kabila aliyekuwa Rais wa nne wa taifa la Kongo DRC jina lake halisi anaitwa Hypolitte Christopher Kanambe na alizaliwa tarehe 04 June 1971 katika kijiji kidogo cha Hewabora, kilichopo katika Mji wa Fizi jimboni Kivu ya kusini (South Kivu Province in the Eastern Congo) huku baba yake akiitwa Christopher Kanambe Kazemberembe na mama yake akiitwa Marcellina Mukambukuje.

Baba yake alikuwa ni muasi kutoka kabila la Watuttsi aliyepinga utawala wa Juvenal Habyarimana raisi wa Rwanda kipindi hicho. Huyo Christopher Kanambe alikimbia Rwanda yeye na familia yake na kukimbilia nchini Kongo DRC mwaka 1960 baada ya machafuko ya kwanza ya kikabila nchini Rwanda yaliyo anza mwaka 1959, na katika harakati hizo za kutaka kuuondoa utawala wa Juvenal Habyarimana madarakani akafanikiwa kutana na Mzee Laurent Kabila mwaka 1964 aliyekuwa kwenye mapigano ya kumpinga Mobutu Seseseko huko mashariki ya Kongo DRC ,wakawa marafiki chanda na pete kwenye issue zao za kivita.

Baada ya kukutana na kuendelea na ushirikiano wao kwa makubaliano kwamba Mzee Kabila amsaidie Christopher Kanambe kumuondoa Juvenal Habyalimana madarakani kisha yeye atamsaidia Kabila kumuondosha Mobutu ikulu ya Kinshasa. Walikubaliana hayo kwakua utawala wa Mobutu ulikuwa umewekeza base yake kubwa Rwanda chini ya utawala wa Juvenal Habyalimana (Mtoto wake wa ubatizo) hivyo kufatia sababu hizo Rwanda ilikuwa kikwazo kikubwa kufanikisha mapambano dhidi ya utawala wa Mobutu.

Mwaka 1977 bwana Christopher Kanambe ambae ndie baba yake wa kumzaa Joseph Kabila alifariki dunia (duru za ndani zinataja Mzee kabila kuhusika, tutalitazama hili baadae) na kwa mujibu wa mila zao na taratibu za kijeshi ilibidi kabila amrithi mke wa Kanambe yani huyo mwanamama Marcellina pamoja na watoto wake wawili mapacha ambao ni Hypolitte na Jenny (wale wa karibu na escape 1 mnakumbuka utajiiri na matanuzi ya huyu dada).

Baada ya kuchukuliwa na Mzee Kabila wote rasmi wakaanza kuitwa kabila, yani huyo Hypolite na Jenny walibadili majina yao kwa Hypolite kuitwa Joseph kabila na huyo Jenny kuitwa Jennifer Kabila. Ila katika harakati za Mzee Kabila za mapambano yalipo mzidi alikimbilia Tanzania na familia yake ingawaje alikuwa na wanawake 13 na watoto 25 katika sehemu mbalimbali huko Kongo DRC.

Huyu Joseph Kabila (JKK) a.k.a Hypolite ni mpwa wa mkuu wa majeshi wa zamani wa Rwanda anae aitwaye James kabarebe na hadi mwaka 1996 huyu Hypolite alikuwa ni dereva wake kwenye vita ya Banyamulenge ya kumsaidia Mzee Kabila kumtoa Mobutu madarakani, hilo linathibitishwa na waziri wa mambo ya nje kipindi cha utawala wa Mzee Kabila aliyeitwa Bizima Karaha ambae alikuwa ni mnyarwanda, ambae mara kadhaa Karaha anasema anakumbuka kumuona Kabila akiwa dereva wa Kabarebe mwaka 94 na 95 alikuwa porini na jeshi la kagame la RPF ambalo lilikuwa likimsaidia Mzee Kabila katika vita vya msituni dhidi ya Mobutu.

