Monitoring thread: John Pombe Magufuli katika Awamu ya Nne

Mhariri
HabariLeo; Tuesday,February 20, 2007 @00:01

STAILI ya utendaji ya John Pombe Magufuli, Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, ina mwelekeo wa kuifanya serikali ya awamu ya nne isieleweke kwa wananchi. Baadhi ya maamuzi ya mheshimiwa huyo yanakwenda kinyume na utaratibu wa kuheshimu sheria na wakati mwingine yanakejeli mfumo mzima wa utawala bora.

Katika hali isiyoeleweka, Magufuli inasemekana ameidhinisha utoaji wa hati ya kumiliki ardhi katika eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya akiba ya barabara huko Mikocheni Dar Es Salaam.
Wale wanaolifahamu eneo hilo watakubali kwamba kilichojengwa pale hakikustahili kuwapo.

Kwanza, kuna jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kulikofungwa vifaa vya kudhibiti na kufuatilia mwenendo wa masafa yote ya mawasiliano, kuanzia redio, televisheni na simu za mkononi na upepo ili kusiwe na muingiliano.

Eneo hilo lingehitajika kuwa na ulinzi wa hali ya juu na kutokuruhusiwa kwa aina yoyote ile shughuli za biashara, hasa biashara ambazo zinaendeshwa hadi usiku wa manane. Isitoshe, katika hali ya kejeli na dharau, wamiliki wa eneo ambalo Magufuli amelitolea hati wamediriki kujenga choo ambacho kimeegemea ukuta wa eneo la mitambo hiyo nyeti ya Taifa.Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni wameshalalamikia kuwapo kwa jengo kwenye eneo la barabara.

Manispaa imehoji uhalali wa hatua ya Waziri Magufuli kutoa hati ya kumiliki ardhi kwenye eneo la hifadhi ya barabara. Hivi ni nani anaielewa zaidi wilaya ya Kinondoni kama sio madiwani wake? Nini maana ya serikali za mitaa kama zinaingiliwa na mawaziri ambao hata hawahusiki na sekta hiyo?

Tunajiuliza: hivi si Magufuli huyu huyu aliyeongoza ubomoaji wa kituo cha mafuta kilichojengwa kwenye kile alichokiona kuwa ni hifadhi ya barabara kule Mwanza? Hivi si Magufuli huyu huyu, aliyesimama Bungeni na kumkosoa hadharani Naibu wake, ambaye kwa wadhifa wake wa ubunge ni diwani Kinondoni akimshutumu kuwa emehodhi viwanja? Madiwani wa Kinondoni na Watanzania kwa ujumla wana uhalali wa kutaka umiliki wa eneo hilo la Mikocheni ubatilishwe mara moja ili kulinda hadhi ya serika
 
viongozi wa dar wanaijua dar kuliko hao mawaziri wanaoingia madarakani wakitokea nachingwea huko wakidhani wanaijua dar, Dar ina wenyewe ! hata huyo JK na EL lazima wajue dar ina wenyewe juzt like baghdad had its people same thing applies 2 dar !
anna kilango malecela inasemekana hakushinda kihalali haya sasa tuone wanataka kumfungulia kesi !!!!!!!!
 
HAO DAILY NEWS KWA NINI WANAANDIKA HABARI NUSU NUSU? Tunawaomba waandike maswala yote yanayohusu hili eneo, sio kuandika vitu namna hii.

Kwa sababu bado sikubaliani na sentensi kama ishirini za hapo juu za lawama kwa waziri Magufuli. Hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria, kama kweli John Pombe Magufuli waziri amekosea kwa nini madiwani wa Kinondoni wasifungue kesi ili kumshitaki yeye binafsi na wizara husika.
 
Dua,
Uandishi wa namna hii ndio unawafanya watu wengi waidharau fani hii ya uandishi wa habari, na kuiona kama fani mbadala, kwa maana ya fani nyingine kushindikana.
Kweli, Mhariri mzima wa gazeti la serikali anaweza kuandika habari ambayo wala sio makala, kwa ushabiki mkubwawa namna hiyo??? Ushabiki ambao unaonyesha kila aina ya kulalia upande mmoja na ambao hauna uchunguzi.

Nimeshatangulia kupost huko awali kuhusu namna ambavyo naona inafaa kushughulikia suala hili.
Kwa maana ya kwamba Magufuli as an individual anaweza kuwa na mapungufu yake tele katika utendaji wake wa kazi, but hii haimaanishi maafisa wengine wa serikali kuu/mitaa wapo safi.
Inabidi wote wapimwe kupitia kipimo hichohicho atakachopimiwa Magufuli.

