yusufummaka
Member
- Apr 7, 2012
- 30
- 20
Hongera "Mjesani" kwa kuipenda club yetu ya Yanga hadi kutamani kuiongoza katika ngazi yake ya juu. Ninakufahamu sana John tangu ulipokuwa Tanga kwenye mashamba ya Mjesani na Mwinduro, shuleni, chuoni na Maramba JKT. Tulikuwa marafiki wa hapa na pale, nakujua ulivyokuwa mbishi wa kila kitu kinavyojadiliwa mbele yako. Lakini hili la yanga waachie wenye pesa waindeshe klabu. Mpira wa leo duniani kote unahitaji fedha nyingi tofauti na zama zile za akina Daud Salum, Kampila na Mahadhi. Wachezaji wa zamani walikuwa wanatoka kwenye kambi za mashamba ya mkonge, tumbaku, mpira na kakao. Hivi leo wachezaji wanatoka Nigeria, Ghana, Kongo, East Africa, Zambia, etc. Hawa wahataka pesa nyingi pamoja na kocha wao. Lazima kiongozi pamoja na mapenzi ya klub pia sharti awe na fweza. Angalia club za Ulaya zote zinavyokabidhiwa kwa matajiri kutoka kwa viongozi wazawa na mashabiki. Acha, acha, acha kabisa habari yako hiyo, wewe huna fweza, utategemea kutembeza bakuri na kupiga magoti kwa matajiri. Wanachama na mashabiki wa Yanga tupo wengi kweli, lakini hatuna kitu, tunashindwa hata kumudu milo 3 kamili kwa siku itakuwa kuchangia club? Najua unaipenda Yanga lakini............