Je ni Kwanini Joseph Kabila alipewa uraisi wa Kongo DRC kama hakuwa raia wa Kongo DRC? Katika kujibu swali hilo na kulielewa vizuri ni vyema turejee historia ya kifo cha baba yake Kabila aliyeitwa Christopher Kanambe ambae alikuwa ni mtusi wa Rwanda. plan hii ya kupewa uraisi Joseph Kabila ni plan iliyo injiniwa na Paul Kagame rais wa Rwanda ambae baada ya kuvulugana na Mzee Kabila kufatia kukwama kwa makubaliano ya kile kilichoitwa "Mkataba wa Lemela" ilikuwa ni mpango wa kumuondoa Laurent Kabila duniani na kumuweka mnyarwanda huyu Joseph (Hypolite) mkakati huu ulifanyika kwa umakini wa hali ya juu sana ambapo kijasusi mbinu hizi huitwa "TROJAN HORSE TECHNIC".

Sasa turejee kwenye habari ya kifo cha BABA YAKE HYPPOLITE........
Christopher Kanambe Kazemberembe na Mzee Laurent Kabila walikutana na kuanza ushirikiano wao mwaka 1964 kila mmoja akiwa anapambania nchi yake, Kanambe Vs Wahutu (Juvenal Habyarimana) na Kabila Vs Mobutu Seseseko, kufatia mapambano hayo mambo yakawa magumu mwaka 1966 kufatia jeshi la Mobutu kujibu mapigo kwa kusambalatisha uasi wote huko mashariki ya Kongo, kufatia hali hiyo Kanambe na Kabila wakakimbilia Tanzania chini ya mwamvuli wa P.R.P. (Parti de la Revolution du Peuple).

Baada ya vita ya Moba, Mobutu seseseko alituma watu kumuhonga hela nyingi Christopher Kanambe ambaye ni baba halisi wa Joseph Kabila ili amuue Laurent Kabila lakini mission ilibuma, baada ya mzee Laurent kabila kupenyezewa taarifa hizo, hivyo Kabila akaitisha kikao sehemu iitwayo Nyunzu huko mashariki ya Kongo DRC wanajeshi wake kadhaa wakapatikana na hatia akiwemo Christopher kanambe na wakahukumiwa kifo, lakini kabla ya hukumu ya Christopher Kanambe kutekelezwa aliuwawa na askali wake mwaka 1977 kisha huyo askali nae kuuwawa na walinzi wa Kanambe.

Baada ya kifo cha Kanambe Laurent Desiree Kabila akamuoa Marcelina mke wa Kanambe na kuwa adopt watoto wake mapacha Jenny na Hypolitte......... Ukweli ni kwamba huyu Hypolite (JKK) alizaliwa Kongo, na baba yake Christopher Kanambe alikuwa ukimbizini akifanya uasi dhidi ya serikali ya wahutu ya Habyarimana, na baada ya kifo chake zilitumika mila za kivu, kurithiwa na mzee Kabila.

Joseph Kabila, jina lake harisi anaitwa Hyppolite Kanambe Kazemberembe, baba yake wa kufikia Mzee Laurent Kabila alikua na wake zaidi ya 13 na watoto zaidi ya 25 na wengine hawajulikani kwani mzee Kabila hakua na muda wa kuwalea watoto hao kwani kipindi wanaishi Msasani Dar es salaam ambako Hyppolite Kanambe alilazimika kufanya kazi za ufundi, taxi dreva na barman katika Jiji la Dar es salaam na Kigoma kipindi hicho baba yake wa kufikia Laurent Desiree Kabila alikua ana ishi Tanzania huku anapigana vita na Mobutu Sese Seko huko Kongo DRC wakati huo ikiitwa Zaire.

Mwaka 1995, Hyppolite Kanambe aliamua kurudi kwao Rwanda ambako alipokelewa na mjomba wake James Kabarebe, ambae alikuwa ni mkuu wa intelijensia ya Rwandan Patriotic Army (APR), alimkaribisha Kanambe nyumabni kwake na kumtafutia kazi ya udereva wa ma lori na baadae akawa dereva wake katika jeshi.