Kwamba kwanini hii bar iliruhusiwa kuwepo hapo kimakosa kwa miaka yote hii???
Hawa madiwani wasilete siasa katika suala hili, badala yake wafanye kazi.

Again....

Ujumbe kwa mwenye bar, kama wenye nchi yao wameona umekwishachuma vya kutosha na sasa inabidi uende zako, basi nawe uondoke utafute eneo lingine la kuwekeza. Haya uliyajua fika kama yatakufika, hata kama kwa kuchelewa.... You should have had Plan B brother.
 
HAO DAILY NEWS KWA NINI WANAANDIKA HABARI NUSU NUSU? Tunawaomba waandike maswala yote yanayohusu hili eneo, sio kuandika vitu namna hii.

Kwa sababu bado sikubaliani na sentensi kama ishirini za hapo juu za lawama kwa waziri Magufuli. Hakuna mtu ambaye yuko juu ya sheria, kama kweli John Pombe Magufuli waziri amekosea kwa nini madiwani wa Kinondoni wasifungue kesi ili kumshitaki yeye binafsi na wizara husika.
I won`t resign -Magufuli

2007-02-21 09:15:14
By Angel Navuri


The Minister for Lands, Housing and Human Settlement Development John Magufuli, yesterday said he would not resign over the issue of the Rose Garden plot as demanded by Kinondoni councilors in Dar es Salaam, because the owner was occupying the area legally.

Last week, the councilors demanded immediate resignation of Magufuli accusing him of issuing a building permit to Rose Garden owner without the consent of the Kinondoni Municipal authority.

However, Magufuli told journalists yesterday that the owner of Rose Garden had not trespassed because he was authorized by the Commissioner for L lands to occupy the area.

The councilors claim that Rose Garden, a famous bar in Kijitonyama suburb, has been built on a road reserve and want it pulled down.

Magufuli said if the Kinondoni Municipal authority wants to demolish the structures, it will have to compensate the owner since he followed all the laid down procedures to secure the plot.

Speaking at the municipal`s full council meeting which was chaired by the Kinondoni Municipal Mayor Salum Londa last week in Dar es Salaam, the councilors said the minister should step down for `skipping` the authority and issuing the permit without following the required procedures.


Waheshimiwa mmesikia magufuli alivyoeleza kuhusu hili swala lilivyo,sasa yupi mkweli?
 
Magufuli kufuta hati 2,500 za viwanja

2007-02-21 09:35:08
Na Emmanuel Lengwa


Serikali inafanya taratibu za kisheria za kufuta hati za viwanja zaidi ya 2,500 vilivyoko katika maeneo ya Tegeta, Boko na Jangwani Beach, jijini Dar es Salaam, ambavyo wamiliki wake wameshindwa kujitokeza.

Pamoja na hatua hiyo, serikali imeamua kubadili hati za viwanja vyote 14,531 katika maeneo hayo na kutoa hati mpya ambazo si rahisi kughushiwa.

Hayo yalitangazwa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. John Magufuli, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Waziri Magufuli alisema hati za zamani zilizokuwa zikitolewa kwa miaka 33, sasa zinabadilishwa na kuongezwa muda hadi kufikia miaka 99.

`Wamiliki wa viwanja vyote katika maeneo ya Mbezi, Tegeta, Boko na Jangwani Beach, wataandaliwa hati mpya ambazo ni vigumu kuzighushi. Hati hizi zitakuwa za miaka 99, badala ya hati za sasa za miaka 33, ili kulinda thamani ya ardhi kwa mmiliki,` alisema.

Aliongeza kuwa, hati hizo pia zitaingizwa kwenye mtandao wa kompyuta pamoja na nyaraka muhimu za mmiliki ili kuepusha utapeli na migogoro ya ardhi inayojitokeza mara kwa mara.

Waziri Magufuli alisema ili kufanikisha zoezi hilo, wamiliki watatakiwa kulipia asilimia tano ya thamani ya viwanja vyao.

Alisema baada ya utaratibu huo kukamilika katika maeneo hayo, hati hizo za muda mrefu zitaendelea kutolewa katika miji yote nchini.

Katika hatua nyingine, Waziri Magufuli amesema Serikali imeongeza muda wa miezi 36 kwa watu wanaomiliki viwanja katika maeneo hayo kuviendeleza.

Alisema muda huo ambao ni sawa na miaka mitatu umetolewa kwa wananchi waliofanya maendelezo hafifu kwenye viwanja vyao na hivyo Serikali kwa kuthamini nguvu zao, imeongeza muda huo ili wakamilishe maendelezo hayo.