Mwaka 1996, Marekani ilipoandaa shambulio dhidi ya Zaire, kupitia ili iliyoitwa "Operation Banyamrenge" chini ya Paul Kagame, Kagame alimchagua Kanal James Kabarebe kuwa kiongozi mkuu wa Operation hiyo na kuhakikisha Mobutu anapinduliwa. Katika kuajilia wanajeshi watakao husika na operation hiyo Banyamrenge Kabarebe aliamua kumweka mpwa wake Hyppolite Kanambe (Joseph Kabila) katika mazoezi ya kijeshi ili baadae ampatie nafasi jeshini, baada ya Hippolyte Kanambe kuhitimu mafunzo aliajiliwa kwenye jeshi la Rwanda kupitia mgongo wa James Kabarebe na alitumika katika jeshi la Rwanda kuanzia mwaka 1995 mpaka 1997, na alitumika pia kama mlinzi wa kagame kuanzia mwaka 1997 mpaka mwaka 1998 alipo rudi Kongo DRC nakuteuliwa kuwa Major General kwenye special Force iliyokuwa ikiendesha operation maalumu huko mashariki ya Kongo DRC.

Je Kuna uhusiano wowote wa Joseph Kabila kuhusika katika mauaji ya Laurent Desiree Kabila?... Je kuna lolote lile linalohusishwa na ulipaji kisasi cha baba yake marehemu Kanambe Kazemberembe? Au upi uhusiano baina ya "Operation Banyamrenge" na mkakati wa Bahama platform dhidi ya Joseph kabila na kifo cha Mzee Kabila?... Itaendelea sehemu ya pili.

Endelea kuwa na mimi katika sehemu ya Pili kupata majibu ya maswali hayo....upate kujua kuwa nchi ya Kongo DRC bado ipo contolled by remote from kigali maana Tshisekedi ni pambo tu.

Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
Wako Mjoli wa Historia na dipromasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copy rights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu

Email- mbwanaallyamtu990@gmail.com
IMG_20190526_203510.jpeg
FB_IMG_1558888437419.jpeg
FB_IMG_1558889195062.jpeg
IMG_20190526_203438.jpeg
FB_IMG_1558888556689.jpeg
FB_IMG_1558888346792.jpeg
 
Uzuri wa story hii ni nini?! Muandishi umewahi kuongea na muhusika?! Au umeandika hisia zako?! Habari hii ingeletwa na report za vinasaba kuthibitisha, ama mtoto kabila na baba , au na hao nduguze kuonyesha hawa shei baba, tafuta bioligical anthropologist wasaidie kuhalalisha ukweli wa simuluzi zako, otherwise naona ni story za kusubiria chai. Is too good to be true.
 
JE UNAFAHAMU JINA HALISI LA JOSEPH KABILA ANAITWA "HYPOLITE KANAMBE KAZEMBEREMBE"? NA NI MTOTO WA KUFIKIA WA LAURENT DESIRE KABILA?.

Na.Comred Mbwana Allyamtu
Sunday -26/5/2019.
Kyala Marangu, Kilimanjaro -Tanzania

Kumekuwepo maswali mengi sana ndani ya Kongo DRC na nchi nyingi Afrika juu ya uhalisia wa Joseph Kabila Kabange (JKK) kuhusishwa na Unyarwanda (Rwandese), kumetolewa taarifa nyingi za siri zinazo mtaja JKK kuwa sio mtoto wa kuzaa wa Mzee Laurent Desiree Kabila raisi wa tatu wa Kongo DRC na kiongozi wa zamani wa kundi la uasi la AFDL, aliye uondosha madarakani utawala wa vipindi virefu wa Mobutu Seseseko Kuku Ngwendu wa Zabanga kupitia ile iliyoitwa Operation Banyamrenge/Bahima.

Joseph Kabila mwenyewe na wafuasi wake wamekuwa wakikanusha hilo na kuhusisha taarifa hizo na njama chafu za kumchafua. Mwaka 2010 kwenye maadhimisho ya miaka kumi ya kifo cha Laurent Desire Kabila, Joseph Kabila mwenyewe alitoa maelezo kuhusiana na taarifa hizo zinazo muhusisha na unyarwanda. Pamoja na maelezo yaliyokanusha ya yeye kuhusishwa na taarifa hizo bado kumekuwepo taarifa na ushahidi mwingi unaoendelea kutolewa kuthibitisha kuwa Joseph Kabila ni Mnyarwanda na sio mtoto wa kuzaa wa Mzee Kabila.