Kuhusu viwanja ambavyo wamiliki wake hawajajitokeza na ambavyo bado havijaendelezwa, Waziri Magufuli alisema utaratibu wa kuvifuta kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999, utatekelezwa.

Na katika hatua nyingine, Waziri Magufuli ameagiza watu wote waliovamia viwanja na kujenga, kubomoa majengo yao mara moja.

Alisema ni kosa kisheria kuendeleza kwenye kiwanja chenye miliki halali ya mtu bila ridhaa yake.

Alisema wavamizi pia wanaweza kufanya makubaliano ya kisheria na wamiliki halali wa viwanja husika ili kutobomoa majengo yao na kuwalipa kiasi chochote watakachotakiwa kulipa kwa mujibu wa matakwa ya mmiliki halali wa kiwanja husika.

`Mvamizi abomoe jengo alilojenga kwenye kiwanja alichovamia ili apishe mmiliki halali kufanya maendelezo kwenye kiwanja chake, vinginevyo, mvamizi akubaliane kisheria na mmiliki huyo, ardhi hivi sasa ni mali,` alisisitiza.

Wakati huo huo, Waziri Magufuli, amesema hajiuzulu ng?o kuhusiana na sakata la eneo la wazi la ulipo mgahawa wa Rose Garden, jijini Dar es Salaam kwa kuwa linamilikiwa kihalali na mmiliki wake.

Waziri Magufuli aliyasema hayo alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusiana na tamko la baadhi ya madiwani wa Manispaa ya Kinondoni waliomtaka aachie ngazi kwa madai kwamba, aliingilia utendaji wa baraza hilo.

Alisisitiza kuwa, eneo hilo ni mali halali ya mmiliki wa mgahawa huo kwa vile anayo hati aliyopewa kisheria.

Alisema suala la yeye kujiuzulu haliwezekani kwa vile amepewa kuiongoza wizara hiyo na kukuta tayari mmiliki huyo akiwa na hati halali ya kiwanja hicho.

`Mgahawa wa Rose Garden una miaka 17 pale, mimi nina mwaka mmoja tu kwenye wizara hii, sasa iweje waseme nimemgawia kiwanja hicho na walikuwa wapi kumvunjia tangu zamani?` alihoji Waziri Magufuli ambaye amerejea hivi karibuni kutoka nchini Ujerumani alikokuwa amelazwa akitibiwa.

Alisema yeye alichokifanya ni kuona haki inatendeka kwa kuwa aliingia madarakani na kumkuta mmiliki wa mgahawa huo akiwa na hati halali ya kiwanja hicho.

Waziri Magufuli alisema anamshangaa mmiliki wa mgahawa huo kwa kutowashtaki watu wanaomzuia kufanya biashara zake bila sababu za msingi.

`Namshangaa mmliki wa mgahawa wa Rose Garden kwa kutowashtaki mahakamani watu wanaomkwaza kufanya kazi zake? Hata akienda mahakamani, mimi na Kamishna wa Ardhi ni mashahidi wake,`alisisitiza.

Pia Waziri Magufuli alisema ni Wizara pekee iliyopewa mamlaka kisheria ya kuidhinisha matumizi ya ardhi nchini kote.

`Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999, inampa Waziri wa Ardhi mamlaka ya kuidhinisha au kubadili matumizi ya ardhi katika vijiji na miji yote nchini, hivyo hata kama ningefanya hivyo, bado ningefanya kwa mujibu wa sheria hiyo,` alisema.

Alisema analishangaa pia Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kinondoni kuvalia njuga kiwanja hicho pekee ambacho kinamilikiwa kihalali, wakati zipo nyumba nyingi zimejengwa kwenye hifadhi ya barabara ndani ya manispaa hiyo.

Alitoa mfano wa nyumba zilizojengwa kando ya barabara ya Morogoro kuanzia Ubungo mpaka kwenye daraja la Kibaha.

`Nawashangaa. Sheria inasema hifadhi ya barabara ya Morogoro ni futi mia tatu kila upande wa barabara. Zipo nyumba nyingi kuanzia Ubungo hadi Kibaha darajani zimejengwa kwenye hifadhi ya barabara hiyo, mbona hizo hawazigusi?` Alihoji Waziri Magufuli.

Alisema yeye yupo kwa ajili ya kusimamia sheria na kutetea haki kwa watu wote bila kujali mwenye mali au asiyekuwa nazo.

Mwishoni mwa wiki, Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni lilimtaka Waziri Magufuli kujiuzulu wakimtuhumu kuwa aligawa eneo la wazi ulipojengwa mgahawa wa Rose Garden.

SOURCE: Nipashe

HAYA TULISEMA KWAMBA MADIWANI WAMEKURUPUKA TUKAAMBIWA WANAFANYA KAZI,SASA WALETE UDHIBITISHO!FACT ZOTE MAGUFULI AMEZIWEKA!
 
KM,
Asante kwa taarifa moto.

Mwenye macho haambiwi tazama, Magufuli kasema yote hapo juu. Kama mwenye Rose Garden anakibali halali toka wizarani, then wanaotakiwa kujiuzulu/kufukuzwa kazi wapo lukuki.

Hawa madiwani aibu tupu na siasa zao za kukurupuka, za mitaani.
What a shame.
 
Katika mawaziri wote hakuna waziri mchapakazi kama Magufuli. Hata kama ana mapungufu yake lakini kama ni utendaji anao tena wa kuungwa mkono.

Hebu tujiulize ni waziri gani ambaye ameweza au anayetumia data kuzungumzia issue za wizara yake. Huyu jamaa ni kichwa kweli kweli, halafu anakaa ofisi na siyo kwenda Airport kupokea viongozi wa Serikali.

Tangia atoke Wizara ya Miundombinu, hakuna barabara hata moja iliyojengwa au inayoendelea kujengwa kwa speed ya kuridhisha.

kuna watu wana mifupa na Magufuli kwa sababu anawaumbua kwa uchapakazi wake.
 
hapa ni fitina tu. haiwezekani road reserve ikawa bar ya rose garden tu. mbona kuna majengo ya maghorofa kutoka rose garden mpaka kona ya kuelekea tpdc na hawasemi kama yako ndani ya reserve?
 
Maamuzi ya Magufuli yaibua maswali mengi

*Apuuza ushauri wa Makamba, manispaa ya Kinondoni

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, John Magufuli, anaelekea kuanzisha mgogoro wa kiutendaji katika utawala wa serikali ya awamu ya nne.

Tayari kuna mvutano baina ya Magufuli na Manispaa ya Kinondoni pamoja na wawekezaji ambao wamemilikishwa viwanja kwa njia halali na za kisheria.

Hali hii mpya imeibuka kutokana na Waziri Magufuli kubariki kubuniwa kwa viwanja kadhaa eneo la Mikocheni, kikiwamo ilipo baa maarufu ya Rose Garden.

Mgogoro huu unahusisha Manispaa ya Kinondoni ambayo imetamka wazi kwamba Waziri huyo amepotoka kwa kubariki viwanja hivyo ambavyo vinaelezwa kubuniwa kinyume cha sheria.

Mbali na mvutano na Manispaa, pia wenye viwanja wengine wamejikuta wakifungiwa njia ya kufika kwenye eneo lao kutokana na kubuniwa kwa viwanja hivyo kwenye eneo la akiba ya barabara.

Mmoja wa watu ambao wamejikuta wakiathirika na uamuzi wa Magufuli wa kubariki viwanja namba 948 hadi 951, ni Kampuni ya ZEK Group ambayo ilinunua viwanja namba 717/5 na 717/4 kutoka Simu 2000 Ltd kwa ajili ya kuwekeza mradi mkubwa wa mabilioni ya shilingi.

Akizungumzia suala hilo jana, Mwenyekiti Mtendaji wa ZEK Group, Zadock Koola, alisema pamoja na kumweleza Waziri Magufuli juu ya mkanganyiko uliokuwako juu ya kubuniwa kwa viwanja hivyo, ameamua kuvitambua bila hata kujibu barua waliyomwandikia mwaka jana, wakimuomba kuingilia kati mgogoro huo.

Hatua ya Magufuli ya kuvitambua viwanja hivyo juzi ni majibu kwa Baraza la Madiwani la Kinondoni chini ya Meya wao, Salum Londa, ambalo lilimtaka awajibike kutokana na kuvamiwa kwa eneo la wazi la barabara ambalo limemegwa na kupimwa viwanja kinyume cha taratibu za sheria ya ardhi.

Madiwani hao wamekwisha kusisitiza mara kadhaa kwamba viwanja hivyo pamoja na ilipo baa ya Rose Garden ni batili na kuna mlolongo wa nyaraka unaoonyesha kwamba eneo hilo ni la barabara lakini liligeuzwa viwanja na watu walioshirikiana na maafisa wa serikali.

Kulingana na mlolongo wa nyaraka zilizoko, mmiliki wa baa ya Rose Garden, Damas Assey, aliomba kibali kutoka Kampuni ya Simu Tanzania, ofisi ya Mkurugenzi wa Kanda ya Dar es Salaam Kaskazini, kutumia eneo iliko baa hiyo mwaka 1995.