Moja ya tafiti hizo zinazo zungumzia sintofahamu hii ya Joseph Kabila ni "Walaka" ulio chapishwa na jarida la "Africa Federation" jarada hilo lilipewa jina la (titled) : CONCERNING THE TRUE IDENTITY OF MR. HYPPOLITE KANAMBE ALIAS “JOSEPH KABILA” ndani ya jarida lina mtaja Joseph Kabila kuwa sio mtoto wa kuzaliwa na Kabila mzee, walaka huu unaonesha kuwa mke wa Kabila mzee aliyeitwa Sifa Mahanga alikuwa na watoto sita (6) tu ambao alizaa na mzee Laurent-Desire Kabila. Kati ya watoto hao ambao Sifa Mahanga mke wa mzee Kabila alio zaa nao ni Josephine, Cecile, Masengo, Gloria, Kiki and Maguy. Katika list hiyo Joseph kabila hayumo.

Je huyu Joseph Kabila Kabangee (JKK) anaye tajwa kuwa sio mtoto wa kuzaa (biological child) wa Mzee Kabila ni nani? Kimsingi huyu Joseph Kabila aliyekuwa rais wa nne wa taifa la Kongo DRC jina lake halisi anaitwa Hypolitte Christopher Kanambe na alizaliwa tarehe 04 June 1971 katika kijiji kidogo cha Hewabora, kilichopo katika mji wa Fizi jimboni Kivu ya kusini (South Kivu Province in the Eastern Congo) huku baba yake akiitwa Christopher Kanambe Kazemberembe na mama yake akiitwa Marcellina Mukambukuje.

Baba yake alikuwa ni muasi kutoka kabila la Watuttsi aliyepinga utawala wa Juvenal Habyarimana raisi wa Rwanda kipindi hicho. Huyo Christopher Kanambe alikimbia Rwanda yeye na familia yake na kukimbilia nchini Kongo DRC mwaka 1960 baada ya machafuko ya kwanza ya kikabila nchini Rwanda yaliyo anza mwaka 1959, na katika harakati hizo za kutaka kuuondoa utawala wa Juvenal Habyarimana madarakani akafanikiwa kutana na Mzee Laurent Kabila mwaka 1964 aliyekuwa kwenye mapigano ya kumpinga Mobutu Seseseko huko mashariki ya Kongo DRC ,wakawa marafiki chanda na pete kwenye issue zao za kivita.

Baada ya kukutana na kuendelea na ushirikiano wao kwa makubaliano kwamba Mzee Kabila amsaidie Christopher Kanambe kumuondoa Juvenal Habyalimana madarakani kisha yeye atamsaidia Kabila kumuondosha Mobutu ikulu ya Kinshasa. Walikubaliana hayo kwakua utawala wa Mobutu ulikuwa umewekeza base yake kubwa Rwanda chini ya utawala wa Juvenal Habyalimana (Mtoto wake wa ubatizo) hivyo kufatia sababu hizo Rwanda ilikuwa kikwazo kikubwa kufanikisha mapambano dhidi ya utawala wa Mobutu.

Mwaka 1977 bwana Christopher Kanambe ambae ndie baba yake wa kumzaa Joseph Kabila alifariki dunia (duru za ndani zinataja Mzee kabila kuhusika, tutalitazama hili baadae) na kwa mujibu wa mila zao na taratibu za kijeshi ilibidi kabila amrithi mke wa Kanambe yani huyo mwanamama Marcellina pamoja na watoto wake wawili mapacha ambao ni Hypolitte na Jenny (wale wa karibu na escape 1 mnakumbuka utajiiri na matanuzi ya huyu dada).

Baada ya kuchukuliwa na Mzee Kabila wote rasmi wakaanza kuitwa kabila, yani huyo Hypolite na Jenny walibadili majina yao kwa Hypolite kuitwa Joseph kabila na huyo Jenny kuitwa Jennifer Kabila. Ila katika harakati za Mzee Kabila za mapambano yalipo mzidi alikimbilia Tanzania na familia yake ingawaje alikuwa na wanawake 13 na watoto 25 katika sehemu mbalimbali huko Kongo DRC.