Ofisi hiyo kwa barua ya Novemba 2, 1995 ilimruhusu Assey kuendesha shughuli kwenye eneo hilo likiwa ni mbele ya viwanja namba 717/5 na 717/4 ambako kiwanda cha uchapaji cha TTCL kilikuwako wakati huo, lakini ikamkataza kujenga jengo la kudumu. Wakati huo alikuwa akifanya biashara ya kuuza maua.

Hata hivyo, baada ya Simu 2000 Ltd kutaka kuuza eneo hilo na kuiomba Manispaa ya Kinondoni kuondoa vibanda vyote vilivyokuwa mbele ya viwanja hivyo kwa sababu wawekezaji walikuwa wakisita kuvinunua, Assey alifungua kesi mahakamani kuzuia kuvunjwa kwa baa hiyo.

Wakati kesi ikiendelea mahakamani, kwa nyakati tofauti na baada ya uchunguzi wa kina, Ofisi ya Mkurugenzi wa Upimaji Ramani Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Julai 12, 2004 ilimwandikia Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ikimwagiza kwamba utaratibu wa kubuni na kupima viwanja kikiwamo 951 iliko baa ya Rose Garden haukufuatwa na kwamba kiwanja hicho kifutwe na mawe ya mpaka (beacons) yang’olewe.

Nayo Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ikiwa imepokea maelekezo ya Wizara ya Ardhi, Novemba 18, 2004 ilimwandikia Assey ikimtaarifu kwamba kiwanja alichojenga baa ya Rose Garden ni batili kwa sababu kimebuniwa kwenye eneo la hifadhi ya barabara na kumtaka aondoke kwenye eneo hilo.

Barua hiyo ya Manispaa pia ilihusu viwanja namba 948 – 951 ambavyo vilikuwa vimepimwa kinyume cha taratibu na kwa maana hiyo hati zake zilikuwa zimefutwa.

Pamoja na barua hizo mbili, aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye sasa ni Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, aliingilia kati mgogoro huo Juni 4, 2004 kwa kumtaarifu aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa, E. Berege, kwamba eneo la barabara limevamiwa na kubuniwa viwanja hivyo kinyume cha sheria. Alimtaka kuhakikisha kwamba majengo yote ya kudumu yaliyojengwa kwenye eneo la barabara yanabomolewa na taarifa kuwasilishwa kwake.

Hayo yakitokea, Assey alifungua kesi namba 23/2006 Mahakana Kuu kitengo cha ardhi kupinga kuhamishwa eneo hilo, lakini wakati huo huo akisukuma maombi ya kumilikishwa kiwanja hicho kisheria.

Kiwanja hicho namba 951 mwaka jana katikati kilipewa hati miliki wakati huo shauri likiwa bado mahakamani, na Waziri Magufuli akijua kwamba Manispaa ya Kinondoni, Mkurugenzi wa Upimaji Ramani wa Wizara yake na hata Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kila mmoja kwa wakati tofauti na kwa uchunguzi unaojitegemea walibainisha kuwako na utata mkubwa wa viwanja hivyo, alibariki miliki hiyo.

Uamuzi wa juzi wa Mafuguli kuhalalisha viwanja hivyo, huku mwenyewe alipokuwa Waziri wa Ujenzi kwenye utawala wa Rais Benjamin Mkapa akiwa amepigania maeneo ya barabara yasivamiwe na kushiriki katika bomoabomoa zilizoaacha maelfu ya watu bila makazi, umemfungua katika sura mpya ambayo haijajulikana.

Alipochaguliwa kuwa Waziri wa Ardhi na Mandeleo ya Makazi, Magufuli, alitoa ilani kwamba wote waliovamia maeneo ya wazi na kumilikishwa kinyume cha sheria watanyang’anywa na kuonya kwamba hakuna mtu anayeruhusiwa kumilikishwa maeneo ya wazi bila ya kibali cha Waziri wa Ardhi.

Kauli hiyo haioani na uamuzi wake wa sasa ambao si tu umemweka kwenye mapambano na mamlaka nyingine za wananchi, Baraza la Madiwani, bali pia na watedaji ndani ya wizara yake mwenyewe.

Wakati huo huo, Andrew Msechu anaripoti kuwa Waziri Magufuli amesema ofisi yake iko tayari kuungana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro, kuhakikisha inawashughulikia matajiri walafi wanaodhulumu ardhi ya wanyonge.

Alitoa kauli hiyo wakati wa kuapishwa kwa Baraza la Ardhi la Manispaa tatu za Mkoa wa Dar es Salaam jana, ambapo Magufuli alielezea kusikitishwa kwake na namna matajiri wanavyotumia uwezo wao kifedha kudhulumu viwanja na ardhi za wanyonge, baadhi wakiwadhulumu hata wajane na yatima.