Huyu Joseph Kabila (JKK) a.k.a Hypolite ni mpwa wa mkuu wa majeshi wa zamani wa Rwanda anae aitwaye James kabarebe na hadi mwaka 1996 huyu Hypolite alikuwa ni dereva wake kwenye vita ya Banyamulenge ya kumsaidia Mzee Kabila kumtoa Mobutu madarakani, hilo linathibitishwa na waziri wa mambo ya nje kipindi cha utawala wa Mzee Kabila aliyeitwa Bizima Karaha ambae alikuwa ni mnyarwanda, ambae mara kadhaa Karaha anasema anakumbuka kumuona Kabila akiwa dereva wa Kabarebe mwaka 94 na 95 alikuwa porini na jeshi la kagame la RPF ambalo lilikuwa likimsaidia Mzee Kabila katika vita vya msituni dhidi ya Mobutu.

Je ni Kwanini Joseph Kabila alipewa uraisi wa Kongo DRC kama hakuwa raia wa Kongo DRC? Katika kujibu swali hilo na kulielewa vizuri ni vyema turejee historia ya kifo cha baba yake Kabila aliyeitwa Christopher Kanambe ambae alikuwa ni mtusi wa Rwanda. plan hii ya kupewa uraisi Joseph Kabila ni plan iliyo injiniwa na Paul Kagame rais wa Rwanda ambae baada ya kuvulugana na Mzee Kabila kufatia kukwama kwa makubaliano ya kile kilichoitwa "Mkataba wa Lemela" ilikuwa ni mpango wa kumuondoa Laurent Kabila duniani na kumuweka mnyarwanda huyu Joseph (Hypolite) mkakati huu ulifanyika kwa umakini wa hali ya juu sana ambapo kijasusi mbinu hizi huitwa "TROJAN HORSE TECHNIC".

Sasa turejee kwenye habari ya kifo cha BABA YAKE HYPPOLITE........
Christopher Kanambe Kazemberembe na Mzee Laurent Kabila walikutana na kuanza ushirikiano wao mwaka 1964 kila mmoja akiwa anapambania nchi yake, Kanambe Vs Wahutu (Juvenal Habyarimana) na Kabila Vs Mobutu Seseseko, kufatia mapambano hayo mambo yakawa magumu mwaka 1966 kufatia jeshi la Mobutu kujibu mapigo kwa kusambalatisha uasi wote huko mashariki ya Kongo, kufatia hali hiyo Kanambe na Kabila wakakimbilia Tanzania chini ya mwamvuli wa P.R.P. (Parti de la Revolution du Peuple).

Baada ya vita ya Moba, Mobutu seseseko alituma watu kumuhonga hela nyingi Christopher Kanambe ambaye ni baba halisi wa Joseph Kabila ili amuue Laurent Kabila lakini mission ilibuma, baada ya mzee Laurent kabila kupenyezewa taarifa hizo, hivyo Kabila akaitisha kikao sehemu iitwayo Nyunzu huko mashariki ya Kongo DRC wanajeshi wake kadhaa wakapatikana na hatia akiwemo Christopher kanambe na wakahukumiwa kifo, lakini kabla ya hukumu ya Christopher Kanambe kutekelezwa aliuwawa na askali wake mwaka 1977 kisha huyo askali nae kuuwawa na walinzi wa Kanambe.

Baada ya kifo cha Kanambe Laurent Desiree Kabila akamuoa Marcelina mke wa Kanambe na kuwa adopt watoto wake mapacha Jenny na Hypolitte......... Ukweli ni kwamba huyu Hypolite (JKK) alizaliwa Kongo, na baba yake Christopher Kanambe alikuwa ukimbizini akifanya uasi dhidi ya serikali ya wahutu ya Habyarimana, na baada ya kifo chake zilitumika mila za kivu, kurithiwa na mzee Kabila.