Alisema kwa hali ilivyo sasa, ni lazima haki itendeke na kwamba hata kama tajiri au mwenye mamlaka fulani alivamia eneo na kujenga ni lazima aondoke iwapo itathibitika kuwa kwa namna yoyote alihusika kuingilia haki za watu wengine.

"Hawa matajiri jeuri wanaotumia uwezo wao kuvamia hawatakiwi kupewa nafasi, tumieni uwezo wenu kuhakikisha kuwa haki inatendeka, hata kama walishajenga maghorofa katika maeneo hayo waondoke, la waelewane na wale wenye maeneo hayo," alisema.

Aliongeza kuwa katika kutatua migogoro hiyo, hata pale itakapobidi serikali kushtakiwa katika mabaraza ya Ardhi yaliyoundwa nchi nzima na kushindwa basi ishindwe.

Magufuli aliagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha zinawashughulikia kikamilifu maafisa ardhi ambao kwa namna yoyote walitajwa kuhusika katika kuzalisha migogoro yote iliyowasilishwa katika Tume Mabaraza yaliyoundwa na Rais kufuatilia migogoro ya ardhi ambayo tayari taarifa zake zilishatolewa.

Magufuli alitoa agizo hilo mara baada ya kupokea kilio cha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, aliyelalamikia maafisa ardhi waliopo chini ya Wizara inayoongozwa na Magufuli kwa kuhusika kwao katika kuzalisha migogoro ya ardhi.

Mabaraza hayo ya Wilaya yaliundwa kwa dharura na Rais Jakaya Kikwete mwaka jana, ambayo yalikuwa yakisimamiwa na Halmashauri za Wilaya chini ya uenyekiti wa Mameya nchi nzima.

Alielezea kushangazwa kwake na ukubwa wa tatizo la zaidi ya migogoro 14,500 iliyopo Wilayani Kinondoni ambayo tayari inashughulikiwa na Wizara yake, huku maafisa wa ardhi wakiwa wanahusika zaidi katika ugawaji wa viwanja kwa watu zaidi ya mmoja.

Akitua mzigo wake kwa Waziri Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, alielekeza kilio chake kwa kwa maafisa Ardhi waliopo chini ya Waziri Magufuli ambao kwa kiasi kikubwa wameonekana kuwa chanzo cha migogoro mingi ya ardhi iliyopo katika jiji la Dar es Salaam.

Kandoro alisema Manispaa ya Kinondoni pia ndiyo inayoongoza kwa migogoro ya ardhi iliyofikishwa ofisini kwake, ikiwa na migogoro 1,028, ikifuatiwa na Temeke 300 na Ilala 209.

Wajumbe wa mabaraza hayo ni Kenneth Wallace, Salma Dossi na aliyewahi kushika wadhifa wa ukuu wa mkoa katika baadhi ya mikoa nchini Mary Chipungahelo ambao watakuwa katika Baraza hilo Manispaa ya Ilala.

Katika Manispaa ya Kinondoni yumo aliyewahi kuwa Waziri wa Nyumba, Tabitha Siwale, Heavenlight Bethuel na Ruth Lugarisha, na Temeke wakiwa ni Sautiel Kulaba, Daniel Mtagula, Azid Ulembo, Marina Mlunde na Rhoda Kahatano.

source: Mwananchi
 
Well,
Hapa Magufuli kachukua sheria mkononi na baada ya taarifa hii sasa yaonyesha ukweli uko wapi.
Siwezi kushangaa kitu wala kuwa mshabiki ktk serikali hii ya chukua chako mapema!
 
KM,
Nimesoma hiyo habari hapo juu nakuelewa kwanini Magufuli analalamikiwa kama Magufuli. Kumbe hati ya kiwanja cha RG ilipatikana mwaka jana tu, basi kweli tunao viongozi.

Haihitaji mtu kuwa engineer kujua kwamba sehemu kubwa ya bar ya RG ipo ndani ya hifadhi ya barabara, na hivyo uhalali wa kutaka iondolewe.

Hata hivyo, swali la kujiuliza ni Je, baada ya hii bar kuvunjwa nini kitafanyika hapo kwenye kiwanja husika????
Kama hiyo bar imesurvive miaka yote bila madhara kwa jamii, basi kwanini ivunjwe sasa????