Joseph Kabila, jina lake harisi anaitwa Hyppolite Kanambe Kazemberembe, baba yake wa kufikia Mzee Laurent Kabila alikua na wake zaidi ya 13 na watoto zaidi ya 25 na wengine hawajulikani kwani mzee Kabila hakua na muda wa kuwalea watoto hao kwani kipindi wanaishi Msasani Dar es salaam ambako Hyppolite Kanambe alilazimika kufanya kazi za ufundi, taxi dreva na barman katika Jiji la Dar es salaam na Kigoma kipindi hicho baba yake wa kufikia Laurent Desiree Kabila alikua ana ishi Tanzania huku anapigana vita na Mobutu Sese Seko huko Kongo DRC wakati huo ikiitwa Zaire.

Mwaka 1995, Hyppolite Kanambe aliamua kurudi kwao Rwanda ambako alipokelewa na mjomba wake James Kabarebe, ambae alikuwa ni mkuu wa intelijensia ya Rwandan Patriotic Army (APR), alimkaribisha Kanambe nyumabni kwake na kumtafutia kazi ya udereva wa ma lori na baadae akawa dereva wake katika jeshi.

Mwaka 1996, Marekani ilipoandaa shambulio dhidi ya Zaire, kupitia ili iliyoitwa "Operation Banyamrenge" chini ya Paul Kagame, Kagame alimchagua Kanal James Kabarebe kuwa kiongozi mkuu wa Operation hiyo na kuhakikisha Mobutu anapinduliwa. Katika kuajilia wanajeshi watakao husika na operation hiyo Banyamrenge Kabarebe aliamua kumweka mpwa wake Hyppolite Kanambe (Joseph Kabila) katika mazoezi ya kijeshi ili baadae ampatie nafasi jeshini, baada ya Hippolyte Kanambe kuhitimu mafunzo aliajiliwa kwenye jeshi la Rwanda kupitia mgongo wa James Kabarebe na alitumika katika jeshi la Rwanda kuanzia mwaka 1995 mpaka 1997, na alitumika pia kama mlinzi wa kagame kuanzia mwaka 1997 mpaka mwaka 1998 alipo rudi Kongo DRC nakuteuliwa kuwa Major General kwenye special Force iliyokuwa ikiendesha operation maalumu huko mashariki ya Kongo DRC.

Je Kuna uhusiano wowote wa Joseph Kabila kuhusika katika mauaji ya Laurent Desiree Kabila?... Je kuna lolote lile linalohusishwa na ulipaji kisasi cha baba yake marehemu Kanambe Kazemberembe? Au upi uhusiano baina ya "Operation Banyamrenge" na mkakati wa Bahama platform dhidi ya Joseph kabila na kifo cha Mzee Kabila?... Itaendelea sehemu ya pili.

Endelea kuwa na mimi katika sehemu ya Pili kupata majibu ya maswali hayo....upate kujua kuwa nchi ya Kongo DRC bado ipo contolled by remote from kigali maana Tshisekedi ni pambo tu.

Ukinakili kazi zangu kumbuka kufanya acknowledgment.
Wako Mjoli wa Historia na dipromasia ya ulimwengu.

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu
Copy rights of this article reserved
written by Comred Mbwana Allyamtu

Email- mbwanaallyamtu990@gmail.comView attachment 1108730View attachment 1108732View attachment 1108734View attachment 1108735View attachment 1108736View attachment 1108737
Ni shahihii kabisa huyu jamaa sio mtoto wa kabila mzee
 
Uzuri wa story hii ni nini?! Muandishi umewahi kuongea na muhusika?! Au umeandika hisia zako?! Habari hii ingeletwa na report za vinasaba kuthibitisha, ama mtoto kabila na baba , au na hao nduguze kuonyesha hawa shei baba, tafuta bioligical anthropologist wasaidie kuhalalisha ukweli wa simuluzi zako, otherwise naona ni story za kusubiria chai. Is too good to be true.
hii stori ishawahi kuwekwa gazeti la Rai , Long time ago
Hahahaha, halafu muandishi anaona kaandika jambo jipya mwenyewe
 
Wee jamaa hizi chai unatunywesha bila sukari, huyo kabila kasoma Tanzania tena mbeya na wakina jay moe, alafu huo muda wakati yuko kaka mkuu shule ya mbeya wewe hapo umemweka alikua vitani anapigana vita vya mobutu, hahahahaha jamaa umetupa mpaka email kabisaa
 
Back
Top Bottom