Kuna nyumba kadhaa katika barabara hii ambapo wenye nyumba wameweka mbele ya nyumba zao (ktk eneo la hifadhi ya barabara) makontena ya biashara za bar, kuuza nguo, salons n.k., Je na hawa nao watavunjiwa maeneo yao ya biashara sambamba na RG, maana wapo eneo moja na wote wanavunja sheria????

Isije ikawa mambo ya kuwanyanyasa wawekezaji wadogo wazawa kwaajili ya kuserve interests za wawekezaji wakubwa wakigeni.

Hii issue ni ya kufuatilia mpaka kieleweke.
 
Zinduka,

Sidhani kama watu wengine walipeleka pia malalamishi yao kortini..

Huyu Magufuli kitu kimoja tu, yaonyesha ana sura nyingi sana pamoja na kwamba ni mfanyakazi mzuri. Mambo yote yaliyosemwa sio kwamba kasingiziwa, yalitokea lakini leo hii tena tunaona sura tofauti inayolinda mtu mmoja hali Magufuli alibomoa vibanda kibao akiwa waziri wa Ardhi. haya mara tunaona tena magufuli anatetea wanyonge kuhusu viwanja vyao dhidi ya ambalo ni jambo zuri sana.
kaniacha hoi!... napenda sana kumwamini yeye lakini kama mpango wenyewe ndio usanii itakuwa kazi kubwa.
Vizuri akitueleza sababu alizofikia yeye kutoa kibali wakati mahakama bado haijatoa uamuzi wake ktk kesi aliyofungua Assey!...
 
KM,
Nimesoma hiyo habari hapo juu nakuelewa kwanini Magufuli analalamikiwa kama Magufuli. Kumbe hati ya kiwanja cha RG ilipatikana mwaka jana tu, basi kweli tunao viongozi.

Haihitaji mtu kuwa engineer kujua kwamba sehemu kubwa ya bar ya RG ipo ndani ya hifadhi ya barabara, na hivyo uhalali wa kutaka iondolewe.

Hata hivyo, swali la kujiuliza ni Je, baada ya hii bar kuvunjwa nini kitafanyika hapo kwenye kiwanja husika????
Kama hiyo bar imesurvive miaka yote bila madhara kwa jamii, basi kwanini ivunjwe sasa????

Kuna nyumba kadhaa katika barabara hii ambapo wenye nyumba wameweka mbele ya nyumba zao (ktk eneo la hifadhi ya barabara) makontena ya biashara za bar, kuuza nguo, salons n.k., Je na hawa nao watavunjiwa maeneo yao ya biashara sambamba na RG, maana wapo eneo moja na wote wanavunja sheria????

Isije ikawa mambo ya kuwanyanyasa wawekezaji wadogo wazawa kwaajili ya kuserve interests za wawekezaji wakubwa wakigeni.

Hii issue ni ya kufuatilia mpaka kieleweke.
Hata mimi napata picha nyingine Lakini unajua hata waandishi wetu wanatupotosha sana Sasa kwanini magufuli alipotoa ufanunuzi huo jana hawakumuuliza wakati wa ile Press conference pale pale kuhusu hili ambalo wamekuja kuliandika baada ya Press Conference ambapo waandishi wote walikuwa na nafasi ya kuuliza hata hili waliloliandika?Hapa kuna kitu hakipo wazi kwetu wote,Ngoja liendelea hili sakata ukweli dhahiri utajulikana.Inaonyesha Madiwani na Halmashauri wana waandishi wao na kinachonifanya niseme hili ni ile hali ya kuwa na fursa ya kuuliza swali kama hili na kumueleza Waziri kinagaubaga kwamba unapotosha umma swala liko hivi na ushahidi ni huu kwani waliacha hiyo nafasi ili hali walikuwa nayo wakati wa Press Conference yake?
 
Jamaa ni mchapa kazi lakini hapa kaliboronga!! no doubt. Hatuwezi kuhalalisha makosa eti kwa sababu mtu amekuwepo 17 years pale, kuna watu Kilwa Road katika mazingira hayo hayo ya miaka 17 na bado wamevunjiwa tena sio Baa peke yake!!!! nyumba za kuishi pia. Kwanini Rose garden iwe special?? Kijana vunja majengo yako, tafuta sehemu nyingine uiite "The New Rose Gaeden"

Complications naanza kuziona inapoingia Simu 2000
 
kwa watoto wa mjini wanaovinjari pale ROSE GARDEN wanajua rose garden imekuwepo tangu zamani pale nje ya uzio wa karakana za posta na simu...miaka ya karibuni lile eneo limenunuliwa na bwana ZK ambaye anataka kina MLATIE watoke pale nje ya eneo alilonunua ili aweze kujenga mradi mkubwa wa mamilioni ya dola utakaoajiri watu 3,000.

sasa huu ugomvi umezusha tag of war kati ya watu wanaomtetea MLATIE na wapambe na marafiki wa ZK...hakuna anayetaka kushindwa,sasa naona hawa manispaa wanamtetea ZK offcourse wanayo sababu ,huyu ni mmoja wa chanzo chao kizuri cha mapato kupitia mrahaba na kodi za mabango anazowalipa kila mwezi,pili amewashawishi kwa business plan na artistic impression aliyowapa ya kuendeleza hilo eneo....na lazima hapa mkumbuke kuwa uhusiano wa ZK na manispaa umepanuka hadi wamempa kile kituo maarufu kipya CHA MWENGE akiendeshe kibiashara ili awalipe mrahaba.

Bw pm, kweli hapa ulikuwa wanena reality ya jijiletu. ZK kafanya kweli tena ni baada ya kusikia Magufuli akisema kwanini Rose Garden hawalistaki jiji na madiwani....kwali hapa pana kutunishiana misuli tena haswaaaa!

Rose Garden saga: Local investor to go to court

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam


Local company ZEK Group Limited has said it will contact its lawyers on what legal action to take following reports that the Minister for Lands, Housing and Human Settlements Development, John Magufuli, has legalised the popular Rose Garden Bar and Restaurant along TPDF Road in Dar es Salaam’s Mikocheni suburb to continue operating despite allegedly being positioned on a road reserve.

ZEK Group Limited chairman and chief executive officer (CEO) Zadock Koola said in the city yesterday that the company was now considering outright litigation because the minister’s decision had been made while there was a pending legal dispute in court over the site.

’’Depending on what my lawyers will advise me, I am intending to take appropriate action because I feel that the minister has not done us justice,’’ said Koola.

The court dispute revolves around claims by the company that the roadside pub is holding back its plans to build a proposed commercial and retail precinct dubbed ’Dar Village’ because it is blocking the front of the property earmarked for the project.

According to ZEK, the estimated 20bn/- Dar Village project has the potential to create over 5,000 new jobs. The company bought the property covering 8.7 hectares at the Tanzania Telecommunications Company Limited’s former Kijitonyama Printing Unit from Simu2000.

Speaking to THISDAY in an interview yesterday, Koola said the minister’s decision to legalise the continued operations of Rose Garden Bar and Restaurant on the proposed project site amounted to frustrating the intended investment.

The ZEK Group CEO said on October 30 last year, he wrote a letter to Magufuli explaining the dispute surrounding the site, ’’but he has never replied to me todate’’.

He said he was shocked to learn through the press that the minister has now approved issuance of a letter of occupancy to the owners of Rose Garden while the matter is still pending in court, an action which he said amounted to contempt of court.

The proposed Dar Village project on the disputed Plot 717/5 is intended to include a 52-bedroom hotel, a three-storey office building and a health club, employing more than 5,000 locals.

Koola said the delay in implementing the project was also discouraging potential financiers in the process of funding the development of the planned property.

He said some banks have shown interest to finance the project, while anchor tenants including the South African Shoprite and Game Store supermarket chains and Nakumatt of Kenya had already visited the project site and interested in opening outlets there.

But all these have expressed discouragement with the continued delay in implementing the project, he added.

It is understood that the Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Development issued a letter of offer to the owners of Rose Garden Bar and Restaurant in June last year. However, Kinondoni municipal council authorities maintain that the joint is built on a road reserve, thus contravening rules and regulations governing the Dar es Salaam City Master Plan.

The then Kinondoni district commissioner, Athuman Mdoe, said last July that he was not aware of the letter of offer issued by the ministry, and maintained that the area was a road reserve.

And in a November 2004 letter to the Kinondoni municipal director, the then Dar es Salaam regional commissioner Yusuf Makamba ordered the demolition of structures along the TPDF Road, saying the area should be maintained as a road reserve.

Prof Issa Shivji, a retired professor of law with the University of Dar es Salaam and a recognised expert on land issues, told THISDAY last year that the government should not have rushed to issue a letter of offer to the owners of Rose Garden Bar and Restaurant while there was a pending case at the High Court’s Land Division involved the Kinondoni municipal council and the Rose Garden owners.

’’The Ministry of Lands, Housing and Human Settlements Development should have waited until the court has made a ruling on the case. Why the rush?’’ Prof Shivji remarked.

He said should the Kinondoni municipal council authorities feel bypassed by the ministry, they could as well take legal action against the ministry.

However, Minister Magufuli told a press conference in the city on Tuesday this week that the popular roadside pub was not sitting on any road reserve as alleged by the Kinondoni municipal council authorities.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom